Balaaa!!! La Sikukuu: Changudoa Atopeza Fahamu Baada Ya Kuzidisha Wanaume Ingia Hapa Kuona Picha Zote Za Tukio Zima

Mwanamke(Jenipher ) ayeanayedaiwa kujiuza akiwa hoi hajitambui.
MSICHANA mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Jenipher, anayedaiwa kujiuza katika maeneo ya Shivaz na Kaloleni jijini hapa, amekutwa akiwa amepoteza fahamu kando ya barabara, katika harakati za kujipatia chochote kipindi hiki cha sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.
Akiwa pembeni ya barabara, Jenipher anayeelezwa kuwa maarufu mjini hapa, anadaiwa kuwa siku hiyo alizidisha idadi ya wanaume aliotoka nao, kwa ajili ya kujipatia kipato cha kutosha ili aweze kuburudika vizuri wakati wa sikukuu ya Krismasi.
Baadhi ya mashuhuda wanaomfahamu msichana huyo walisema kwamba katika kipindi cha wiki nzima iliyopita, alikuwa akisaka wanaume kwa bidii na kwamba alikuwa tayari kwa ajili ya kutoa huduma hiyo mahali popote.
“Unajua hapa kila mtu na mambo yake, huyu Jenipher siku zote tupo naye ila wao huwa hawaendi kulipia gesti, ila wanafanya ngono popote hata mtaroni, kwenye ukuta ilimradi huyo mwanaume yupo tayari, ila usiku alizidiwa na wanaume na hakuwa amekula,’’ alisema mmoja wa dada poa aliyekataa kutaja jina lake.
Mmoja wa wamiliki wa baa iliyo maeneo hayo, aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema wasichana wengi wanaojihusisha na biashara hiyo wamekuwa na tamaa kiasi cha kushindwa kujali afya zao, kwani baadhi yao huacha hata kula chakula, badala yake, hunywa pombe aina ya viroba.
Hadi paparazi inaondoka eneo hilo, bado binti huyo alikuwa yupo eneo hilo akiwa hajitambui.

0 comments:

MTOTO WA ANNA TIBAIJUKA AWATUKANA WATANZANIA HUKU AKIMTETEA MAMA YAKE KWA KUCHOTA PESA ZA ESCROW

Kagem Tibaijuka.
WAKATI Rais Jakaya Kikwete akiwa amemuwajibisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka kufuatia kumegewa mgawo wa fedha za Tegeta Escrow, binti anayedaiwa kuwa mwanaye, amejikuta akipata wakati mgumu baada ya kumtetea mama yake kupitia mitandao ya kijamii.

Katika Mtandao wa Twitter, binti huyo aliyejitambulisha kwa jina la Kagem Tibaijuka, alimtetea mama yake akisema fedha zilizowekwa kwenye akaunti yake zilikuwa ni safi na halali na kwamba ziliwekwa kwa nia njema ya kuwasaidia kielimu watoto wa kike
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka.
“My mum did nothing wrong except wanting to help young girls get an education. A school built with my late father. Accepted a donation,” (Mama yangu hakufanya kosa lolote isipokuwa alitaka kuwasaidia wasichana kupata elimu. Shule ilijengwa na marehemu baba yangu. Mchango ukakubaliwa)yalikuwa  ni moja ya maneno yake katika mtandao huo wa Twitter.
Aidha, aliwashambulia wanawake walioonekana kushangilia wakati Rais Kikwete alipotangaza kumuwajibisha mama yake, akiwaambia kuwa anawashangaa kushangilia anguko la mwanamke mwenzao na kwamba hata wao iko siku yatawakuta ya kuwakuta.
Rais Jakaya Kikwete.
Lakini katika mitandao mingine ya kijamii, ikiwemo Facebook na Jamii Forum inayotembelewa na watanzania wengi, walimshambulia binti huyo kwa kumwelezea kama mtu aliyelewa fedha na kwamba mama yake alistahili kuondolewa kwenye nafasi yake, ikiwa ni pamoja na kushtakiwa.
Wachangiaji walioonekana kuchukizwa na utetezi wa binti huyo kwa mama yake, walisema licha ya Profesa Tibaijuka kuondolewa, pia watu wote waliotajwa, wakiwemo Waziri Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu, Eliakim Maswi nao walistahili kuondolewa katika nafasi zao.
Mtandao huu ulimtafuta mama Tibaijuka kupitia simu zake mbili za mkononi, ili kuzungumzia maoni yake baada ya kukutwa na ajali hiyo ya kisiasa pamoja na kumuuliza kama Kagem ni bintiye, lakini moja iliyopatikana, iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Hata hivyo baadaye simu hiyo ilipopigwa, ilionekana imezimwa.
Aidha Kagem mwenyewe, ambaye ofisi zake zinadaiwa kuwa eneo la Kijitonyama jijini Dar es Salaam, naye hakupokea simu yake ya mkononi aliyopigiwa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, hakujibu.
Jumatatu iliyopita, Rais Kikwete alizungumzia suala hilo la fedha zilizodaiwa na Bunge kuwa ni za umma, kuchukuliwa isivyo halali katika akaunti iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania. Wakati Mwanasheria Mkuu, Jaji Frederick Werema alijiuzulu mwenyewe na mama Tibaijuka kuwajibishwa, viongozi wengine waliodaiwa kuhusika na fedha hizo wanaendelea kuchunguzwa na hatua stahiki dhidi yao zitachukuliwa.


0 comments:

TAMASHA LA WAFALME: DIAMOND, MZEE YUSUF WAWEKA HISTORIA DAR LIVE

Diamond Platnumz akisema na mashabiki wake waliofurika Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Diamond akiwachombeza mashabiki.
Nyomi ya kufa mtu ndani ya Dar Live.
Diamond akiwa kwenye jukwaa la kupanda na kushuka.
Mfalme Mzee Yusuf on da stage.
Mfalme akiwapa 5 mashabiki wake waliofurika Dar Live.
Mzee Yusuf akiwadatisha mashabiki kwa ngoma zake kali.
Nyomi ikiwa imedata na shoo kali kutoka kwa Mzee Yusuf.
Mzee Yusuf akicharaza gitaa.
Diamond akicheza sebene ndani ya Dar Live.
Platnumz akizidi kufanya yake stejini.
Diamond akimtambulisha kwa mashabiki mshindi wa zaidi ya milioni 500 za Big Brother Hotshots, Idris Sultan.
Diamond na Idris wakifanya yao stejini.
Idris Sultan akimtambulisha kwa mashabiki wa Dar Live mshikaji wake aliyekuwa naye kwenye mjengo wa BBA, Samantha wa Afrika Kusini.
Diamond akichana mistari ya wimbo wa Muziki Gani na mshikaji aliyepanda stejini kumwakilisha Nay wa Mitego.
Baada ya mshikaji huyo kufanya makamuzi ya hatari, Diamond aliamua kumpatia shilingi 50,000.
Diamond akizidi kuwapa raha mashabiki wake wa Dar Live.
Nyomi ya kutisha ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.
Diamond akifanya makamuzi na dansa wake.
Dansa wa Diamond akionyesha umahiri wake stejini.
...Sebene time.
Diamond akilitawala jukwaa kwa sarakasi.
NIMEMALIZA: Diamond baada ya kuwakonga nyoyo mashabiki wake waliofurika Dar Live na wao kuridhika aliamua kupozi nao kwa picha hii.
Ijumaa Sexiest Bachelor anayemaliza muda wake, Yusuf Mlela akiwasalimia mashabiki.
Diamond akisalimia na msanii wa filamu, Yusuf Mlela baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Ijumaa Sexiest Bachelor. Taji hilo alikuwa nalo Mlela.
Diamond akipokea tuzo ya Ijumaa Sexiest Bachelor kutoka kwa Mkurugenzi wa Kijumosi Traders Ltd, Mohammed Mustapha.
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa waandaaji wa shindano hilo, Amran Kaima akimkabidhi Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz cheti.
Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz akipozi na tuzo yake pamoja na cheti.
Mzee Yusuf akikandamiza kinanda wakati wa shoo yake Dar Live.
Mzee Yusuf na vijana wake wakifanya yao stejini.
Mzee Yusuf akionyesha ujuzi wa kucharaza gitaa chini kwa chini.
Mashabiki baada ya kupagawa na shoo ya Mzee Yusuf.
MFALME wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' usiku wa Krismasi amewadhihirishia mashabiki wake kuwa ni mfalme baada ya kufanya makamuzi ya hatari katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar kwenye Tamasha la Wafalmelililodhaminiwa na VODACOM pamoja na COCACOLA.
Staa huyo aligonga ngoma zake zote na kuzikonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliofurika katika uwanja huo wa burudani.
Mbali na Diamond, Mfalme wa Taarab nchini, Mzee Yusuf naye alifanya shoo kali na kuwapagawisha mashabiki waliofika kwa wingi kuliko siku zote katika ukumbi huo wa kisasa wa Dar Live.

0 comments: