Showing posts with label SPORTS. Show all posts

ARSENAL YAICHAPA 'MKONO' ASTON VILLA

0 comments

 
Mesut Ozil akiifungia Arsenal bao la pili dakika ya 56.
 
Theo Walcott  akishangilia baada ya kuifungia Arsenal bao la tatu dakika ya 63.
 
Santi Cazorla akifunga bao la nne kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 75.
ARSENAL imeibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Aston Villa leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England uliopigwa Uwanja wa Emirates jijini London.
Mabao ya Arsenal yamewekwa kimiani na Olivier Giroud dakika ya 8, Mesut Ozil dakika ya 56, Theo Walcott dakika ya 63, Santi Cazorla dakika ya 75 na Hector Bellerin aliyefunga la mwisho muda wa nyongeza.
VIKOSI:
Arsenal: Ospina, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Ramsey, Walcott, Cazorla, Ozil, Giroud
Benchi: Szczesny, Gibbs, Gabriel, Rosicky, Flamini, Chambers, Akpom

Aston Villa: Guzan, Hutton, Okore, Clark, Richardson, Delph,Gil, Sanchez, Cleverley, Benteke, Weimann
Benchi: Sinclair, Baker, Bacuna, Agbonlahor, Westwood, Cissokho, Given


Read More »

Picha na Orodha ya washindi wa tuzo za FIFA Ballon d’Or 2014.

0 comments


cr 2

Tuzo za Ballon d’Or zimefanyika 12 Jan 2014 ambapo wachezaji bora wa mwaka wamepokea tuzo kutoka shirikisho la soka ulimwenguni FIFA Kupitia Fifa Ballon d’Or.
Tuzo ya mchezaji bora duniani imeshindwa na Cristiano Ronaldo, alikuwa akiwani na Lionel Messi na mlinda mlango Manuel Neur.
Cristiano Ronaldo ameshinda kwa asilimia 37.66 ya kura zote akimshinda Lionel Messi  mwenye asilimia 15.76% na Manuel Neuer mwenye asilimia 15.72%.
Tuzo ya goli bora ameshinda James Rodriguez .

Tuzo ya mwanasoka wa kike ameshinda Nedine Kassler.
Tuzo ya mlinda mlango bora ameshinda Manuel Neur .
Tuzo ya kocha bora ameshinda mjerumani Joachim Law  .
Kikosi bora cha FIFA kimetajwa kuwa na hawa wachezaji . Neuer; Lahm, Ramos, David Luiz, Thiago Silva; Di Maria, Iniesta, Kroos; Messi, Ronaldo, Roben
cr 1
ronald

Read More »

Ifahamu klabu pekee inayoweza kumsajili Messi kwa sasa… INGIA HAPA

0 comments
lionel_messi_barcelona

Huku habari kuhusu uhusiano mbaya wa Lionel Messi na klabu yake ukiendelea kutengeneza headlines kwenye vyombo vya habari barani Ulaya tetesi za kuondoka kwake zimezidi kushika kasi huku kila siku ikiibuka story mpya.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtaalamu wa biashara kwenye mchezo wa soka ni klabu mbili pekee ambazo kwa sasa zina uwezo wa kumsajili nyota huyu raia wa Argentina kinyume na ilivyoripotiwa kuwa klabu kadhaa ziko kwenye harakati za kumsajili.
Klabu hizi zimetajwa kuwa Manchester United na Real Madrid kutokana na kuwa na msuli wa kifedha pamoja na sababu nyingine ambazo zinaleta ugumu kwa zile klabu ambazo zinaweza kuwa na fedha lakini zikashindwa kufanya usajili kutokana na kubanwa kwenye sehemu tofauti.
Katika hali ya kawaida klabu kama Manchester City, PSG , Chelsea na Bayern Munich zinaweza kumsajili mchezaji yoyote kwa bei yoyote, lakini hali kwa sasa ni tofauti kwani kanuni za kusimamia matumizi ya fedha kwa vilabu ‘Financial Fair Play’ zinafanya matumizi kwa vilabu yafanywe kwa kuzingatia vitu vingi.
Hapa ndio mahali ambako United na Real zinapata faida endapo zitakuwa na dhamira ya kumsajili Messi.
Ili kumnunua Messi klabu inayomtaka itapaswa kulipa ada ya uhamisho ambayo ni paundi milioni 196 na mshahara wake utalazimika kuwa mkubwa kutokana na hadhi ya mchezaji mwenyewe na kwa mantiki hiyo ni United na Madrid pekee ambazo zinatengeneza aina ya fedha ambayo inaweza kutosha kumnunua Messi pasipo kukiuka sheria za Financial Fair Play.
Klabu ambazo zinatangaza hasara ya zaidi ya paundi milioni 23.5 kwa muda wa miaka mitatu zinaadhibiwa na sheria za FFP na tayari Man City na PSG zimekumbana na rungu hilo jambo ambalo linawaondoa kwenye mbio za kumsajili Messi endapo nyota huyo atawekwa sokoni.
Pamoja na ukweli huu bado haitakuwa rahisi kwa Barcelona kukubali kumuona Messi akiondoka hasa ukizingatia kuwa klabu hiyo ina adhabu ya kutofanya usajili kwa muda wa mwaka mzima hali inayowafanya wasiwe kwenye nafasi ya kumuuza mchezaji yoyote muhimu kwani kufanya hivyo itakuwa sawa na kujidhoofisha huku wakiwa hawana nafasi ya kujiimarisha.

Read More »

Man U yamsajili kipa wa Barcelona

0 comments

Victor Valdes akisaini kuichezea Man U.

MANCHESTER, England  
KLABU ya Manchester United imethibitisha kumsajili kipa wa zamani wa Barcelona, Victor Valdes kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
Valdes mwenye umri wa miaka 32, alikuwa akifanya mazoezi na klabu hiyo tangu Oktoba, mwaka jana baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akisumbuliwa na maumivu ya goti.
Valdes ameeleza kuwa amefurahishwa na usajili huo na yupo tayari kufanya kazi na kipa chaguo la kwanza la timu hiyo, David de Gea ambaye ni raia mwenzake wa Hispania.

Read More »

Yanga yamtema Kaseja rasmi, yamdai 400m

0 comments


Kipa wa Yanga Juma Kaseja.

YANGA imetangaza rasmi kuachana na kipa Juma Kaseja lakini Championi Ijumaa linafahamu ukweli kuwa klabu hiyo imepanga kumfungulia mashitaka ya kumtaka alipe shilingi milioni 400, kutokana na kuvunja mkataba.
Akitangaza kwa waandishi wa habari jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro alisema kuwa Kaseja ndiye aliyevunja mkataba na klabu hiyo kutokana na kutoonekana mazoezini kwa zaidi ya saa 48, hivyo kuvunja kipengele katika mkataba wake.
“Yanga inatangaza rasmi kuwa haitakuwa na kipa Juma Kaseja kwa sababu amevunja mkataba na klabu yetu na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya  huko aendako,” alisema Muro
Kuhusu madai kuwa Kaseja anaidai Yanga, Muro alifafanua: “Kaseja alisaini mkataba na klabu Novemba 8, 2013, siku hiyohiyo akalipwa shilingi milioni 20, makubaliano ilikuwa alipwe shilingi milioni 40 ndani ya kipindi cha mkataba wake wa miaka miwili na hakukuwa na muda maalum uliopangwa.
“Januari 15, 2014 klabu ikamlipa fedha zake zilizosalia shilingi milioni 20, lakini Novemba 11, 2014, akaleta barua ya malalamiko kadhaa kwetu akidai hapati nafasi ya kucheza jambo ambalo siyo kweli na alilalamika kuhusu masuala ya bima.
“Desemba 15, 2014, Klabu ya Yanga ilimjibu barua hiyo na kumfafanulia kile alichohitaji, lakini yote kwa yote hakuna ambacho anatudai wala tunachomdai.”Baada ya hapo gazeti hili lilipata taarifa za ndani juu ya mpango huo wa Yanga kumshitaki Kaseja kwa kukiuka masharti ya mkataba, lakini alipoulizwa Muro alisema hajui chochote kuhusua suala hilo.

Read More »

David Moyes Azungumzia Ushindi dhidi Ya Barcelona Na Jina Alilopewa Baada.

0 comments
moyes
David Moyes ambaye kwa sasa ni kocha wa klabu ya Real Sociedad amesema “Kushinda dhidi ya Barcelona ni jambo ambalo aliwaza kwa muda mrefu bila kujua atalifanikisha vipi na hatakama itawezekana
Kwenye mechi yake ya kwanza dhidi ya Barcelona, Moyes ambaye alikuwa manager wa Manchester United alifanikiwa kushinda kwa bao moja bila.
Moyes alisema “Ushindi huu umemkumbusha wakati alivyokuwa manager wa Everton, wakati anashinda dhidi ya timu kubwa kama Arsenal, Liverpool na Man United ” yMoes alifukuzwa man utd baada ya miezi kumi kwenye nafasi ya Sir Alex Ferguson.
Mtangazaji maarufu wa soka kutoka Span amembatiza David Moyes jina la ‘Braveheart‘.

Read More »

FULL TIME: TOTTENHAM HOTSPUR 0-0 MANCHESTER UNITED

0 comments

 

Robin van Persie wa Manchester United akijaribu kufunga bao lililookolewa na kipa Hugo Lloris wa Spurs.

 
Patashika wakati wa mtanange wa leo.
 
Mchezaji wa Tottenham, Nacer Chadi (kulia) akiruka juu kuwania mpira na Antonio Valencia wa Manchester United.
TIMU za Tottenham Hotspur na Manchester United zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka suluhu katika mechi yao ya Ligi Kuu England iliyomalizika kwenye Uwanja wa White Hart Lane hivi punde.
VIKOSI VYA LEO
Tottenham: Lloris, Chiriches, Fazio, Vertonghen, Davies, Mason, Stambouli; Chadli, Eriksen, Townsend, Kane
Waliokuwa benchi: Vorm, Dier, Walker, Lamela, Dembele, Paulinho, Soldado

Manchester United: De Gea, Jones, McNair, Evans, Valencia, Carrick, Rooney, Mata, Young, Van Persie, Falcao
Waliokuwa benchi: Lindegaard, Rafael, Smalling, Shaw, Fletcher, A.Pereira, Wilson


Read More »

TAMASHA LA WAFALME: DIAMOND, MZEE YUSUF WAWEKA HISTORIA DAR LIVE

0 comments
Diamond Platnumz akisema na mashabiki wake waliofurika Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Diamond akiwachombeza mashabiki.
Nyomi ya kufa mtu ndani ya Dar Live.
Diamond akiwa kwenye jukwaa la kupanda na kushuka.
Mfalme Mzee Yusuf on da stage.
Mfalme akiwapa 5 mashabiki wake waliofurika Dar Live.
Mzee Yusuf akiwadatisha mashabiki kwa ngoma zake kali.
Nyomi ikiwa imedata na shoo kali kutoka kwa Mzee Yusuf.
Mzee Yusuf akicharaza gitaa.
Diamond akicheza sebene ndani ya Dar Live.
Platnumz akizidi kufanya yake stejini.
Diamond akimtambulisha kwa mashabiki mshindi wa zaidi ya milioni 500 za Big Brother Hotshots, Idris Sultan.
Diamond na Idris wakifanya yao stejini.
Idris Sultan akimtambulisha kwa mashabiki wa Dar Live mshikaji wake aliyekuwa naye kwenye mjengo wa BBA, Samantha wa Afrika Kusini.
Diamond akichana mistari ya wimbo wa Muziki Gani na mshikaji aliyepanda stejini kumwakilisha Nay wa Mitego.
Baada ya mshikaji huyo kufanya makamuzi ya hatari, Diamond aliamua kumpatia shilingi 50,000.
Diamond akizidi kuwapa raha mashabiki wake wa Dar Live.
Nyomi ya kutisha ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.
Diamond akifanya makamuzi na dansa wake.
Dansa wa Diamond akionyesha umahiri wake stejini.
...Sebene time.
Diamond akilitawala jukwaa kwa sarakasi.
NIMEMALIZA: Diamond baada ya kuwakonga nyoyo mashabiki wake waliofurika Dar Live na wao kuridhika aliamua kupozi nao kwa picha hii.
Ijumaa Sexiest Bachelor anayemaliza muda wake, Yusuf Mlela akiwasalimia mashabiki.
Diamond akisalimia na msanii wa filamu, Yusuf Mlela baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Ijumaa Sexiest Bachelor. Taji hilo alikuwa nalo Mlela.
Diamond akipokea tuzo ya Ijumaa Sexiest Bachelor kutoka kwa Mkurugenzi wa Kijumosi Traders Ltd, Mohammed Mustapha.
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa waandaaji wa shindano hilo, Amran Kaima akimkabidhi Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz cheti.
Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz akipozi na tuzo yake pamoja na cheti.
Mzee Yusuf akikandamiza kinanda wakati wa shoo yake Dar Live.
Mzee Yusuf na vijana wake wakifanya yao stejini.
Mzee Yusuf akionyesha ujuzi wa kucharaza gitaa chini kwa chini.
Mashabiki baada ya kupagawa na shoo ya Mzee Yusuf.
MFALME wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' usiku wa Krismasi amewadhihirishia mashabiki wake kuwa ni mfalme baada ya kufanya makamuzi ya hatari katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar kwenye Tamasha la Wafalmelililodhaminiwa na VODACOM pamoja na COCACOLA.
Staa huyo aligonga ngoma zake zote na kuzikonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliofurika katika uwanja huo wa burudani.
Mbali na Diamond, Mfalme wa Taarab nchini, Mzee Yusuf naye alifanya shoo kali na kuwapagawisha mashabiki waliofika kwa wingi kuliko siku zote katika ukumbi huo wa kisasa wa Dar Live.

Read More »

Shindano la Miss Tanzania limefungiwa. Taarifa kamili ipo hapa. INGIA HAPA KUPATA HABARI KAMILI

0 comments
Update_810_500_55_s_c1
Tangu atangazwe aliyekuwa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu mengi yameongelewa kuhusiana na tetesi za udanganyifu wa umri na vitu vingine kadhaa vinavyomhusu mrembo huyo ikiwemo suala la umri wake na kiwango cha elimu yake ambapo yeye mwenyewe alikanusha taarifa hizo.

Story ikaendelea Novemba 8, 2014 siku ambayo Kamati ya Miss Tanzania ilikutana na waandishi wa habari Dar es salaam na kutangaza kwamba Sitti Mtemvu ameandika barua kwa hiari yake yeye mwenyewe, kwamba amelivua taji hilo hivyo kamati hiyo ikamtangaza Lilian Kamazima aliyekuwa mshindi wa pili kushikilia taji hilo.

Leo December 25 kuna taarifa kwamba Serikali imelifungia shindano la Miss Tanzania kwa miaka miwili kutokana na sababu mbalimbali na ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea, ikiwemo udanganyifu mkubwa unaojitokeza kila mwaka kwenye shidano hilo.

Maamuzi hayo yamechukuliwa na BASATA, ambapo Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza amesema maamuzi hayo yalifikiwa baada ya kukaa kikao cha tathmini ambapo Kamati ya Miss Tanzania ilishindwa kujibu hoja za msingi za wadau na kukiri kuwepo udhaifu katika uendeshaji wa shindano hilo.

Baada ya kupitia maelezo yote na taarifa ya tathmini ya shindano hilo ni vyema tulisimamishe kwa muda ili mwandaaji ajipange upya, atakaporejea arejee kwa nguvu na kuandaa shindano lenye hadhi kubwa kuliko ilivyo hivi sasa…“– Mngereza.

Shindano hilo limekumbwa na kashfa mbalimbali tangu mwaka 2006 ikiwemo ya kuvisha mataji warembo wasiokidhi vigezo.

Chanzo cha Habari: Gazeti la Mtanzania, December 25.

Read More »

Mliberia Yanga anatafutwa Ulaya HABARI KAMILI IPO HAPA

0 comments
Mshambuliaji hatari wa Simba, Kpah Sherman.
Na Saleh Ally
WAKATI Yanga ikiwa katika maandalizi ya mwisho kuwavaa Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara, jambo jipya limeibuka kuwa yule mshambuliaji wake hatari, Kpah Sherman raia wa Liberia, anatuhumiwa kutoroka kazini nchini Cyprus.

Taarifa kutoka Cyprus barani Ulaya kwa mmoja wa Watanzania wanaoishi nchini humo zimeeleza vyombo vya habari nchini humo, vimeripoti kuwa Mliberia huyo atafunguliwa mashitaka baada ya kutorokea Tanzania.“Nimesikia huyo mchezaji yuko huko nyumbani, ila huku vyombo vya habari vya hapa vimeripoti timu yake ina mpango wa kufungua kesi Fifa kuelezea kuhusiana na kutoroka kwake,” alisema Mtanzania huyo anayeishi nchini humo.
Juhudi za kuwapata viongozi wa Yanga ilikuwa ni ‘sheedaa’, imeelezwa Mwenyekiti Yusuf Manji yuko nje ya nchi na katibu mkuu mpya, hajaingia ofisini rasmi.Uongozi wa Klabu ya Centikaya TSK ya Cyprus, umethibitisha kushitushwa na taarifa za Sherman kuondoka nchini humo akidai ana matatizo ya kifamilia.
Lakini baadaye ukapata taarifa kuwa amejiunga na klabu kongwe ya Tanzania iitwayo Yanga nao wakaanza mipango ya kufungua mashitaka kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Akizungumza na Championi Jumatano kutoka Cyprus, Rais wa Centikaya TSK, Meric Erulku amesema ni kweli kumekuwa na hali kutoelewana.“Kweli hali hiyo imetokea, hatukuambiwa kama anakwenda kwenye majaribio na ruhusa aliyopewa haikuwa ya kwenda kufanya majaribio.
“Kweli tuna mkataba naye, haujaisha na haujavunjwa. Pia hatujalipwa na kulikuwa na mpango wa kwenda Fifa, lakini meneja wake amezungumza nasi.“Hivyo tunaendelea na hayo mazungumzo ili kujua tutafikia wapi. Kwa kuwa hapa katikati kuna sikukuu, naomba unitafute Jumanne ijayo nitakupa jibu sahihi kama tunakwenda Fifa au tumemalizana nao,” alisema Erulku maarufu kama Buzlat.
Sherman amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akichukua nafasi ya Mganda Hamis Kiiza.
Tayari Sherman ameichezea Yanga mechi moja ya kirafiki dhidi ya Simba ambayo Yanga ililala kwa mabao 2-0.Hata hivyo, Mliberia huyo ameonekana kukonga nyoyo za mashabiki kiuwezo baada ya mechi hiyo moja.

Read More »

Picha,Marcio Maximo aondoka rasmi nchini kurejea kwao nchini Brazil. INGIA HAPA

0 comments

Baada ya Taarifa rasmi kutoka klabu ya Yanga December 15, 2014 kuwa kocha Mbrazil Marcio Maximo ameondoka ndani ya timu hiyo  baada ya uongozi wa Yanga kufikia makubaliano naye ya kuvunja mkataba, Marcio Maximo aondoka rasmi nchini kurejea kwao nchini Brazil na ndege ya shirika la ndege la Emirates.
 Maximo

Read More »