PAC yaibua ufisadi wa bilioni 9/- katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere JNIA

  Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),Zitto Kabwe.
Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) imeibua ufisadi uliopelekea upotevu wa zaidi ya Shilingi bilioni tisa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam.
Akiwasilisha taarifa ya mwaka ya Kamati hiyo kuhusu hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2013, Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alisema kuwa ufisadi huo umetokea kwenye mradi wa ujenzi wa Jengo la watu mashuhuri kwenye uwanja huo. 
Zitto alisema kuwa ukaguzi uliofanyika unadhihirisha kwamba harama halisi za ujenzi wa jengo la watu mashuhuri kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere zina mkanganyiko.
Alisema katika ukaguzi ulofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG), mkaguzi huyo alishindwa upata nyaraka wala vilelezo vyote vilivyomo kwenye majalada ya ofisi za Mamlaka ya vya Ndege (TAA) na yale ya kiwanja cha JNIA ikiwemo mkataba kwa ajili ya kuonyesha gharama halisi za ujenzi huo. 
Alisema kuwa kilichopatikana ni ‘offer for Grant for VIP Launge’ yenye thamani ya fedha za kitanzania shilingi bilioni 5.3. 
Zitto alisema kuwa ili thamani ya ujenzi wa jengo hilo, CAG aliagiza Wizara ya Uchukuzi iwasiliane na mthathimini Mkuu wa Majengo ya Serikali ili afanye thathmini ya thamani ya jengo hilo.
“Kwa mujibu wa taarifa ya Mthamini Mkuu wa Majengo ya Serikali hadi kufikia mwezi Mei, 2014 gharama za ujenzi wa jingo hilo zilikuwa ni Shilingi bilioni tatu na mchango wa Serikali kwa shughuli zilizohusu ujenzi wa jengo hilo ulikuwa ni Shilingi milioni 869.4 tu. 
Alisema kuwa hata hivyo katika mikutano mbalimbali ya bunge kati ya mwaka 2011 na 2012, Serikali ilitoa tamko kuwa jengo la watu mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam kuwa ni jumla ya shilingi bilioni 12!  
 
Zitto alisema kuwa tamko hilo la Serikali ni tofauti ya shilingi bilioni tisa zaidi ya kiwango cha Mthamini Mkuu wa Serikali, hali ambayo inaonyesha kuna matumizi yasiyo ya kawaida ya fedha hizo.

0 comments:

LEMA " Natamani Kwenye Amri za Mungu Iongezwe ya 11 Isemayo 'USIWE CCM' "...Hii ni kauli ya Lema Bungeni Ingia hapa kwa habari kamili

 

LEO Wabunge wameendelea kuchangia taarifa za Kamati za Hesabu za Serikali PAC na LAAC zinazoonesha ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma. Hapa  chini nimekuwekea  michango  ya  baadhi  ya  Wabun

Lema: Haiwezekani kila siku tukija humu tunazungumzia wizi tu, inatakiwa tuzungumzie mipango ya maendeleo ya wananchi sio kila siku wizi wizi wizi unaosababishwa na CCM.
Lema: Kama ningeweza kupendekeza pia kwenye Amri Kumi za Mungu, ningependekeza iongezwe amri ya 11 inayosema 'USIWE CCM'
  
Lema: Katika mazingira kama haya, nathubutu kusema 'My Country is like a Getho' mambo hayaendeshwi kwa utaratibu kabisa
  
Esther Bulaya: "Yani watu wanagawana posho Bilion 9, na wanafunzi wanasoma kwa shida halafu mnataka tuwapigie makofi haiwezekani"
  
Esther Bulaya: "Hatuwezi kila siku tunakuja hapa majibu yaleyale kila siku wizi wizi wizi, haiwezekani, hawa watu washughulikiwe"
  
Lissu: "Kinachotufikisha hapa ni Rais kushindwa kutimiza wajibu wake wa kikatiba wa kuwawajibisha watendaji wake"
  
Lissu: "Tunachotakiwa kufanya hapa ni kuanza na hawa mawaziri tulionao humu ndani, tukubaliane kuwawajibisha"

0 comments:

WAFUASI 29 WA CUF WAACHIWA KWA DHAMANA





WAFUASI 29 kati ya 30 waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam wameachiwa leo baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Wafuasi hao walikamatwa majuzi huko Mtoni Mtongani, Dar wakati Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba akielekea Mbagala kuwataka wananchi watawanyike baada ya maandamano ya chama hicho kuzuiliwa na jeshi la polisi.
Wafuasi hao 29 wameachiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar baada ya kila mmoja wao kutimiza masharti ya dhamana kwa kutoa kiasi cha shilingi 100,000 pamoja na barua ya mdhamini mmoja ambaye hana hatia.
Mmoja wa watuhumiwa alikuwa bado mikononi mwa polisi kwa kutokamilisha taratibu za dhamana hiyo akiendelea kumsubiri mdhamini wake aliyechelewesha barua ya udhamini.

Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo amesema kesi yao itatajwa tena Februari 12, 2015.

0 comments:

Muendelezo wa Lil Wayne kujitoa Cash Money,kuondoka na Drake,Minaj na Tyga, Viko hapa


wayne-birdman 

Rapa Lil Wayne ameripotiwa na mtandao wa TMZ kuwa amefungua kesi ya madai ya dola milioni 51 pesa alizotakiwa kulipwa na Birdman toka mwaka jana kwa muziki aliotoa chini ya usimamizi wake.
Malipo mawili anayotakiwa kupokea Lil Wayne ni dola milioni 51 ya kazi za mwaka jana na dola milioni 8 za kurekodi album ya The Carter V toka December 2013 ambazo ni pesa za awali kabla ya kufanya album na dola milioni mbili baada ya album kukamilika kwa album.
Report zinasema Universal inayosambaza album za Cash Money italipa deni la milioni 10 na tayari kampuni hio imewaambia Cash Money watatue matatizo yao.
Lil Wayne akilipwa dola milioni 10 hatakuwa tena na sababu za kutaka kusitisha mkataba na Cash Money, na kuhusu album kutoka hio itabaki kuwa maamuzi ya Birdman.

0 comments:

Mh.Mbatia,Jeshi la polisi lifanyiwe marekebisho ya kimfumo ili kuboresha utendaji wake

POLISI 3 

Serikali imeshauriwa jeshi la polisi lifanyiwe marekebisho ya kimfumo ili kuboresha utendaji wake ambao kwa sasa unalalamikiwa kwa sehemu kubwa na wananchi kwa kukiuka haki za binadamu.

Akizungumza jana mjini Dodoma katika kuhitimisha hoja kuhusu kukamatwa kwa kiongozi wa wa chama cha CUF, Prof Ibrahim Lipumba na wanachama wake na kusema kuwa kitendo hicho kilikiuka haki za binadamu ikiwemo wanawake kudhalilishwa kijinsia.

Mh. Mbatia emeongeza kuwa ili chaguzi zijazo ziwe za amani na utulivu ameishauri serikali kubadilisha sera za vyama vya siasa na utawala pamoja na mfumo wa jeshi la polisi kuendeleza amani na utulivu ambavyo kwa sasa vinaonekana kuanza kutoweka.

0 comments:

IYOBO: MIMBA YA ‘BABY’ NI FARAJA KWANGU

Moses Iyobo akiwa na mpenziwe ambaye ni staa wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel.
Na Imelda Mtema/Amani
Dansa mahiri wa staa wa muziki Bongo na nje ya nchi, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aitwaye Moses Iyobo, amefunguka kuwa hakuna kitu kinachompa faraja kubwa kama mimba ya mpenzi wake ambaye ni staa wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel.
Akizungumza na Amani hivi karibuni, Iyobo ambaye nyuma kidogo alipost picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kutoa pongezi kwa mpenzi wake huyo kwa kumbebea ujauzito, alisema kuwa hakuna kitu ambacho anaona fahari kama hicho.
“ Mimi tu nikiwaza mtu ambaye ninampenda kwa dhati ana mimba yangu napata faraja kubwa sana hivyo kila siku namuomba Mungu ajifungue salama na ampitishe katika majaribu mazito,” alisema Iyobo.

0 comments: