Zari na Diamond kama Beyonce na JayZ, haya matukio yanafanana kila kitu INGIA HAPA KWA HABARI KAMILI

Picha,Zari anavyokodolea macho simu ya Diamond kama Beyonce kwa Jay Z.




Wapenzi Diamond na Zari wamekuwa wakifananishwa na couple tofauti za mastaa duniani kwa picha na pozi tofauti. Kupitia instagram yake Zari amejifananisha na Beyonce kwa jinsi anavyofuatilia shughuli za Diamond kwenye simu yake muda wote wanapokuwa pamoja.


0 comments:

KIRIA na mama mtoto wambwagia MBUNGE MTOTO MLEMAVU KIKAONI...MWANDISHI WA MWANANCHI APOKEA KICHAPO

Kwenye picha kubwa ndiyo Abdalha Sheria Mh Mbunge wa Zanzibar jimbo la Dimani


                           
Mwandishi wa gazeti la Mwananchi amepata kipigo na kutaka kupokonywa kamera kwenye tukio hili la Mbunge kutelekeza familia yake hasa mtoto wake mwenye ulemavu, amepingwa na mbunge wa Blandes Gosbert mbunge wa Karangwe, Kagera.





Kiria akiwa polisi

0 comments:

CHADEMA Yalaani Kufukuzwa Chuoni Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi Philipo Mwakibinga

            Mwakibinga aliyevalia Kombati Nyeusi ya CHADEMA
Wanafunzi wa UDOM Diploma wakiwa Chini ya Ulinzi

Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kimelaani vikali uongozi wa Chuo kikuu cha Dodoma kwa kumfukuza chuoni mtetezi mkuu wa wanafunzi ambaye ndiye waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi Philipo Mwakibinga.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini zinasema viongozi wakuu wa chama hicho wanalaani tabia ya kufukuza ovyo viongozi wa serikali za wanafunzi ili kuwaziba mdomo.
Philipo Mwakibinga ni mwanachama machachari wa Chadema na aliwahi kugombea Uenyekiti wa Bavicha Taifa.
Inaaminika Mwakibinga amefukuzwa kwa sababu ya Itikadi yake kisiasa.Na haya ni maelekezo ya uongozi wa CCM mkoa wa Dodoma kwa viongozi wa chuo hicho wakiamini kufanya hivi ni kuwatisha wanavyuo wasijiunge na Chadema.
Taarifa zaidi zinasema Kiongozi wa upinzani bungeni Freeman Mbowe amemeiagiza wizara ya Elimu kipitia Waziri Kivuli Suzane Lyimo kufuatilia kwa ukaribu suala hili ili kulinda haki za wanachuo hawa.

Updates.......
Maneno ya Philipo Mwakibinga aliyosema huku akiwa amezungukwa na polisi zaidi ya 500 ni haya :
""Nitarudi tena kusoma UDOM as soon as possible.Nitawashangaza Ulimwengu kwakuwa Mlacha na Kilua hawanielewi kama habari za Wagalatia.Lakini naamini makaburi yao na vizazi vyao vitakuja kunielewa hata kama miaka 20 ikipita.
Nawapenda wana UDOM Naipenda UDOM.TETEENI HAKI.KIVULI CHANGU KITAISHI TU.By Mwakibinga P.J.""""
Baada ya maneno hayo aliingizwa ndani ya gari ya polisi huku akisindikizwa na msururu wa magari zaidi ya 10 ya polisi na kuondolewa ndani ya eneo la chuo huku yeye akitabasamu na kuwapunguia mkono wanafunzi wenzake.

0 comments:

WEMA SEPETU: NAJUTIA MIMBA YA KANUMBA INGIA HAPA KWA HABARI KAMILI

Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akiwa na marehemu Kanumba.
MWANADADA asiyeishiwa habari, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ anadaiwa kujutia mimba yake aliyopachikwa na aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ wakati wa mapenzi yao.

Chanzo makini kilicho karibu na Wema kilieleza kwamba, mwanadada huyo kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu huku akijutia mimba aliyopewa na Kanumba ambayo ilichoropoka kwa bahati mbaya na huyo ndiye mwanaume pekee aliyewahi kumpa ujauzito.

   
Mwanadada asiyeishiwa habari, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.

“Yaani Wema anajutia kweli kwamba kwa nini hakuzaa na Kanumba kwani ndiye mwanaume pekee aliyewahi kumpa ujauzito ambapo kwa sasa anatafuta mtoto lakini hapati, yaani yupo kwenye wakati mgumu sana akikuelezea mwenyewe unaweza kulia kwani ana simulizi ya kusikitisha kuhusu maisha yake na Kanumba.
“Hii yote inatokana na kwamba kwa sasa anatamani kuitwa mama lakini hapati hivyo kujikuta akiukumbuka ule ujauzito wa Kanumba anateseka kweli moyoni,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa Wema kuhusu ishu hiyo alikiri na kuonesha namna gani anateseka moyoni.
“Nateseka kweli, tangu ilipotokea kwa Kanumba haijawahi kutokea tena. Hakuna mtu ambaye hapendi kuwa mama, nazidi kumuomba Mungu huenda na mimi itatokea nitapata,” alisema Wema.

0 comments:

MATONYA: NAKUTAFUTA POPOTE ULIPO JAYDEE KWA KUNIDHARIRISHA KWA KUSAMBAZA PICHA NIKIWA SIJITAMBUI

STAA aliyewahi kukamata vilivyo kwenye anga ya muziki wa Bongo Fleva, Shabani Ramadhani ‘Matonya’ ameibuka na kumvaa mwanadada Judith Wambura ‘Jide au Lady Jaydee’ akidai amemdhalilisha kwa mashabiki wake.
Staa aliyewahi kukamata vilivyo kwenye anga ya muziki wa Bongo Fleva, Shabani Ramadhani ‘Matonya’
Akizungumza na paparazi wetu, Matonya alisema anamtafuta Jide popote alipo ili amuulize kinaga ubaga kwa nini aliamua kuposti picha kwenye mitandao yake ya kijamii ikimuonesha akiwa hajitambui pasipo kumtaarifu.
Mwanadada Judith Wambura ‘Jide au Lady Jaydee’.
“Nimeumizwa sana na Jide kwa kitendo chake cha kuamua kunidhalilisha kwa kiasi hicho tena akijua mimi ni mwanamuziki mwenzake na kama kuna kitu aliona simfurahishi kwenye mwenendo wa maisha yangu basi alikuwa wazi kuniita na kunikalisha chini na siyo kama uamuzi alioutumia wa kunianika kwenye mitandao,” alisema Matonya.
Matonya alifafanua kuwa picha hiyo alipigwa katika video yake mpya lakini Jide akaichukua na kuiweka mitandaoni pasipo kumuuliza.
Matonya akiwa mtungi.
“Ile picha aliyoitumia kunidhalilisha ilikuwa ni ya video yangu ya wimbo mpya unaoitwa Homa ya Jiji ambayo itatoka hivi karibuni, sasa yeye ameweka mitandaoni na kusababisha watu wanidharau kwa kuona nimelewa chakari, asiponiomba radhi nitahakikisha namfikisha mahakamani,” alisema Matonya.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Jide aliiposti picha ya Matonya akiwa amelala na kusindikiza na ujumbe ulioonesha kama hamjui msanii huyo hali iliyosababisha mashabiki wengi kumsema vibaya Matonya.

0 comments:

MATONYA: NAKUTAFUTA POPOTE ULIPO JAYDEE KWA KUNIDHARIRISHA KWA KUSAMBAZA PICHA NIKIWA SIJITAMBUI

STAA aliyewahi kukamata vilivyo kwenye anga ya muziki wa Bongo Fleva, Shabani Ramadhani ‘Matonya’ ameibuka na kumvaa mwanadada Judith Wambura ‘Jide au Lady Jaydee’ akidai amemdhalilisha kwa mashabiki wake.
Staa aliyewahi kukamata vilivyo kwenye anga ya muziki wa Bongo Fleva, Shabani Ramadhani ‘Matonya’
Akizungumza na paparazi wetu, Matonya alisema anamtafuta Jide popote alipo ili amuulize kinaga ubaga kwa nini aliamua kuposti picha kwenye mitandao yake ya kijamii ikimuonesha akiwa hajitambui pasipo kumtaarifu.
Mwanadada Judith Wambura ‘Jide au Lady Jaydee’.
“Nimeumizwa sana na Jide kwa kitendo chake cha kuamua kunidhalilisha kwa kiasi hicho tena akijua mimi ni mwanamuziki mwenzake na kama kuna kitu aliona simfurahishi kwenye mwenendo wa maisha yangu basi alikuwa wazi kuniita na kunikalisha chini na siyo kama uamuzi alioutumia wa kunianika kwenye mitandao,” alisema Matonya.
Matonya alifafanua kuwa picha hiyo alipigwa katika video yake mpya lakini Jide akaichukua na kuiweka mitandaoni pasipo kumuuliza.
Matonya akiwa mtungi.
“Ile picha aliyoitumia kunidhalilisha ilikuwa ni ya video yangu ya wimbo mpya unaoitwa Homa ya Jiji ambayo itatoka hivi karibuni, sasa yeye ameweka mitandaoni na kusababisha watu wanidharau kwa kuona nimelewa chakari, asiponiomba radhi nitahakikisha namfikisha mahakamani,” alisema Matonya.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Jide aliiposti picha ya Matonya akiwa amelala na kusindikiza na ujumbe ulioonesha kama hamjui msanii huyo hali iliyosababisha mashabiki wengi kumsema vibaya Matonya.

0 comments:

Saluni ya Ngono Yafumuliwa jijini Dar......Wahudumu wake ni makahaba, mteja hulipa Elfu 60 kwa tendo moja

 
Wakati suala la ajira likiwa bado ni kitendawili kikubwa kwa serikali, Jiji la Dar hivi sasa linatisha, baada ya watu kubuni mtindo mpya wa kujipatia fedha kwa kujihusisha na biashara haramu ya ngono katika maeneo yanayotambulika kufanya shughuli nyingine halali.

Uchunguzi wa paparazi huru unaonyesha kuwa zipo saluni nyingi jijini Dar zinazojishughulisha na biashara ya massage (kuchua) lakini ndani yake wahudumu wanajiuza hadi miili ambapo wateja wakubwa ni waume za watu na vigogo serikalini.

Uchunguzi huo unathibitishwa na tukio moja la hivi karibuni lililonaswa  na polisi katika saluni moja ya kuchua iliyopo  eneo la Kinondoni-Morocco, Dar. Polisi hao walikuwa  katika msako  baada  ya  kudokezwa  maovu  yanafanyika  ndani  ya  saluni  hiyo na paparazi wetu.


Ndani ya saluni hiyo, Polisi walishuhudia mhudumu wa mapokezi ambaye baada ya kuonyeshwa vitambulisho vya askari wa Jeshi la Polisi, alinywea na kuwaruhusu kupekua chumba kimoja baada ya kingine, ili kujionea kama kweli nyumba hiyo ilikuwa ikijihusisha na masuala ya saluni ya uchuaji pekee na siyo vinginevyo.

Katika chumba cha kwanza, askari hao walimkuta mwanaume mmoja akiwa uchi wa nyama, lakini mwanamke aliyekuwa naye akiwa amevaa nguo zake, kitu kilichoashiria kuwa tayari ‘mchezo ulishafanyika’.
 

Katika hali isiyotarajiwa, baada ya kupitia vyumba vingine vinne na kuvikuta tupu, kilichofuata, polisi walishuhudia mwanamke mwenye asili ya Kisomali akiwa uchi na mwanaume wake, dalili zote zikionyesha kuwa walikuwa wakijiandaa kufanya uzinzi.

Baada ya kuwakuta katika hali hiyo, kiongozi wa askari hao, aliwauliza kama hiyo ndiyo biashara ya masaji waliyopata kibali cha kuifanya, lakini wakabakia kujiumauma pasipo kutoa jibu la kueleweka.
 
Binti huyo wa Kisomali, ghafla aliibuka na kuanza kuomba msamaha kwa kitendo hicho, akidai maisha magumu wanayoishi, ndiyo yanayosababisha waifanye biashara hiyo.

Lakini la kushangaza zaidi, ni pale mwanamke huyo alipodai kuwa nyumbani alikotoka, ambako ameolewa, pia alimuacha mwanaye mwenye umri wa miezi minne.
 
Mwanaume aliyekutwa naye, alipoulizwa biashara hiyo inafanyika kwa bei gani, alisema makubaliano yake na mwanamke huyo, ni kutoa kiasi cha shilingi elfu sitini kwa tendo moja!

0 comments:

WEMA NA BOB JUNIOR LIVE, WATUMIA DAKIKA 10 KUONYESHANA MAHABA

Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akizidi kupozi kimahaba na ‘Bob Junior'.

LICHA ya Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kuwahi kufikishwa kortini na Mbongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior, wamebambwa ‘live’ wakioneshana mahaba niue.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akiwa mapajani mwa Mbongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior'.

TUJIUNGE TEGETA, DAR
Ishu hiyo iliyopigwa chabo na paparazi wetu hivi karibuni lilijiri ndani ya Ukumbi wa Club 71 uliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam ambapo Wema siku hiyo alimtambulisha msanii wake mpya anayesimamiwa na kampuni yake ya Endless Fame anayeitwa Ally Luna.

WAKUTANA
Katika tukio hilo, Wema ndiye aliyeanza kufika ukumbini humo akifuatana na timu yake, akiwemo Petit Man (kama kawa).
Muda mfupi baadaye, Bob Junior naye alifika ambapo alipokutana na Wema walianza kupeana mahaba huku wakigandana kwa zaidi ya dakika kumi.

Mbali na Bob Junior, Wema alialika wasanii kibao kwa ajili ya kumsapoti ambao hata wao walipigwa butwaa baada ya kushuhudia tukio hilo.
Wakiwa katika chumba cha VIP, Wema aliendelea kuwa ‘veri klozi’ na Bob Junior hivyo kusababisha minong’ono ya hapa na pale.

MAPOZI
Katika tukio hilo, kilichowashangaza mashuhuda zaidi ni kitendo cha Wema kukaa mapajani kwa Mbongo Fleva huyo bila kujalia macho ya watu.
Wema Sepetu na ‘Bob Junior' wakiteta jambo.

SALAMU KWA DIAMOND NA ZARI?
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walikwenda mbali zaidi na kuanza kuhisi tabia hiyo ya Wema na Bob Junior ni salamu kwa aliyekuwa mwandani wake na kumwagana Nasibu Abdul ‘Diamond’ na ‘bebi’ wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari’.
“Hapa naona kama sielewielewi maana ni mara ya kwanza kumwona Wema na Bob Junior wakigandana kiasi hiki tangu walipopelekana mahakamani kipindi kile na ukizingatia Sharobaro (Bob Junior) alikuwa hasimu wa Diamond aliyekuwa mpenzi wa Wema kipindi hicho,” alisema mmoja wa mastaa wakubwa (jina linahifadhiwa). Akaongeza:
Wema Sepetu akimchumu ‘Bob Junior.

“Nakuhakikishia hizi ni salamu kwa Diamond na yule Zari wake. Hapa Wema anajua kabisa salamu zitawafikia.”
Baadhi ya mastaa hao walionekana kulaani tukio hilo na kujaribu kumtahadharisha Wema juu ya ukaribu huo kwani kama Diamond atagundua atajua ni ishu za kulipizana visasi.
“Kwa vyovyote Diamond akigundua jambo hili litamfanya ukaribu wake na Wema kuzidi kuwa mgumu na kuurejesha ni ndoto kama wana mpango wa kurudiana.”

WENYEWE WANASEMAJE?
Paparazi wetu alipojaribu kuwadodosa wawili hao juu ya uhusiano wao, kila mmoja aliishia kucheka tu bila kutoa majibu ya kueleweka.

DAKTARI AMUONYA WEMA
Wakati huohuo, mmoja wa madaktari wa mastaa Bongo (jina lipo) amemuonya Wema kuhusu masuala ya mapenzi kwamba, kama ni kweli ameanzisha uhusiano mwingine si vizuri kwani bado akili yake haijatulia tangu amwagane na Diamond hivyo anahitaji muda ili kutuliza akili.
“Wema hatakiwi kuanzisha uhusiano wa kimapenzi kwa haraka, wala si vizuri kulipiza kisasi kwani anaweza kujikuta pabaya zaidi, haya mambo ya mapenzi yanatesa sana mastaa wengi na nimekuwa nikiwapa huduma za kisaikolojia,” alisema dokta huyo kwa sharti la kutotajwa mtandaoni.

TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2011, Mahakama ya Mwanzo Kinondoni jijini Dar ilimhukumu Wema kwenda jela miezi sita au faini ya shilingi elfu 40 baada ya kupatikana na hatia ya kumtukana matusi ya nguoni Bob Junior ambapo alilipa faini na kuachiwa huru jambo lililoibua uhasama mkubwa kati yao.

Hivyo, tukio la kuonekana pamoja na kugandana kimahaba ni ishara njema kuwa sasa wapo vizuri na ule uhasama haupo tena!!

0 comments:

Dogo Aslay Ndani ya Penzi Zito na Naima, Naima Ajichora Tatuu ya Jina la Aslay INGIA HAPA



Jamani Mahaba Kitu Kingine , Mwanzo tulijua Nuhu Mziwanda pekeake ndio mwenye ujasiri huu wa kujichora tattoo ya mpenzi wake ..lakini sasa list imeongezeka , Mrembo Naima nae avunja Ukimya , Ajichora Tattoo ya mpenzi wake Dogo Aslay .

Naima ni yule binti aliyekuwaga kwenye beef na Wema Sepetu wakimgombania CK..



0 comments:

Mr Dannis akiwa na Msouth kato baada ya kumtembelea kijana ambaye ni mwanafunzi wa Udom aliyepata majanga ya kuvunjika mguu baada ya kuruka kwenye gari na kutaka kuwakwepa Polisi waliokuwa wanahakikisha usalama unapatikana katika chuo hicho cha Udom kutokana na baadhi ya wanafunzi kuwashawishi wanzao kufanya maandamano yasiyokuwa ya Maani kutokana na kile kinachodaiwa kutopata Mkopo kwa muda unaostahili


Kijana ambaye ni mwanafunzi wa Udom anayefahamika kwa jina la Iddy aliyepata masaibu baada ya kuvunjika mguu katika vurugu za mgomo uliyofanywa na wanafunzi wa Udom wa college ya social science.. Kijana Iddy ambaye amelazwa katika hospitali ya General Dodoma leo hii amepatiwa msaada Mh Shabiby wa fedha za 
matibabu pamoja na while chair baada ya kuzuiliwa kutoka hospitali hapo nkutokana na deni kubwa la matibabu aliyokuwa anadaiwa hospitalini hapo.. Paparazi alifanikiwa kupata nafasi ya kuongea na mzazi wa mwanafunzi huyo na kudai kuwa aliambiwa atapata msaada kutoka chuoni hapo lakini cha kushangza mpaka muda huu wa jioni hatujapa msaada wowote kutoka chuo hicho zaidi ya kupigwa chenga na kutupiana mpira.. Baba wa kijana huyo ametoa shukrani za pekee kwa Mh Shabiby baada ya kuguswa kiubinadamu na kumsaidia kijana wake... Kijana Iddy kwa sasa anaendelea vizuri

0 comments:

Bei za Petroli na Dizeli Kushuka zaidi March Mwaka huu



Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imebainisha kuwa hadi kufikia Machi mwaka huu, bei ya mafuta nchini itaendelea kushuka kulingana na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.

Hata hivyo, mamlaka hiyo imeonya kuwa bei hiyo ya mafuta nchini haitaweza kupungua kwa kiasi kikubwa, kutokana na kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya dola ya Marekani pamoja na kutokubadilika kwa ushuru mbalimbali wa ndani wa mafuta.
 
Pamoja na hayo, Kampuni ya Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PICL) imeiomba Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini kuingilia kati na kuihamasisha Serikali iongeze ulinzi katika mabomba na matangi ya mafuta Kurasini, ambayo kwa sasa hayako salama na ni hatari kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
 
Akiwasilisha taarifa ya ukokotoaji wa mafuta kwa kamati hiyo Dar es Salaam jana, Mtaalamu kutoka EWURA, Lorivii Long’idu, alikiri kuwa ni kweli kwa sasa bei ya mafuta katika soko la dunia imekuwa ikishuka kwa kasi ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.
 
“Bei hizi zimeshuka kutoka dola 100 hadi kufikia dola 60 kwa pipa ambayo ni sawa na asilimia 40 kutokana na kudorora kwa uchumi wa bara la Ulaya katika kipindi hiki na kuwepo kwa tofauti za mitazamo ya kisiasa hasa katika nchi za Marekani na Urusi,” alisema Long’idu.
 
Hata hivyo, alisema pamoja na bei hizo kushuka tangu Julai hadi Desemba mwaka jana, kwa kawaida kwa Tanzania huchukua takribani miezi miwili bei hiyo kuweza kufikia soko la ndani.
 
Alisema bei zote za mafuta katika soko la ndani, zimekuwa zikishuka kuanzia robo ya mwisho wa mwaka jana sambamba na kushuka katika soko la dunia na kwamba bei hizo hukokotolewa na Ewura kwa kutumia kanuni maalum, inayotumia gharama halisi za uagizaji mafuta nchini, zinazotokana na meli za mafuta yaliyopokelewa mwezi husika yaliyonunuliwa mwezi wa nyuma yake.
 
Alisema uhusiano wa bei za soko la dunia na soko la ndani, unapishana kwa miezi miwili na kwamba mafuta yanayotumika mwezi huu, Ewura ilikokotoa bei zake tangu Novemba kulingana na bei ya mafuta yaliyonunuliwa katika soko la dunia mwezi huo.
 
Long’idu alisema kwa hali ilivyo sasa bei za mafuta ghafi katika soko la dunia, zitaendelea kushuka kama hakutakuwa na tukio lisilo la kawaida duniani, hali itakayochangia kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo katika soko la ndani japo si kwa kiwango sawia.
 
Alisema pamoja na bei kushuka katika soko la dunia kwa kiwango chochote kile, bei ya ndani itashuka kulingana na thamani ya Shilingi dhidi ya dola ya Marekani lakini pia ushuru uliopo ambao katika petroli unatozwa Sh 878, dizeli Sh 754 na mafuta ya taa Sh 701 kwa lita ambao wenyewe haubadiliki.
 
Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Nishati na Madini, Jerome Bwanausi, aliagiza Ewura na PICL wanapokokotoa bei za mafuta kuhakikisha wanatoa ufafanuzi wa hali halisi ya bei za soko la dunia na utaratibu mzima wa uingizaji wa mafuta nchini ili kuondoa habari potofu zinazosambazwa juu ya bei hizo za mafuta.
 
Aidha, aliagiza Wizara ya Nishati na Madini kuchukua hatua za haraka na kushughulikia suala la ulinzi katika mabomba na matangi ya mafuta ili kudhibiti hali ya hatari ya kulipuliwa kwa matangi hayo na kuhatarisha usalama wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
 
“Hii ni hatari sana kwa namna yale mabomba yalivyo hayana ulinzi, watu wanatoboa mabomba na kuiba mafuta na kuweka maboya, endapo mtu yeyote akitupa moto pale Dar es Salaam nzima itakuwa haipo, hatua za haraka zichukuliwe, na kamati ipatiwe taarifa za ulinzi wa sasa katika eneo hilo,” alisisitiza.
 
Aidha, alisema kutokana na hali ya hatari ya usafirishaji wa mafuta iliyopo sasa kupitia malori hasa katika vijiji malori hayo yanakopita na kulala, ni vyema Serikali ikaanza mchakato wa kuchimba mabomba ya kusafirishia mafuta na kufufua reli ili kudhibiti usalama wa wananchi

0 comments: