MBUNGE CCM AMVAA PINDA SOMA HAPA KWA HABARI KAMILI
Mbunge wa Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Kagasheki amemtuhumu Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa ndiye aliyekuza mgogoro wa Bukoba uliosababisha madiwani wa halmashauri kushindwa kufanya vikao, akidai kuwa mtendaji huyo mkuu wa Serikali ameshindwa kuchukua hatua. Pinda hakuweza kupatikana, lakini msemaji wake alisema Waziri Mkuu ameshalishughulikia suala hilo kwa kiasi kikubwa.
Tuhuma hizo za Kagasheki ni za nadra kwa mbunge huyo wa chama hicho tawala kuelekeza kwa mtendaji mkuu wa Serikali na mmoja wa wajumbe wa vikao vya juu vya CCM.
Kagasheki, ambaye alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, alitoa tuhumu hizo wakati wa mahojiano maalumu na gazeti hili wiki iliyopita, akisisitiza kuwa ni makosa kuutazama mgogoro huo kuwa ni kati ya yake na meya na akataka ijulikane kuwa kinachoendelea Bukoba ni suala la wizi.
Mgogoro huo wa kisiasa, ambao umedumu kwa takriban miaka miwili na unaotishia kugawanyika kwa CCM, umekolezwa na kufunguliwa kwa kesi tatu ambazo zimezuia utekelezaji wa shughuli za maendeleo na umekuwa ukihusishwa na vita vya ubunge baina ya Kagasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani.
“Hii ni mara yangu ya kwanza kupata nafasi ya kuzungumzia suala hili. Hakuna unafiki hapa, hili nitalisimamia mahali popote na nitalisema mahali popote kuwa Pinda, ndiye tatizo katika mgogoro huu ulioinyima Bukoba maendeleo,” alisema Kagasheki.
“Lakini hiyo hainizuii kusema kuwa Tamisemi ndiyo tatizo, ingawa waziri wake ni Hawa Ghasia. Pinda ndiye msimamizi na bungeni alisema Amani siyo meya tena, lakini hakuna lililofanyika hadi leo na wananchi wanakosa maendeleo,” aliongeza akirejea kauli ya Pinda bungeni kuwa meya huyo alijiuzulu halafu siku chache baadaye Amani akaibuka na kukanusha habari za kuachia kiti cha umeya.
Alisema kuwa awali wakati mgogoro huo unafukuta, uongozi wa juu CCM uliagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG) kwenda Bukoba, naye akaenda kufanya utafiti, akamaliza na akatoa kila kitu.
Kagasheki alieleza: “ Nilikwenda katika kikao cha CCM, Pinda yupo ndani ya chama, kikaagiza madai hayo yafanyiwe kazi, lakini mpaka leo Takukuru hawajafanya chochote. Ndiyo maana nasema, Pinda akija kuomba kura (za urais) Bukoba, pale mjini, hali ni ngumu kwelikweli, atapata shida sana.
“Huu siyo mgogoro, ni wizi wa fedha na ripoti ya CAG ipo wazi lakini wahusika walio chini ya Waziri Mkuu hawataki kuifanyia kazi…Jambo hili lisipofanyiwa kazi, lazima itakuwa ajenda katika Uchaguzi Mkuu.”
Mbunge huyo wa Bukoba Mjini alisisitiza akisema: “Unajua kuna vitu vinaumiza, maana vile siyo vitu vyangu ni taarifa ya CAG na kwa kweli huyu CAG aliyeondoka ungekuwa unamuuliza ukweli, angekwambia amegundua mambo mengi ndani ya Serikali ambavyo hayafanyiwi kazi. Wizi usio na kifani, upotevu wa fedha na jambo zuri ni kuwa ile kazi aliyokuwa akafanya CAG ipo kikatiba.”
Alisema kuwa CCM ilitoa maelekezo na kupitia Serikali ikayapeleka Tamisemi, lakini hadi sasa hakuna pendekezo hata moja la CCM wala CAG lililofanyiwa kazi, lakini Waziri Mkuu yupo kimya.
“Tunapozungumzia Tamisemi, tunazungumzia Waziri Mkuu, bahati nzuri yeye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM. Uamuzi wa Kamati Kuu, Pinda hakufanya hata moja na hapo ndipo mgogoro ukapamba moto,” alidai.
MWANANCHI
MATUKIO BUNGENI- MJINI DODOMA
Spika
wa Bunge la Jamhuri, Anne Makinda akieleza jambo Januari 31, 2015
Bungeni mjini Dodoma ambapo mkutano wa 18 wa Bunge hilo unaendelea.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji George Masaju akitoa ushauri kwa Bunge la Jamhuri.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Dkt. Festus Limbu, akijibu hoja za wabunge waliochangia kwenye taarifa yake.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akijibu hoja za kamati zilizoelekezwa katika wizara yake.
Mbungge wa Kawe, Halima Mdee akitoa mchango wakati wa kujadili taarifa za kamati za Bunge, bungeni mjini Dodoma.
Habari Picha na Hussein Makame-MAELEZO, Dodoma
………………………………………………………………………………………..
KAMATI za Bunge za Serikali za Mitaa (LAAC) na ile ya Hesabu za Serikali (PAC), zimeridhishwa na mafanikio na hatua zilizochukuliwa na Serikali kwa kuongeza mapato yake na kushughulikia changamoto zinazoikabili katika kutekelza majukumu yake.
Kufuatia hali hiyo, Bunge limepitisha taarifa za kamati hizo na nyingine tatu, huku Serikali ikiahidi kufanyia kazi yale yote yaliyopendekezwa kwenye taarifa hizo ili kulipeleka Taifa kule kunakotakiwa.
Taarifa za Kamati ambazo Bunge limezipitishwa jana na juzi usiku ni za Kamati ya Bajeti, Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Hesabu za Serikali (PAC), Miundombinu na Nishati na Madini.
Akihitimisha hoja yake, Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC Rajabu Mbarouk aliipongeza Serikali na Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia kwa hatua alichokua kwa watendaji wa Serikali waliobainika kutumia vibaya fedha za umma.
“Mimi ni mpinzani lakini kwa hili, kwa kweli nimpongeza Waziri kwa sababu jana aliniletea list (orodha) karibu ya halmashauri zote nchini ambazo wakurugenzi amewachukulia hatua, kilichobaki ni mimi kuichukua ile taarifa na kumpelekea kwa CAG kwa ajili ya kuihathibitisha” alisema Mbarouk.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Zitto Kabwe aliipongeza Malmalaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kuongeza mapato na kwamba wameiomba iongeze mapatao katika miaka ijayo ili kuifanya mamlaka hiyo iwe na tija kwa taifa.
“Ni lazima tuwe wakweli, Mamlaka ya Bandari imeongeza sana sana ufanisi katika kazi zake, mapato yameongezeka kutoka shilingi Bilioni 320 mpaka shilingi Bilioni 537 katika kipindi cha miaka miwili” alisema Zitto.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba aliithibitishia kamati na wabunge waliotoa michango yao kuwa wamepokea michango yao na wataifanyia kazi.
“Kwanza nisema ndugu Mwenyekiti, tumewasikia wabunge, tumepokea waliyoyasema na tutayafanyia kazi, tupo kwa ajili hiyo” alisema Naibu Waziri Nchemba.
Alisema tangu mwaka wa fedha ulipoanza, mkakati wa Wizara chini ya usimamizi wa Waziri wa Fedha ilikuwa ni kuhakikisha kila fedha inapokusanywa inakwenda pale ilipokusudiwa.
Alifafanua kuwa hata hoja za baadhi ya wabunge kuwa kuna miradi imepata mgawo sifuri, inawezekana hiyo sifuri ni ya fedha zile zinazotoka nje.
“Naongea hili kwa uhakika, mwaka wa fedha uliooanza tu tulitoa Bilioni 500 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na mpaka wizara zingine wakashangaa wakauliza hizi fedha mmekosea au ndivyo kweli zinatakiwa zije” alisema na kuongeza:
“Walidhani ni za mishahara, haikuzoeleka kutokea fedha nyingi ndani ya mwezi wa kwanza wa bajeti kwa ajili ya shughuli za maendeleo”
Hivyo aliwaomba wabunge wazingatie mambo mamwili, moja Waziri ameweka utaratibu kwamba kila taasisi inapopokea fedha za maendeleo ni lazima ipeleke mrejesho imetumia fedha zile kwa shughul gani na mradi ule uonekane kabla fedha zingine hazijakwenda.
Alisema jambo la pili ni nia ya Serikali kuhakikisha kwamba fedha zilizotengwa kwa ajili ya mifuko na matumizi maalum ya miradi ya maendeleo na kwamba kuanzia mwezi Februari wanarekebisha utaratibu wa kutengeneza mchanganuo wa fedha kuhakikisha fedha hizo zimekwenda kwenye miradi ya maendeleo.
Mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri unatarajiwa umeahirishwa hadi Jumatatu ambapo bunge hilo linataraji kupokea taarifa za Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji.

DIAMOND PLUTNAMZ ATUA NA MPENZI WAKE ZARI MJINI SONGEA
Mwanamuziki Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songea tayari kwa kufanya onesho kubwa kwenye sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM zinazofanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea leo ambapo viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Dr. Jakaya Kikwete.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SONGEA.Diamonda Plutnamz akiongozana na mpenzi wake Zari wakiondoka kwenye uwanja wa ndege wa Songea kuelekea hotelini.Mkuu wa wilaya ya Songea Bw.Joseph Mkirikiti akisalimiana na Zari Mpenzi wa Diamond Plutnamz.
LIPUMBA AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI LEO NA KUZUNGUMZA KWA UCHUNGU KWA KUPIGWA NA POLISI KWENYE MAANDAMANO...AMTAKA KIKWETE AFUTE KESI
MWENYEKITI WA PROFESA CUF IBRAHIM LIPUMBA AKIWASILI KATIKA MKUTANO HUO
Kwa
mara ya Kwanza tangu kutokea kwa vurugu za kisiasa ambazo zilisababisha
mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF profesa IBRAHIM LIPUMBA kupigwa na
kukamatwa na jeshi la polisi na hatimaye kupelekwa mahakamani
mwenyekiti huyo amejitokeza leo jumapili mbele ya wanahabari na kueleza
hali halisi ya tukio hilo huku akieleza adhma yake ya kutaka kumuona
rais kikwete kumueleza matatizo ambayo polisi wa Tanzania wanayo ambayo
yanapaswa kuzibitiwa mara moja.
Akizungumza
kwa uchungu mkubwa LIPUMBA amesema kuwa kilichotokea juzi huko mbagala
ni ishara tosha kuwa Tanzania hakuna amani na democrasia ya kweli kwani
kuzuia maandamanao ambayo kila mwaka huwa yanafanyika kwa amani na
utulivu ni kuwanyima haki watanzania ya kuwakumbuka ndugu zao
waliofariki katika vurugu za Zanzibar.
Amesema
kuwa kitendo walichokifanya polisi kimewasikitisha sana wao kama
wapenda amani na haki kwani polisi hao walikuwa na taarifa tangu tarehe
22 mwezi wa kwanza ila wao wakaja kupiga marufuku maandamano hayo terehe
26 jioni jambo ambalo ni kinyume na utaratibu kwani hawakuwa na muda wa
kuwaambia wanachama wao kuwa maandamano hayo yamepigwa marufuku.
“sasa
nafanya utaratibu wa kistaarabu kabisa wa kwenda kuonana na rais
kikwete na lengo langu ni moja tu la kutaka kumueleza uhalisia wa jeshi
la polisi na vitendo vibaya wanavyovifanya kwani tukiendelea kufumbia
macho matukio kama haya mwisho wa siku tutajikuta mahali pabaya sana
sisi kama nchi hivyo nataka kumueleza kuwa tusiruhusu hali hiyo
itokee.”amesema lipumba.
Aidha
akizungumzia kauli ya serikali iliyotolewa bungeni na waziri wa mambo
ya ndani mh MATHIAS CHIKAWE kuwa CUF walikaidi maagizo ya polisi ya
kusitisha maandamano na ilikuwa ni njia ya kujitafutia umaarufu wa
kisiasa amesema kuwa ni kauli za kutunga na uzushi mkubwa na kauli hizo
zimeonyesha ni jinsi gani serikali imedhamiria kuwapiga wananchi kisawa
sawa katika matukio kama hayo.
Mnamo
tarehe 27 mwezi wa kwanza CUF walikuwa wafanye maandanano ya amani
kuwakumbuka wanachama wenzao waliouawa huko zanzibari lakini maandamano
hayo yaliishia mikononi mwa jeshi la polisi huko mbagala.
Aidha
amewashukuru sana watanzania hususani vyombo vya habari kwa kuonyesha
ushirikiano mkubwa katika sakata hilo na kuuweka ukweli wa jambo hilo
wazi ambapo kila mtanzania ameweza kufahamu ni nini kimetokea.
DIAMOND PLATNUMZ ATUA NA ZARI MJINI SONGEA, APIGA SHOO KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 38 YA CCM
Diamond
Platnumz na madansa wake wakifanya vitu vyao kwenye uwanja wa Majimaji
mjini Songea wakati wa sherehe za miaka 38 ya CCM leo.
Diamond akiimba pamoja na mwanamuziki Abdul Misambano wa kundi la TOT katika sherehe za miaka 38 ya CCM mjini Songea leo.
Mwanamuziki
Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari wakiwasili kwenye uwanja wa ndege
wa Songea tayari kwa kufanya onesho kubwa kwenye sherehe za miaka 38 ya
kuzaliwa kwa CCM zinazofanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea
leo ambapo viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho
Dk. Jakaya Kikwete wamehudhuria.
Diamonda akiongozana na mpenzi wake Zari wakiondoka kwenye uwanja wa ndege wa Songea kuelekea hotelini.
Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joseph Mkirikiti akisalimiana na Zari Mpenzi wa Diamond.
Umati wa wananchi waliohudhuria katika maadhimisho hayo.
(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SONGEA)
ARSENAL YAICHAPA 'MKONO' ASTON VILLA
Mesut Ozil akiifungia Arsenal bao la pili dakika ya 56.
Theo Walcott akishangilia baada ya kuifungia Arsenal bao la tatu dakika ya 63.
Santi Cazorla akifunga bao la nne kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 75.
ARSENAL imeibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Aston Villa
leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England uliopigwa Uwanja wa Emirates
jijini London.Mabao ya Arsenal yamewekwa kimiani na Olivier Giroud dakika ya 8, Mesut Ozil dakika ya 56, Theo Walcott dakika ya 63, Santi Cazorla dakika ya 75 na Hector Bellerin aliyefunga la mwisho muda wa nyongeza.
VIKOSI:
Arsenal: Ospina, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Ramsey, Walcott, Cazorla, Ozil, Giroud
Benchi: Szczesny, Gibbs, Gabriel, Rosicky, Flamini, Chambers, Akpom
Aston Villa: Guzan, Hutton, Okore, Clark, Richardson, Delph,Gil, Sanchez, Cleverley, Benteke, Weimann
Benchi: Sinclair, Baker, Bacuna, Agbonlahor, Westwood, Cissokho, Given
Subscribe to:
Posts (Atom)
0 comments: