MWALIMU MKUU ALIYESHIRIKIANA NAYE APEWA ONYO KALI
BAADA ya Mtandao huu kuibua tuhuma na mwanafunzi Monica Masunga kufanya mtihani wa darasa mara mbili katika shule tofauti mbili zilizo kata moja mwanafunzi huyo sasa amefutiwa matokea ya mtihani wa darasa la saba mwaka huu 2014.
Uchunguzi wa Mtandao huu ulibaini kuwa mwanafunzi Monica Sayi Masunga (15) ambaye baba yake ni Mratibu Elimu kata katika kata ya Kakubilo
alimaliza darasa la saba mwaka jana katika shule ya msingi Kakubilo ambapo bada ya matokea kutoka hakuwa amefaulu mtihani huo .
Matokeo ya Monica katika mtihani wa mwaka jana yalionesha Somo Kiswahili alipata alama C,Kiingereza D, Maarifa alama C, Hisabati D, na Sayansi alipata alama D hivyo wastani wake kwa masomo yote ukiwa alama D ambao haukumwezesha kufaulu.
Uchunguzi zaidi ulibaini kuwa mwanafunzi huyo aliingizwa kinyemela na kusajiriwa kuwa mtahiniwa wa mtihani wa darasa la saba mwaka huu 2014 akifanya mtihani huo katika shule ya msingi Kawawa ambako alisajiriwa kwa jina la Monika silya Masunga akitofautishwa kidogo na jina la mwaka jana alilofanyia mtihani.
Mwanafunzi huyo alionekana shule ya msingi Kawawa siku ya mtihani ambako muda wote kabla ya mtihani alikuwa nyumbani bila kusoma hali iliyowafanya hata wanafunzi wa shule hiyo kushangaa kuwa na mtahiniwa mwenzaoambaye hawakuwahi kumuona katika shule hiyo ,walimu kwa maelekezo ya Mratibu huyo walionywa kutomtilia shaka.
Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Geita baada ya chapisho la habari hii ulilazimika kutuma ujumbe wa maafisaelimu wawili Stephene Mase Afisaelimu taaluma na Heri Bihemo Afisaelimu ya Watu wazima ambao walifika shule ya msingi Kakubilo alikofanyia mtihani mwaka janana kisha shule ya msingi Kawawa alikofanya mtihani mwaka huu.
Walibaini viashiria vya kuwepo udanganyifu na ukiukwaji mkubwa maadili kutokana na kukuta mwanafunzi huyo kuonekana kufanya mtihani mara mbili kinyume kabisa na sheria ya elimu ya mwaka 1978.
Baada ya kufikisha tarifa hiyo Afisaelimu wa wilaya Deus Seif alilazimika kuunda tume kutoka Ofisi ya ukaguzi wa shule kwa ajili ya kwenda kufanya uchunguzi wa kina kisha kutoa majibu ya uchunguzi wa kwa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya .
Uchunguzi wa tume hiyo ulibaini kuwa mwanafunzi huyo ni kweli alifanya mtihani mara mbili katika shule mbili tofauti kwa maagizo ya Mratibu Elimu Kata Masunga akiwa baba wa mwanafunzi huyo kwa kubadilisha taarifa ili ionekane Monica alianzia darasa la kwanza s/m Kawawa .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri ya wilaya ya Geita Ally Kidwaka alisema amepokea taarifa ya uchunguzi huo kwa masikitiko makubwa kutokana na jinsi elimu inavyochezewa tena na watu waliopewa dhamana ya kuongeza sekta hiyo muhimu kwa ustawi wa taifa letu.
Alisema tume ilipomhoji mwalimu mkuu aliyekuwa shule ya msingi Kawawa Chobabona Michael ambaye kwa sasa alihamishiwa shule ya msingi Njingami ambaye ndiye alimsajiri mwanafunzi huyo kinyemela ili aweze kufanya tena mtihani mwaka huu alikiri mbele ya tume kufanya udanganyifu huo.
Aidha Mkurugenzi huyo alisema hata mratibu huyo wa elimu naye alikiri mbele ya tume kutoa maelekezo kwa mwalimu mkuu wa shle ya Kawawa kuhakikisha mtoto wake Monica anasajiriwa kufanya mtihani akikiri kukiuka taratibu za kielimu ambako alimwelekeza Afisaelimu wa wilaya kuchukua hatua kali.
Alipofuatwa na Mtandao huu kuelezea jinsi alivyopokea matokea ya uchunguzi huo Afisaelimu Deus Seif alilimwagia sifa Mtandao huu kwa kuifumbua macho wilaya hiyo juu ya hujuma zinazofanywa za kuzalisha wasomi feki na kufanya wasiostahili kufaulu mitihani.
Alisema maamuzi yaliyochukuliwa dhidi ya Mratibu elimu kata huyo ni kwamba amevuliwa wadhifa wake huku mwalimu Chobabona aliyekubali kukiuka sheria ya Elimu amepewa barua ya onyo kali ,akisema pia kuwa mwanafunzi huyo ambaye alikuwa amefaulu matokea yake yamefutwa.
Matokeo ya mwanafunzi Monica ambaye pia alikiri kuoneshwa majibu ya mtihani katika mtihani wa mwaka huu Kiswahili ana alama B, Eglish D,Maarifa C, Hisabati D na Sayansi ana alama C Wastani wake wa jumla ni alama C.
Monica alianza darasa la kwanza katika shule ya msingi Buligi mwaka 2007 kabla ya kuhamia shule ya msingi Kakubilo mwaka 2011 akiwa darasa la tano ambako aliandikishwa kwa namba 4548 ambapo mwak jana alikwa miongoni mwawanafunzi 78 wa shule ya msingi kakubilo waliofanya mtihani akitumia namba ya mtihani PS 2404051/062.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kakubilo Magessa Mashabala alisema Monica alikuwa mwanafunzi wake tokea 2011alipohamia hapo akitokea shule ya msingi Buligi alikoanzia darasa la kwanza ambako kabla ya kupandishwa cheo baba yake alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Buligi.
Aliposajiriwa kinyemela shule ya msingi Kawawa Monica alipewa namba za usajiri 530 na kuonekana kuwa alianzia hapo darasa la kwanza hadi darasa la saba namba yake ya mtihani mwaka huu ikiwa ni PS 2404064/O83.
Kitabu cha mahudhurio ya kila siku ya wanafunzi cha shule ya msingi Kawawa kilionesha Monica amehudhuria siku zote shuleni bila kukosa hata siku moja huku ikionesha wazi kuwa kilitkitabu kipya cha mahudhurio na kumwingiza Monica kisha kuweka alama ya vema kuonesha hakuwahi ukosa shule hata siku moja.
Mbaya zaidi mwanafunzi huyo kwa maelekezo ya baba yake yake aliaidiwa kufanya mtihani ambap alikiri kupewa majibu ambayo ndiyo yalimsaidia kufaulu mtihani wa mwaka huu.
Alipozungumza na Mtandao huu Monica alikiri kupewa majibu ambapo alisema yeye baada ya kufeli mtihani mwaka jana akijijua uwezo wake kiakili kuwa mdogo alimuomba baba yake kumtafutia cherahani ili mapeleke akijifunze ushonaji.
Alisema baba yake alimwambia asubiri ataenda kufanya tena mtihani na kwamba angesaidiwa japo alisema alimsihi baba yake kuwa yeye hawezi kabisa kuyamudu masomo ya sekondari.
"Ilipofika mwezi wa saba mwaka huu baba aliniambia niende nikipime sare ya shule na nijiandae kufanya mtihani katika shule ya msingi Kawawa ilipobaki siku ya mtihani nilikuta tayari nimeandaliwa dawati langu nikaingia chumba cha mtihani ambapo niliuwa naletewa majibu " alisema Monica .
0 comments: