Spika
wa Bunge la Jamhuri, Anne Makinda akieleza jambo Januari 31, 2015
Bungeni mjini Dodoma ambapo mkutano wa 18 wa Bunge hilo unaendelea.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji George Masaju akitoa ushauri kwa Bunge la Jamhuri.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Dkt. Festus Limbu, akijibu hoja za wabunge waliochangia kwenye taarifa yake.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akijibu hoja za kamati zilizoelekezwa katika wizara yake.
Mbungge wa Kawe, Halima Mdee akitoa mchango wakati wa kujadili taarifa za kamati za Bunge, bungeni mjini Dodoma.
Habari Picha na Hussein Makame-MAELEZO, Dodoma
………………………………………………………………………………………..
KAMATI
za Bunge za Serikali za Mitaa (LAAC) na ile ya Hesabu za Serikali
(PAC), zimeridhishwa na mafanikio na hatua zilizochukuliwa na Serikali
kwa kuongeza mapato yake na kushughulikia changamoto zinazoikabili
katika kutekelza majukumu yake.
Kufuatia
hali hiyo, Bunge limepitisha taarifa za kamati hizo na nyingine tatu,
huku Serikali ikiahidi kufanyia kazi yale yote yaliyopendekezwa kwenye
taarifa hizo ili kulipeleka Taifa kule kunakotakiwa.
Taarifa
za Kamati ambazo Bunge limezipitishwa jana na juzi usiku ni za Kamati
ya Bajeti, Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Hesabu za Serikali (PAC),
Miundombinu na Nishati na Madini.
Akihitimisha
hoja yake, Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC Rajabu Mbarouk aliipongeza
Serikali na Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia kwa hatua alichokua kwa
watendaji wa Serikali waliobainika kutumia vibaya fedha za umma.
“Mimi
ni mpinzani lakini kwa hili, kwa kweli nimpongeza Waziri kwa sababu
jana aliniletea list (orodha) karibu ya halmashauri zote nchini ambazo
wakurugenzi amewachukulia hatua, kilichobaki ni mimi kuichukua ile
taarifa na kumpelekea kwa CAG kwa ajili ya kuihathibitisha” alisema
Mbarouk.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Zitto Kabwe aliipongeza Malmalaka ya
Bandari Tanzania (TPA) kwa kuongeza mapato na kwamba wameiomba iongeze
mapatao katika miaka ijayo ili kuifanya mamlaka hiyo iwe na tija kwa
taifa.
“Ni
lazima tuwe wakweli, Mamlaka ya Bandari imeongeza sana sana ufanisi
katika kazi zake, mapato yameongezeka kutoka shilingi Bilioni 320 mpaka
shilingi Bilioni 537 katika kipindi cha miaka miwili” alisema Zitto.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba aliithibitishia
kamati na wabunge waliotoa michango yao kuwa wamepokea michango yao na
wataifanyia kazi.
“Kwanza
nisema ndugu Mwenyekiti, tumewasikia wabunge, tumepokea waliyoyasema na
tutayafanyia kazi, tupo kwa ajili hiyo” alisema Naibu Waziri Nchemba.
Alisema
tangu mwaka wa fedha ulipoanza, mkakati wa Wizara chini ya usimamizi wa
Waziri wa Fedha ilikuwa ni kuhakikisha kila fedha inapokusanywa
inakwenda pale ilipokusudiwa.
Alifafanua
kuwa hata hoja za baadhi ya wabunge kuwa kuna miradi imepata mgawo
sifuri, inawezekana hiyo sifuri ni ya fedha zile zinazotoka nje.
“Naongea
hili kwa uhakika, mwaka wa fedha uliooanza tu tulitoa Bilioni 500 kwa
ajili ya miradi ya maendeleo na mpaka wizara zingine wakashangaa
wakauliza hizi fedha mmekosea au ndivyo kweli zinatakiwa zije” alisema
na kuongeza:
“Walidhani
ni za mishahara, haikuzoeleka kutokea fedha nyingi ndani ya mwezi wa
kwanza wa bajeti kwa ajili ya shughuli za maendeleo”
Hivyo
aliwaomba wabunge wazingatie mambo mamwili, moja Waziri ameweka
utaratibu kwamba kila taasisi inapopokea fedha za maendeleo ni lazima
ipeleke mrejesho imetumia fedha zile kwa shughul gani na mradi ule
uonekane kabla fedha zingine hazijakwenda.
Alisema
jambo la pili ni nia ya Serikali kuhakikisha kwamba fedha zilizotengwa
kwa ajili ya mifuko na matumizi maalum ya miradi ya maendeleo na kwamba
kuanzia mwezi Februari wanarekebisha utaratibu wa kutengeneza mchanganuo
wa fedha kuhakikisha fedha hizo zimekwenda kwenye miradi ya maendeleo.
Mkutano
wa 18 wa Bunge la Jamhuri unatarajiwa umeahirishwa hadi Jumatatu ambapo
bunge hilo linataraji kupokea taarifa za Kamati ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Mazingira na Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji.
Read More »