WEMA SEPETU AKIFUNGUKA JUU YA MAHUSIANO YAKE YA KIMAPENZI KWA SASA.
Wema Sepetu amechoka uhusiano wa boyfriend na girlfriend. Muigizaji hiyo wa filamu amesema anataka kuolewa.
Wema alisema hayo jana kwenye reality show yake, In My Shoes baada ya meneja wake Martin Kadinda kumuuliza kwanini hana ‘kiki’ kwa sasa.
Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 alisema kuna vitu vingi anataka kuvifanya ikiwemo kuwa na hamu ya kutulia na kuwa mke wa mtu.
Hata hivyo Wema alisita kumweka wazi mwanaume anayetaka kumweka ndani na kumtaka meneja wake kuwa na subira
0 comments: