Maelezo ya Wabunge Anna Tibaijuka na Chenge kwenye Baraza la Maadili ya Utumishi…
Baraza la maadili ya utumishi wa umma siku ya February 26 limekaa kikao kujadili ishu ya fedha za Escrow ambapo Mbunge Andrew Chenge alifikishwa kwa mara ya pili mbele ya Baraza hilo kwa ajili ya kuhojiwa.
Baraza hilo lilikwama kumhoji Chenge
kutokana na Mbunge huyo kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga kuhojiwa
ambapo mwenyekiti wa Baraza hilo amesema wanasubiri mwongozo wa Mahakama
Kuu kuhusu kumhoji Mbunge huyo.
Ikafika zamu ya Mbunge Anna Tibaijuka, katika kuhojiwa kuhusu ishu ya mgao wa fedha za Escrow aliulizwa kuhusu matumizi ya fedha alizopata.
Katika maelezo yake kuna fedha milioni
kumi ambazo alisema kwamba ilikuwa ni hela ya mboga kitu ambacho
kiliwachekesha watu waliokuwa ndani ya kikao hicho.
0 comments: