Kipa wa Yanga Juma Kaseja.
YANGA imetangaza
rasmi kuachana na kipa Juma Kaseja lakini Championi Ijumaa linafahamu
ukweli kuwa klabu hiyo imepanga kumfungulia mashitaka ya kumtaka alipe
shilingi milioni 400, kutokana na kuvunja mkataba.
Akitangaza
kwa waandishi wa habari jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa
klabu hiyo Jerry Muro alisema kuwa Kaseja ndiye aliyevunja mkataba na
klabu hiyo kutokana na kutoonekana mazoezini kwa zaidi ya saa 48, hivyo
kuvunja kipengele katika mkataba wake.
“Yanga
inatangaza rasmi kuwa haitakuwa na kipa Juma Kaseja kwa sababu amevunja
mkataba na klabu yetu na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake
mapya huko aendako,” alisema Muro
Kuhusu
madai kuwa Kaseja anaidai Yanga, Muro alifafanua: “Kaseja alisaini
mkataba na klabu Novemba 8, 2013, siku hiyohiyo akalipwa shilingi
milioni 20, makubaliano ilikuwa alipwe shilingi milioni 40 ndani ya
kipindi cha mkataba wake wa miaka miwili na hakukuwa na muda maalum
uliopangwa.
“Januari
15, 2014 klabu ikamlipa fedha zake zilizosalia shilingi milioni 20,
lakini Novemba 11, 2014, akaleta barua ya malalamiko kadhaa kwetu akidai
hapati nafasi ya kucheza jambo ambalo siyo kweli na alilalamika kuhusu
masuala ya bima.
“Desemba
15, 2014, Klabu ya Yanga ilimjibu barua hiyo na kumfafanulia kile
alichohitaji, lakini yote kwa yote hakuna ambacho anatudai wala
tunachomdai.”Baada ya hapo gazeti hili lilipata taarifa za ndani juu ya
mpango huo wa Yanga kumshitaki Kaseja kwa kukiuka masharti ya mkataba,
lakini alipoulizwa Muro alisema hajui chochote kuhusua suala hilo.
0 comments: