MWANAMKE AINGIZWA CHUPA SEHEMU ZA SIRI NA KUSHAMBULIWA KWA NYAYA ZA UMEME

Mkazi wa Kitangiri jijini Mwanza, Biera Edwin (22) amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou Toure akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake kwa tuhuma za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wa mtu.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, lakini Biera mwenyewe alisema kabla ya kufanyiwa kitendo hicho mama ambaye ni jirani yao alimtuma mtoto wake amwite nyumbani kwao, alipokwenda mama huyo alianza kumshambulia.
Alisema alimshambulia akishirikiana na marafiki zake na kumjeruhi vibaya kwa nyaya za umeme, kumwingizia chupa kwenye sehemu zake za siri na baadaye kuchoma nguo zake.
Binti huyu kwa sasa amelazwa katika wadi ya majeruhi kwenye Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure akipatiwa matibabu na alisema baada ya kufanyiwa ukatili huo pia waliteketeza nguo zake kwa moto.
Kama da wa polisi mkoa wa mwanza,Valentino mlowola

Naye dada wa majeruhi, Nice Cosmas anaeleza kuwa akiwa nyumbani kwao, mama huyo wa jirani alituma watoto wake ambao walieleza kuwa wakamchukue mtu wao.
Alisema walipokwenda hapo jirani alimkuta ndugu yake akiwa hana nguo huku akiwa amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake.
Alisema walilazimika kurudi nyumbani kumchukulia nguo za kumvisha na kisha kutoa taarifa kwa mamlaka husika kabla ya kumpeleka hospitali kwa matibabu.
Baadhi ya viongozi wa mtaa wa Kitangiri A walisikitishwa na kitendo hicho na kuomba vyombo vya sheria kuwachukulia hatua kali wahusika.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitangiri A, Issa Salum alisema wanataka haki itendeke kwani kitendo hicho ni nusu ya mauaji.
Naye Mjumbe wa Serikali za Mitaa, Mariam Yusuf alisema mama huyo wa jirani alipaswa kutoa taarifa kwa mabalozi ama kwa wazazi wa binti huyo kama alikuwa na uhakika na madai yake kabla ya kuchukua ukatili dhidi ya binti huyo.


0 comments:

NEW ALART: CCM KUANZA FAGIO LA VIONGOZI WIKI IJAYO


Chama cha Mapinduzi (CCM) wiki ijayo kitaanza rasmi vikao vyake kwa ngazi ya Taifa vitakavyo chunguza maadili ya viongozi ikiwa ni maandalizi ya kuwapata wagombea wanaokubalika na wananchi katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alitoa taarifa hiyo jana katika mkutano maalumu wa kuwashukuru Watanzania kwa kukichagua chama hicho katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 14, mwaka jana. Alisema chama chake kinajipanga kuwa na viongozi wasio wamangimeza na wenye moyo wa kuwatumikia wananchi.
Katibu huyo Mkuu aliwashukuru Watanzania kwa kukipa ushindi chama chake na kubainisha kuwa kitaifa, CCM imeshinda kwa asilimia 81.
Hata hivyo, alisema katika maeneo ambayo imeshindwa kama Wilaya ya Pangani, itafanyika tathmini na watajipanga kuhakikisha Uchaguzi Mkuu ujao wanapa ushindi wa kishindo.Alisema watahakikisha wanashinda katika maeneo yote waliyofanya vibaya.

0 comments:

Alichosema Ney Wa Mitego Kuhusu Nikki Mbishi Kuacha Muziki

ney
Kupitia exclusive interview na Power Jams, Ney wa Mitego amezungumzia hatua ya Nikki Mbishi ya kuacha muziki nakusema “Ukiona kitu hakikulipi ni bora uachane nacho, mtu anaweza kuangalia kitu na kujua hakimfai na bora afanye mambo mengine
Ney aliendelea kusema ” Sijui kwanini amechelewa, nimefurahi kuona maamuzi mazuri kijana mwenzangu aliyofanya, amejitambua na kuamua kuangalia vitu vingine, niko tayari kumshauri kama bado hajapata cha kufanya” .

0 comments:

MAHAKAMA YAIANDIKIA WIZARA KUREJESHA MALI ZA MELI YA MAGUFULI

Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.

Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imeiandikia barua Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya kurejesha mali ikiwamo meli ya Tawariq 1 na  zaidi ya Sh. bilioni mbili za tani 296.3 za samaki kwa raia wawili wa China.
Watu hao ni Hsu Tai na Zhao Hanquing walikamatwa wakivua samaki katika Ukanda wa Kiuchumi wa Bahari ya Tanzania bila kibali.

Kwa mujibu wa barua hiyo iliyosainiwa na msajili wa Mahakama hiyo ya Desemba 17, 2014, imeitaka Serikali kurejea ahadi, kupitia hati ya kiapo iliyotolewa na Godfrey Nanyaro, Dk. Charles Nyamlundana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

Kwa mujibu wa barua ya msajili huyo, kiapo kinasema endapo washtakiwa hawatakutwa na hatia mahakamani Serikali italipa gharama za samaki waliokutwa nao wa tani 296.3 za Sh. 2,074,249,000 ndani ya siku 30 tangu kuachiwa na mahakama.

Chanzo cha NIPASHE kinaeleza kwamba mbali na barua hiyo, Mahakama Kuu, imeambatanisha nakala ya amri ya kuuza samaki hao uliotolewa Desemba 11, mwaka 2009 na Jaji Radhia Sheikh, hukumu ya kuwaachia huru ya Mahakama ya Rufani na Hati ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) ya kuwafutia mashitaka Agosti 14, mwaka 2014.

Septemba Mosi, mwaka huu, upande wa utetezi uliwasilisha barua ya kudai vielelezo hivyo, mbele ya Msajili wa mahakama hiyo.

Katika barua hiyo utetezi wanaomba kwamba mahakama iwarejeshee vielelezo vilivyotolewa katika Mahakama Kuu katika kesi namba 38 ya mwaka 2009 mbele ya Jaji Radhia Sheikh.

Barua hiyo ilivitaja vielelezo hivyo kuwa ni, meli ya uvuvi Tawariq 1 pamoja na Sh. 2, 074,249,000 za tani 296.3 za samaki walizokutwa nazo raia hao ambavyo vilitolewa Oktoba Mosi, 2009 mbele ya Jaji Sheikh.

Awali, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, iliamuru serikali ya Tanzania kulipa meli ya uvuvi pamoja na samaki waliokamatwa miaka mitano iliyopita vyote vikiwa na thamani ya Dola miliobi 3.2  baada ya kuwaachia washtakiwa wawili raia wa China, waliokuwa wanakabiliwa na kesi hiyo.

Wakili wa utetezi Kapteni Ibrahim Bendera, alisema baada ya mahakama kutoa amri hiyo, meli iliyokamatwa na wateja wake ilikuwa na thamani ya Dola milioni 2.5 na samaki waliokutwa nao washtakiwa hao walikuwa na thamani ya Dola 720,000.

Agosti 22, mwaka huu Hakimu Mkazi Mkuu, Mfawidhi, Isaya Arufani alisoma uamuzi wa kuwaachia huru wachina hao pamoja na mambo mengine mahakama yake iliamuru serikali kulipa mali hizo pamoja na hati zao za kusafiria.

0 comments:

HII NDIYO AJALI ILIYOTOKEA KIKATITI JIJINI ARUSHA JANA

Mwili wa mwanamke anayedaiwa kuwa mke wa mmiliki wa hoteli na klabu ya AQ baada ya ajali.

Basi la Mrindoko Trans baada ya ajali hiyo.

Gari dogo lililogongana na basi.

Mwanamke aliyepoteza maisha katika ajali hiyo enzi za uhai wake.

AJALI mbaya iliyolihusisha basi la Mrindoko Trans na gari dogo lililokuwa linaendeshwa na mwanamke anayedaiwa kuwa mke wa mmiliki wa Hoteli na Klabu ya AQ iliyopo jirani na stendi ya mabasi jijini Arusha ilitokea jana jioni maeneo ya Kikatiti mkoani Arusha.
Katika ajali hiyo, mwanamke huyo alifariki dunia papo hapo.

0 comments:

EWURA YASHUSHA BEI YA MAFUTA NI KUANZIA KESHO JANUARI 7, 2015‏

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), Felix Ngamlagosi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, kuhusu mwenendo wa bei za mafuta nchini na katika soko la Dunia. Kulia ni Mkurugenzi wa Petroli, Godwin Samwel.

Mkurugenzi wa Petroli, Godwin Samwel (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Ofisa Mawasiliano wa Ewura, Titus Kaguo (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Dotto Mwaibale
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), imepunguza bei za mafuta kote nchini kuanzia leo kutokana na kudorora kwa uchumi wa bara la ulaya.
 
Hayo yalibainishwa  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), Felix Ngamlagosi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mwenendo wa bei za mafuta nchini na katika soko la Dunia.
Alisema kuanzia leo bei ya mafuta ya petroli kwa lita moja itauzwa sh.1955 na hiyo inatokana na kushuka kwa jumla ya asilimia 16 sawa na pungufu kwa jumla ya sh.311 kwa lita.
Alisema bei ya petroli katika soko la dunia imeshuka kwa jumla ya aasilimia 25 kuanzia Julai hadi Novemba 2014, sawa na pungufu kwa jumla ya dila 249 kwa tani.
Ngamlagosi alisema mafuta ya dizeli kwa lita moja yatauzwa sh.1846 na kuwa bei hiyo imeshuka kwa asilimia 13 sawa na pungufu kwa jumla ya sh.244 kwa lita na kuwa dizeli kwa soko la dunia imeshuka kwa jumla ya asilimia 28 kuanzia Julai hadi Novemba 2014 sawa na pungufu kwa jumla ya dola 189 kwa tani na kuwa mafuta ya taa yatauzwa sh. sh.1833 kwa lita.
 
Alisema katika kipindi cha robo ya mwisho wa mwaka kuanzia mwezi Septemba hadi Desemba 2014, bei za mafuta ghafi zimekuwa zikishuka kwa kasi ikilinganishwa na kipindi cha hapo nyuma ambapo zimeshuka toka dola 100 kwa pipa hadi kufikia wastani wa dola 60 kwa pipa moja ambayo ni sawa na  karibu asilimia 40.
 
Alisema viwango hivyo vya bei iliyopungua ni katika soko la Dar es Salaam na mikoa mingine bei zao zimepangwa kutokana na kuwepo kwa gharama za usafirishaji.
 
Ngamlagosi alitoa mwito kwa wanunuaji wa mafuta hayo kuhakikisha wanapatiwa lisiti baada ya kununua kwani itasaidia kuwabaini wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wataendelea kuuza kwa bei ya zamani.
 
"Natioa mwito wa kuwaomba wanunuaji wa mafuta kuhakikisha wanapewa lisiti kwani itatusaidia kuwabaini wale wanauza kwa bei ya juu, na pia itamsaidia mnunuzi iwapo atauziwa mafuta yaliyochini ya kiwango na ukusanyaji wa kodi ya serikali" alisema Ngamlagosi.
 
Naye Mkurugenzi wa Petroli, Edwin Samwel alisema Ewura imejipanga vizuri kuhakikishha hakuna ujanja ujanja utakaojitokeza wa kudai mafuta yamekwisha au yaliyopo yatauzwa kwa bei yaliyonunuliwa.
 
Alisema mfanyabiashara yeyote atakayekiuka utaratibu huo atachukuliwa sheria pamoja na kufungiwa biashara yake ingawa alisema hali hiyo haitajitokeza.

0 comments:

POLISI DAR WAZIMA VURUGU KWA MABOMU YA MACHOZI



Polisi jijini Dar es Salaam wamelazimika kufyatua risasi hewani na kupiga mabomu ya machozi kufuatia kuibuka kwa vurugu katika hoteli ya Land Mark ambapo shughuli ya uapishaji wa wenyeviti wa Serikali za Mitaa ulikuwa ukifanyika.
Vurugu hizo, zimeibuliwa na kambi ya upinzani ambayo ilikuwa ikilalamikia kuwa Mwenyekiti mmoja wa Chama tawala CCM aliyeapishwa hakuwa ameshinda katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika mwaka jana.



0 comments:

WAKUBWA TU Picha,Mwanamitindo aliyetoa mbavu mbili ili awe na umbo namba nane.

Mwanamitindo na stripper maarufu kutoka Miami ‘Estrelle’ amefanya maamuzi ya mugumu ili kupata muonekano aupendao. Model huyu wa video na matangazo amekubali kutolewa mbavu zake mbili ili apate umbo namba 8.

Mwana mitindo huyu alikwenda Miami kwenye hospitali maarufu inayofanya zoezi hilo ambalo limetajwa kuwa ni hatai sana na kupona kwa mgonjwa inaweza kuchukua mpaka miezi 6 kupona.
nomaa 2

nomaa 1

nomaa 3

nomaa 4
Baada ya zoezi kufanyika alikuwa hivi

0 comments: