MAJANGA MWISHONI MWA MWAKA 2014: NDEGE YA AIRASIA QZ8501 YAPOTEA IKIWA NA WATU 162
Kati ya watu hao 162, abiria walikuwa 155, marubani 2 na wafanyakazi wa ndege hiyo 5. Watu 157 ni raia wa Indonesia, 3 raia wa Korea Kusini, 1 kutoka Malaysia na 1 raia wa Singapore.
Imeelezwa kuwa kabla ya ndege hiyo kupoteza mawasiliano, rubani aliomba kubadili uelekeo wa kawaida kutokana na hali mbaya ya hewa.
Ndege hiyo ilifanyiwa matengenezo kwa mara ya mwisho Novemba 16, 2014 kama ilivyokuwa imepangwa.
Rubani wa ndege hiyo ana uzoefu wa saa 6,100 angani huku msaidizi wake akiwa na uzoefu wa saa 2,275.
Miongoni mwa abiria 155 waliokuwa kwenye ndege hiyo, 138 ni watu wazima, 16 watoto na 1 mama mjamzito.
QZ8501 imetoka Indonesia saa 11: 27 alfajiri na ilitarajiwa kuwasili Singapore saa 2:37 asubuhi.
FULL TIME: TOTTENHAM HOTSPUR 0-0 MANCHESTER UNITED
Robin van Persie wa Manchester United akijaribu kufunga bao lililookolewa na kipa Hugo Lloris wa Spurs.
Patashika wakati wa mtanange wa leo.
Mchezaji wa Tottenham, Nacer Chadi (kulia) akiruka juu kuwania mpira na Antonio Valencia wa Manchester United.
TIMU za Tottenham Hotspur na Manchester United zimeshindwa kutambiana
baada ya kutoka suluhu katika mechi yao ya Ligi Kuu England
iliyomalizika kwenye Uwanja wa White Hart Lane hivi punde.VIKOSI VYA LEO
Tottenham: Lloris, Chiriches, Fazio, Vertonghen, Davies, Mason, Stambouli; Chadli, Eriksen, Townsend, Kane
Waliokuwa benchi: Vorm, Dier, Walker, Lamela, Dembele, Paulinho, Soldado
Manchester United: De Gea, Jones, McNair, Evans, Valencia, Carrick, Rooney, Mata, Young, Van Persie, Falcao
Waliokuwa benchi: Lindegaard, Rafael, Smalling, Shaw, Fletcher, A.Pereira, Wilson
BREAKING NEWS: MWISHONI MWA MWAKA 2014: NDEGE YA AIRASIA QZ8501 YAPOTEA IKIWA NA WATU 162 INGIA HAPA KWA HABARI KAMILI
NDEGE ya AirAsia, QZ8501 iliyokuwa na watu 162 ikitokea Indonesia kwenda Singapore imepoteza mawasiliano leo asubuhi.
Kati ya watu hao 162, abiria walikuwa 155, marubani 2 na wafanyakazi wa ndege hiyo 5. Watu 157 ni raia wa Indonesia, 3 raia wa Korea Kusini, 1 kutoka Malaysia na 1 raia wa Singapore.
Imeelezwa kuwa kabla ya ndege hiyo kupoteza mawasiliano, rubani aliomba kubadili uelekeo wa kawaida kutokana na hali mbaya ya hewa.
Ndege hiyo ilifanyiwa matengenezo kwa mara ya mwisho Novemba 16, 2014 kama ilivyokuwa imepangwa.
Rubani wa ndege hiyo ana uzoefu wa saa 6,100 angani huku msaidizi wake akiwa na uzoefu wa saa 2,275.
Miongoni mwa abiria 155 waliokuwa kwenye ndege hiyo, 138 ni watu wazima, 16 watoto na 1 mama mjamzito.
QZ8501 imetoka Indonesia saa 11: 27 alfajiri na ilitarajiwa kuwasili Singapore saa 2:37 asubuhi.
Tuzo Walizoshinda @VanessaMdee Na @diamondplatnumz Zilizofanyika Nigeria.
Vanessa ameshinda tuzo ya Best Female Artist in East Africa [Msanii bora wa kike Afrika Mashariki ] huku Diamond akishinda Tuzo Ya Best Male Artist in East Africa [ Msanii bora wa kiume Africa Mashariki] . Tuzo ya Diamond ilipokelewa na Peter Msechu ambaye pia alikuwa kwenye kuwania tuzo hizo.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewatimua wanachama wake 42 wakiwemo wagombea walioshindwa kupita kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa hivi karibuni.
Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho, kutimuliwa kwa wanachama wake hao ni hatua ya chama hicho kujisafisha kutokana na kile kinachodaiwa kwamba baadhi ya wagombea hao wanatuhumiwa kufanya hujuma wakati wa mchakato wa uchaguzi serikali za mitaa, vitongoji na vijiji uliofanyika Desemba 14, mwaka huu.
Akitangaza uamuzi huo mjini humo, Katibu wa Chadema Jimbo la Korogwe Mjini, Ezekiel Mbwilo alisema wahusika waliotimuliwa uanachama wanatuhumiwa kwa kukubali vitisho na wengine kurubuniwa kwa fedha za wapinzani wao, hatua iliyowalazimu kwenda kuondoa majina yao katika hatua za mwisho kuelekea kwenye kinyang’anyiro hicho.
“Tuligundua kuwa baadhi ya wahusiska walijihusisha na hujuma mbalimbali dhidi ya chama chetu, ikiwamo kukubali kupewa fedha na wapinzani wao ili wajiondoe. Tangu awali, tulishakubalina kwamba ikibainika watu waliofanya hujuma tutawatimua kundini na hapa ndipo tunahitimisha lile tulilokubaliana,” alisema.
Mbwilo alitaja maeneo wanayotoka wanachama hao waliotimuliwa na idadi yao kwenye mabano ni Kwamsisiwatu (6), Mahenge (10), Kitifu (25) pamoja na mmoja kutoka Manundukati ambaye alidai kwamba mhusika huyo aliamua kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi ukiwa katika hatua za mwisho baada ya kurubuniwa na wapinzani wa chama hicho.
Akizungumzia vitisho alivyodai vilitolewa baadhi ya wanachama wa vyama vingine dhidi ya wagombea wa Chadema, Mbwilo alisema tayari amewasilisha taarifa hizo kwenye vyombo vya usalama na katika jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi.
BABY MADAHA MAPENZI NI HOBI YANGU INGIA HAPA KUNA STORY KAMILI
Mwanadada asiyeishiwa matukio Bongo, Baby Madaha.
MWANADADA
asiyeishiwa matukio Bongo, Baby Madaha ameibuka na kutoa kali ya mwaka
kwamba anapenda mapenzi kuliko kitu kingine chochote duniani.
Akichezesha taya na paparazi wetu, Baby Madaha alisema ‘hobi’ yake ni
mapenzi japokuwa anapenda muziki lakini haifikii jinsi anavyoyapenda
mapenzi kwani yanampumzisha akili yake na kumfurahisha moyo wake pia.
“Ukweli napenda mapenzi kuliko kitu chochote ila sipendi kuzinguliwa
na wanaume, ninapenda muziki, filamu lakini haviwezi kufikia mapenzi
kwani ndiyo kila kitu kwangu na yananipa starehe kuliko kitu chochote
hapa duniani,” alisema Baby Madaha.
Subscribe to:
Posts (Atom)
0 comments: