Watatu wafukiwa na kifusi wakichimba madini wilayani Kahama mkoani Shinyanga
Wachimbaji watatu wa madini ya dhahabu ya Kalole kata ya Lunguya wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamefariki dunia baada ya kufukiwa na udongo wakiwa kwenye shimo la dhahabu wakitafuta dhahabu.
Kwa
mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus
Kamugisha alisema tukio hilo limetokea Januari 7,2015 saa 12 asubuhi
katika machimbo madogo ya dhahabu ya Kalole kata ya Lunguya,tarafa ya
Msalala wilayani Kahama.
Aliwataja waliofariki kwa kufukiwa kwenye shimo hilo la dhahabu kuwa ni Kulwa
Magele(20) mkazi wa Shishani wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Ihalu
Maheme(23) mkazi wa Idisa wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu na Lameck
Frank(22) mkazi wa Nzega mkoani Tabora.
Kamanda
Kamugisha alisema vijana hao ambao ni wachimbaji wadogo wa madini
waligundulika wakiwa wamekufa ndani ya shimo la kuchimbia dhahabu na
inaelezwa kuwa waliingia kwenye shimo hilo ambalo halitumiki kwa nia ya
kuchimba dhahabu ndpo likabomoka na kuwafukia na kusababisha vifo vyao papo hapo.
Wakati huo huo mwanamke aitwaye Sayi Shitunguru(50) mkazi wa kijiji
cha Buruma kata ya Isaka wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ameuawa kwa
kupigwa kitu kizito kichwani na watu wasiofahamika akiwa nyumbani kwake.
Kamanda
Kamugisha alisema tukio hilo limetokea Januari 7,2015 saa 1 asubuhi
ambapo mwanamke huyo akiwa nyumbani kwake alivamiwa na mtu/watu
wasiojulikana kasha kumpiga na kitu kizito kichwani na kusababisha kifo
chake papo hapo.
Alisema chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na jeshi la polisi linaendelea kufanyan uchunguzi ili kubaini chanzo chake.
Hata hiyvyo alisema tayari wanamshikilia mtu mmoja aitwaye John
Jota(33) mkazi wa Kazungu wilayani Kahama kwa mahojiano zaidi huku
akiwataka wananchi kushirikiana na polisi ili kusaidia kukamatwa kwa
wahusika wa mauaji hayo.
0 comments: