Unaweza kumiliki vigari vidogodogo kama Toyota IST na nyingine lakini zisifanane na hizi.
Ni
miaka kadhaa imepita ndipo nilipoamini gari ni mtu mwenyewe, yani wewe
mmiliki ndio mwenye maamuzi kama utapenda gari lako liwe na swagg au
muonekano wa kuvutia zaidi.
Mara nyingi huwa tunayaacha magari yetu
kama tulivyoyanunua na yanabaki yakawaida tu lakini kuna ambao
hujiongeza alafu magari yao yanatofautiana na ya kwetu wakati aina ni
ileile.
Toyota IST ambazo zinatolewa na Airtel kupitia Yatosha Bundle
ni gari nzuri kiukweli kuanzia kwenye mafuta, nafasi yake ndani ni
kubwa pia na kwenye mishemishe zetu sisi tusio na kipato kikubwa kihivyo
zinatuondolea gharama kubwa.
Muonekano wa gari lako unaweza kubadilika na kuvutia kwa kuongeza vitu vidogovidogo tu kama kubadilisha Matairi na kuweka manene kiasi, rims kali, taa, tinted na vitu vingine kama muonekano wa mbele na wa nyuma.
Magari makali yaliyokua pimped na yenye mvuto yapo Tanzania pia, ni vitu ambavyo vinawezekana hata ukiwa Dar es salaam kuna wachache wameweza kuyatengeneza kwa viwango vyao.
Kama mapenzi yako yako kwenye vigari vidogovidogo kama hivi, kipi kimekuvutia hapa ?
Magari yote hapo juu yanao muonekano tofauti na hili hapa chini ambalo halijafanyiwa mabadiliko yoyote toka kiwandani.
0 comments: