Simba yamsajili beki wa Mtibwa. Ingia Hapa Kwa Habari Kamili

hassan kessy

Katika usiku ambao umekuwa na movement nyingi za wachezaji na makocha , klabu ya Simba imekamilisha usajili wa beki wa pembeni toka timu ya Mtibwa Sugar Hassan Kessy .
Beki huyo ambaye ametokea kuwa moja kati ya wachezaji wa kutmainiwa kwenye klabu hiyo ya wakata miwa wa huko Manungu Turiani mkoani Morogoro anaungana na wachezaji wapya waliosajiliwa katika kipindi hiki cha dirisha dogo ambao ni Simon Sserunkuma , Danny Sserunkuma , na Juko Murshid wote toka Uganda .
Kessy ambaye ametajwa kuwa moja kati ya wachezaji wanaokaribia kutiwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars aliicheza Mtibwa kwa mara ya mwisho katika mchezo wa kirafiki ambao ilifungwa na Azam Fc 3-1 .
Beki huyu anasajiliwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu yaliyofanyika chini ya usimamizi wa viongozi wa Simba wakiongozwa na Geoffrey Nyange Kaburu na Kiongozi wa Mtibwa Jamal Bayser .
Tetesi zaidi zinasema kuwa Simba imemsajili beki huyo kwa thamani ya shilingi milioni 30 .

0 comments:

Breaking News Rasmi…Marcio Maximo aondoka Yanga. Ingia Hapa Kwa Habari Kamili



maximo+manji+leo.tif
Habari rasmi toka ndani ya klabu ya Yanga zinasema kuwa kocha Mbrazil Marcio Maximo ameondoka ndani ya klabu hiyo .
Habari hizi zinakuja dakika chache baada ya Maujanjayamjini kuripoti tetesi zinazohusu mustakabali wa kocha huyo Mbrazil.
Maximo anaondoka Yanga baada ya uongozi wa klabu hiyo kukubaliana naye kuvunja mkataba wake baada ya kushindwa kuelewana juu ya jinsi ya kuiendesha klabu hiyo kwenye masuala ya ufundi .
Yanga ilishikilia msimamo wa kumuajiri mkurugenzi wa ufundi ambaye alipangwa kuwa Charles Boniface Mkwasa jambo ambalo Maximo hakukubaliana nalo.
Nafasi ya Maximo sas aitachukuliwa na Mholanzi Hans Van Der Pluijm ambaye aliifundisha timu hiyo kwa nusu msimu baada ya kufukuzwa kwa Mholanzi mwenzie Ernst Brandts .
Tukio hili linaendeleza historia ya Yanga kufukuza makocha baada ya kufungwa na Simba kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe baada ya kufukuzwa kwa Ernst Brandts msimu uliopita kufuatia kipigo cha 3-1 mbele ya Simba iliyokuwa inaongozwa na Dravko logarusic.

0 comments:

Breaking News , Yanga yamsajili Amisi Tambwe toka Simba. Soma Hapa Kwa Habari Kamili



tambwe yanga
Taarifa zilizoingia kwenye mtandao huu dakika chache zilizopita ni kwamba Dar-es-salaam Young Africans imemsajili mshambuliaji wa Simba aliyeachwa Amisi Tambwe .
Yanga imemsajili Tambwe dakika chache zilizopita ambapo anakuja kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Hamis Kiiza ambaye amejiunga na URA ya Uganda .
Tambwe amesajiliwa na Yanga baada ya kuachwa na Simba.
Tambwe amesajiliwa na Yanga baada ya kuachwa na Simba.
Tambwe alikuwa mfungaji bora wa ligi msimu uliopita ambapo alifunga mabao 19 kwenye ligi lakini alishindwa kuwika msimu huu baada ya kutopewa nafasi ya kutosha chini ya Patrick Phiri.
Simba imemuacha Tambwe baada ya kumsajili Danny Serunkuma toka Gor Mahia ya nchini Kenya .
Yanga imekamilisha usjaili huu saa chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa kama ilivyopangwa na Tff .

0 comments:

HAUSIGELI ALIYEMTESA MTOTO UGANDA AHUKUMIWA MIAKA 4 JELA


 Jolly Tumuhirwe (22).

HAUSIGELI aliyenaswa kwenye video akimtesa mtoto nchini Uganda, amehukumiwa kwenda jela miaka minne katika mahakama moja nchini humo.


Jolly Tumuhirwe wakati akimtesa mtoto Arnella mwenye miezi 18.

Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe (22) aliiambia mahakama kuwa anajutia kile alichokifanya na anaomba msamaha kwa familia na jamii nzima.
Amehukumiwa kwa kosa la kumtesa mtoto Arnella mwenye miezi 18.

0 comments: