Polisi Mwanza watumia risasi za moto kulinda mkutano wa Machinga
Mkutano
huo wa uchaguzi ambao ulifunguliwa na katibu tawala wa wilaya ya
nyamagana Marcella Mayala, ulitawaliwa na zomeazomea, shangwe na
vigelegele wakati wagombea wa nafasi mbalimbali walipokuwa wakijinadi,
huku baadhi ya machinga wakihoji zilipo fedha zao zaidi ya shilingi
milioni 10 zilizotolewa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Mh.Dk. Jakaya Kikwete kwa ajili ya kuwasaidia machinga kukopeshana ili
kuinua biashara zao.
Baadhi
ya wagombea wa nafasi ya uenyekiti waliokuwa wakishangiliwa wakati
wakijieleza kuomba kura ni pamoja na Said Tembo, Richard Mushi na
Kabaila Liberatus.
Kila
mgombea aliwahakikishia machinga kupata maeneo mazuri ya kufanyia
biashara pamoja na kumaliza kilio cha muda mrefu cha kukamatiwa mali zao
na askari mgambo wa jiji.
Uchaguzi
wa umoja wa machinga jijini mwanza unafanyika kufuatia machinga kukosa
viongozi kwa muda mrefu na hadi paparazi wetu anaondoka katika uwanja
huo wa CCM kirumba, zoezi la upigaji kura lilikuwa limekamilika katika
nafasi zote zinazowaniwa.
Na
habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Said Tembo amechaguliwa
kuwa mwenyekiti wa muda wa umoja wa machinga jijini mwanza.
0 comments: