WEMA, AUNT KICHEKO KABURINI KWA NGWEA INGIA HAPA KWA HABARI KAMILI

Mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na shostito wake, Aunt Ezekiel wakiangusha kicheko katika kaburi la marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’.

INAWEZEKANA ilikuwa utani? Au ‘waliamka’ nazo?! Kweli binadamu anaweza kuvunjika mbavu (kicheko) juu ya kaburi la mpendwa wake? Mh!
Lakini imetokea! Wakati dunia ikisherehekea ujio wa mwaka mpya wa 2015, mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na shostito wake, Aunt Ezekiel walionesha jambo tofauti kufuatia kutinga kwenye kaburi la aliyekuwa nyota wa Bongo Fleva, marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’ na kutumia muda mwingi kucheka na kutuma meseji kwa simu wakiwa juu ya kaburi hilo.
ENEO LA TUKIO
Tukio hilo lililonaswa zimazima na kamera za paparazi, lilijiri Januari Mosi, mwaka huu kwenye kaburi la Ngwea lililopo katika Makaburi ya Kihonda mjini Morogoro.
ILIVYOKUWA
Aunt ndiye aliyeanza kutia timu kwenye makaburi hayo na kukaa. Baadhi ya ‘kruu’ ya Wema, akiwemo Petit Man nayo ilifika na kuungana na Aunt.Baada ya dakika tatu, Mama la Mama, Wema aliwasili akiwa ndani ya nguo isiyokuwa ya mtoko, akakaa upande wa pili wa kaburi. Yeye na Aunt walikaa kwa kupeana ubavu.
CHA AJABU SASA
Awali ilidaiwa kuwa, kruu hiyo ilipanga kuwa baada ya kufika kwenye kaburi hilo wangefanya dua fupi kwa ajili ya kumwombea marehemu apumzike kwa amani huko aliko.Lakini cha ajabu, kabla ya ibada hiyo, Wema, Aunt na wafuasi wao walikuwa wakipiga stori za hapa na pale na katika hali ya kushangaza zaidi, ilifika mahali wakaanza kucheka kile kicheko cha kuvunjika mbavu bila shuhuda wa tukio hili kujua nini hasa kilichokuwa kikiwachekesha!
Baadhi ya wapita njia waliokuwa wakikatiza karibu na makaburi hayo, nao walipigwa na butwaa kuwaona watu hao, walioamini ni ndugu wa marehemu, wakiangua vicheko kama hawana akili nzuri. kwa nukta kadhaa walisimama na kushangaa kabla ya kuendelea na ‘hamsini zao’.-
WEMA ATUMIA SIMU KUFICHA USO
Ni dhahiri kuwa, Wema alijishtukia kuwa kitendo cha kucheka juu ya kaburi hakikuwa na ujazo wa kiungwana hivyo haraka sana aliweka simu sehemu ya midomoni na kumfanya asionekane kwenye kamera kwamba alikuwa akicheka. Miwani ya jua aliyovaa pia ilimsaidia.
Wakati Wema akionesha ubinadamu huo, ‘mwenzangu na mimi’, Aunt yeye alijimalizia kiu yake ya kicheko mpaka pale alipoamua mwenyewe kuacha na si kwa kuogopa kamera wala malaika waliolizunguka kaburi lile (kama wapo) la mmoja wa marapa bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania.
WEMA AJIELEZA
Baada ya wote kuacha kucheka na kila mmoja kuchukua nafasi ya ubinadamu, paparazi wetu alimuuliza Wema ni kwa nini walionesha kuwa na furaha juu ya kaburi la staa huyo.Wema: “Tumepita hapa ili kumuombea ndugu na rafiki yetu Mangweha hivyo hatuna lengo lingine zaidi ya hilo.“Ishu ya kupiga stori na kucheka, tusingeweza kuacha kuongea eti kisa tupo kaburini, maana kila kitu lazima kijadiliwe hata kukaa hapa tumekaa kwa sababu tunafarijika kuona kaburi la mwenzetu.”
Albert Mangweha ‘Ngwea’ enzi za uhai wake.
KWA NINI WALIFANYA ZIARA KABURINI KWA NGWEA?
Awali, mastaa hao na wapambe wao walikuwa na shoo ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika Desemba 31, 2014 ndani ya Ukumbi wa  Matei Lounge mjini Dodoma.Wakiwa wanarudi Dar, walipiga kituo mjini Morogoro ambapo miongoni mwa mambo waliyokuwa nayo kwenye ratiba ni kulitembelea kaburi la Ngwea na kuangusha dua fupi.
Hata hivyo, baada ya yote hayo, kundi hilo la Wema na watu wake hatimaye walifanya dua fupi ya kumuombea malazi mema Albert Mangweha.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Mangweha alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Akiwa na miaka 31 alifariki dunia, Mei 28, 2013 nchini Afrika Kusini. Chanzo cha kifo chake inadaiwa ni matumizi yaliyopitiliza  ya madawa ya kulevya. Alizikwa Morogoro, Tanzania, Juni 6, 2013.

0 comments:

MSANII WA KIZAZI KIPYA MATONYA BAADA YA KULEWA KAVULIWA NGUO


Picha hizi zimezagaa kwenye Mitandao tofauti tofauti ya kijamii ambazo zimeleta utata na kudai kuwa msani Maarafu wa kizazi kipya Matonya baada ya kulewa vijana wa kihuni walimvua nguo na kumfanya kitendo kibaya.... Mtandao huu unajaribu kumtafuta msanii huyu ili kutoa ufafanuzi wa picha hizi ila kwa bahati mbaya hatukufanikiwa kumpata

vijana wa kihuni wakifanya kazi yao

0 comments:

10 wajeruhiwa ajali ya Noah wakitoka Maulid

Mmoja wa majeruhi, Mwanahawa Ramadhani, akiwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza kupatiwa matibabu baada ya kuvunjika mkono kutokana na ajali ya gari wakitokea Bagamoyo mkoani Pwani kusherehekea Maulid. 
Watu 10 wamejeruhiwa baada ya gari dogo aina ya Noah kupinduka katika kijiji cha Kitumbi Wilaya ya  Handeni mkoani Tanga.

Ajali hiyoilitokea juzi gari hilo likiwa limebeba abiria wanawake watupu waliokuwa wakitoka Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kusherehekea sikukuu ya Maulid kuelekea kijiji cha Kwakibuyu kata ya Songa wilayani Muheza.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,  Frasser Kashai, abiria waliopata ajali hiyo walikuwa wakitoka katika Msikiti wa Songa kwa Kibuyu wilayani Muheza.

"Walikodi magari mawili yote aina ya Noah moja liliwabeba wanaume na lingine wanawake kwa ajili ya kuwapeleka Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kusherehekea Maulid," alifafanua Kamanda Kashai.

Alifafanua kuwa baada ya Maulid kumalizika, waligeuza siku iliyofuata kurejea Muheza.

Alisema kuwa gari iliyokuwa imewabeba wanawake, ilitangulia mbele na kufuatiwa ya wanaume.

Hata hivyo, Kamanda Kashai alisema walipofika maeneo ya kijiji cha Kitumbi, gari lililokuwa limewabeba wanawake, lilipinduka na kusababisha majeruhi hao.

Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni baada ya dereva kutaka kulipita gari lingine ambapo lilitokea gari lingine mbele yake na alipojaribu kulikwepa, likapinduka

Baadhi ya majeruhi walivunjika mikono katika ajali hiyo.

Sheikh Mkuu wa kata ya Songa, Twaha Saidi, alimueleza Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu, aliyekwenda kuwajulia hali majeruhi hao katika Hospitali Teule Muheza kuwa majeruhi wote walioumia ni waumini wa dini ya Kiisilamu na walikuwa wanatoka katika Maulid wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Na katika hatua nyingine, majeruhi sita wa ajali ya ajali ya basi dogo aina ya Hiace wakati wakitokea kijiji cha Misozwe kuelekea mjini Muheza mjini, wamelazwa Hospitali Teule Muheza, wametoa kilio kwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu,  wakidai  kwamba tangu wapate ajali hiyo zaidi ya wiki moja sasa, hawajapatiwa huduma yoyote ya matibabu.

Kutokana na kilio cha majeruhi hao, Mgalu amewaagiza viongozi wa hospitali hiyo kuwashughulikia haraka majeruhi hao ikiwamo na kuwapiga picha za X-ray.

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya, ameahidi kwamba atafika hospitali hapo kila siku kusikiliza kero za majeruhi hao.

0 comments:

BREAKING NEWS: Askari wa jeshi la polisi ajiua kwa kujipiga risasi ya Mdomoni Mkoani Mbeya


Askari wa jeshi lapolisi, Sajenti Patrick Kondwa amejiua kwa kujipiga risasi akiwa katika ofisi yake kwenye ghala lakuhifadhia silaha katika kituo cha polisi cha wilaya ya mbozi mkoani mbeya.
Akizungumza na Paparazi wetu kwanjia ya simu, kamanda wa polisi mkoawambeya amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika na kwamba jeshi lapolisi linaendelea na uchunguzi wa tukiohilo.
 
Sajenti Patrick mwenye umri wamiaka 54 ,akiwa katika ofisi yake kwenye chumba cha kuhifadhia silaha katika kituo cha polisi cha wilaya ya mbozi amejipiga risasi mdomoni ambayo imetokea kisogoni na kuondoka na uhai wake, tukio ambalo limetokea majira ya saa tisa usiku na kuthibitishwa na kaimu mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya ileje, Rosemary Staki Senyamule.
 
Baadhi ya waombolezaji ambao wamezungumza na Mwandishi wetu wamesema kuwa wamepokea msiba huo kwa masikitikomakubwa hasa kwa kuzingatia kuwa Sajenti Patrick alikuwani askari mwadilifu na anayeipenda kazi yake.

0 comments:

Ata baada ya kupewa ushauri,Wasanii wa Rnb bado wanapiga picha vifua wazi,huyu mwingine. WAKUBWA TU

Msanii wa Rnb uliyemsikia kwenye hit zake kama 2 On na Pretend “Tinashe” ameng’arisha jarida la V kwa picha zake akiwa kifua wazi kwenye toleo la mwaka 2015.
Tinashe amezungumzia kufananishwa na Jhene Aiko na kusema ‘ kama kila msanii anatengeneza kazi bora basi wote tuna nafasi yetu kwenye muziki ila tusichanganye mashabiki ‘.
Tinashe-x-V-Magazine 
 Tinashe-x-V-Magazine-2 Tinashe-x-V-Magazine-Music-Issue-700x954

0 comments:

Unaambiwa huko DMV imedondoka Theluji (Snow) balaaa

B6rCt6nIYAICE3Q


Kama vile matangazo ya hali ya hewa yalivyo tolewa mwazoni mwa wiki hii na National Weather Service, katika maeneo mbali mbali ya hapa DMV kwamba hali ya hewa itazidi kuwa baridi na kutegemea kuanguka theluji ya inches mbili hadi tatu katika maeneo mbali mbali hapa DMV

0 comments:

Hii sasa Kali Angalia Picha,Unataka midomo tofauti,Daktari anakosea,Imemtokea Mwigizaji wa kike wa filamu za X.

0106-farrah-abraham-lips-twitter-9
Farrah Abraham mwigizaji wa filamu za wakubwa amekutwa na mkasa uliobadilisha maisha yake baada ya kufanyiwa zoezi la kuongeza midomo yake na daktari kukosea na midomo kuwa tofauti na alivyotaka.
Farrah anasema ” alifanya uchunguzi wa zoezi hili na kumtafuta daktari bora wa kazi hii, ganzi niliyochomwa kabla ya zoezi ndio imesababisha nipate tatizo hili, haikuendana na mimi ” .
lips 3

0 comments: