Siku
ya jana December 12 kulikuwa na Sherehe za Utoaji wa Tuzo za
Wanamichezo Bora Tanzania mwaka 2013/2014, zilizotolewa na Chama cha
Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ambazo zilifanyika
katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, ambapo Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo
alikuwa Rais Wa Zanzibar,
Dr. Ali Mohamed Shein
Tuzo kubwa ya kwanza iliyotolewa usiku wa jana ni Tuzo ya Heshima ambayo ilitolewa kwa Hayati Sheikh Abeid Aman Karume na kupokelewa na Mama Fatma Karume.
Sheridah Boniface alivunja Rekodi kwenye
sherehe hizo baada ya kutoka na jumla ya Tuzo tatu, Tuzo ya Jumla ya
Mwanamichezo Bora 2013/ 2014, tuzo ya Mwanamichezo Bora Chipukizi na
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Soka Wanawake.
Wachezaji wa Azam, Erasto Nyoni na Kipre Cheche baada ya kupokea tuzo zao.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Gofu Wanawake imechukuliwa na Madina Iddy.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Gofu imechukuliwa na Nuru Mollel.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Gofu Wanawake imechukuliwa na Madina Iddy.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Gofu ya Kulipwa imechukuliwa na Hassan Kadio.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Kikapu Wanaume imechukuliwa na Lusajo Samweli.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Kikapu wanawake imechukuliwa na Sajda Ahmed Lyaimaga.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Wavu Wanaume imechukuliwa na Kelvin Peter Severino.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Wavu Wanawake imechukuliwa na Teddy Abwao.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Magongo Wanaume imechukuliwa na Yohana Wilson.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Magongo Wanawake imechukuliwa na Kidawa Seremala.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Soka Wanaume imechukuliwa na Erasto Nyoni.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Tenisi Walemavu imechukuliwa na Novatus Emmanuel Temba kwa upande wa Wanaume.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Tenisi Walemavu imechukuliwa na Rehema Selemani Saidi kwa upande wa Wanawake.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Olimpiki Maalum imechukuliwa na Blandina Blasi kwa upande wa Wanawake.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Olimpiki Maalum imechukuliwa na Raphael Kalukula kwa upande wa Wanaume.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Nje anayechezea Tanzania imechukuliwa na Kipre Cheche.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mtanzania anayechezea nje imechukuliwa na Mbwana Samatta.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mpira wa Mikono Wanaume imechukuliwa na Hemed Saleh.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mpira wa Mikono Wanawake imechukuliwa na Veronica Mapunda.
Tuzo ya Mwendeshaji Bora wa Baiskeli imechukuliwa na Richard Laizer kwa upande wa wanaume.
Tuzo ya Mwendeshaji Bora wa Baiskeli imechukuliwa na Sophia Adson kwa upande wa wanawake.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ngumi za Ridhaa imechukuliwa na Bondia Suleiman Kidunda.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa ngumi za Kulipwa imechukuliwa na Bondia Francis Cheka.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Tenisi Wanaume imechukuliwa na Omary Sulle.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Tenisi Wanawake imechukuliwa na Rehema Athumani.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kike mchezo wa Judo imechukuliwa na Grace Alfonce Mhanga.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kiume mchezo wa Judo imechukuliwa na Geofrey Edward Mtawa.
Tuzo ya Mwanariadha Bora wa Kike imechukuliwa na Zakia Mrisho.
Tuzo ya Mwanariadha Bora wa Kiume imechukuliwa na Alfonce Felix.
Tuzo ya Muogeleaji Bora wa Kike imechukuliwa na Catherine Maswa.
0 comments: