Simba yamsajili beki wa Mtibwa. Ingia Hapa Kwa Habari Kamili

0 comments

hassan kessy

Katika usiku ambao umekuwa na movement nyingi za wachezaji na makocha , klabu ya Simba imekamilisha usajili wa beki wa pembeni toka timu ya Mtibwa Sugar Hassan Kessy .
Beki huyo ambaye ametokea kuwa moja kati ya wachezaji wa kutmainiwa kwenye klabu hiyo ya wakata miwa wa huko Manungu Turiani mkoani Morogoro anaungana na wachezaji wapya waliosajiliwa katika kipindi hiki cha dirisha dogo ambao ni Simon Sserunkuma , Danny Sserunkuma , na Juko Murshid wote toka Uganda .
Kessy ambaye ametajwa kuwa moja kati ya wachezaji wanaokaribia kutiwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars aliicheza Mtibwa kwa mara ya mwisho katika mchezo wa kirafiki ambao ilifungwa na Azam Fc 3-1 .
Beki huyu anasajiliwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu yaliyofanyika chini ya usimamizi wa viongozi wa Simba wakiongozwa na Geoffrey Nyange Kaburu na Kiongozi wa Mtibwa Jamal Bayser .
Tetesi zaidi zinasema kuwa Simba imemsajili beki huyo kwa thamani ya shilingi milioni 30 .

Read More »

Breaking News Rasmi…Marcio Maximo aondoka Yanga. Ingia Hapa Kwa Habari Kamili

0 comments


maximo+manji+leo.tif
Habari rasmi toka ndani ya klabu ya Yanga zinasema kuwa kocha Mbrazil Marcio Maximo ameondoka ndani ya klabu hiyo .
Habari hizi zinakuja dakika chache baada ya Maujanjayamjini kuripoti tetesi zinazohusu mustakabali wa kocha huyo Mbrazil.
Maximo anaondoka Yanga baada ya uongozi wa klabu hiyo kukubaliana naye kuvunja mkataba wake baada ya kushindwa kuelewana juu ya jinsi ya kuiendesha klabu hiyo kwenye masuala ya ufundi .
Yanga ilishikilia msimamo wa kumuajiri mkurugenzi wa ufundi ambaye alipangwa kuwa Charles Boniface Mkwasa jambo ambalo Maximo hakukubaliana nalo.
Nafasi ya Maximo sas aitachukuliwa na Mholanzi Hans Van Der Pluijm ambaye aliifundisha timu hiyo kwa nusu msimu baada ya kufukuzwa kwa Mholanzi mwenzie Ernst Brandts .
Tukio hili linaendeleza historia ya Yanga kufukuza makocha baada ya kufungwa na Simba kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe baada ya kufukuzwa kwa Ernst Brandts msimu uliopita kufuatia kipigo cha 3-1 mbele ya Simba iliyokuwa inaongozwa na Dravko logarusic.

Read More »

Breaking News , Yanga yamsajili Amisi Tambwe toka Simba. Soma Hapa Kwa Habari Kamili

0 comments



tambwe yanga
Taarifa zilizoingia kwenye mtandao huu dakika chache zilizopita ni kwamba Dar-es-salaam Young Africans imemsajili mshambuliaji wa Simba aliyeachwa Amisi Tambwe .
Yanga imemsajili Tambwe dakika chache zilizopita ambapo anakuja kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Hamis Kiiza ambaye amejiunga na URA ya Uganda .
Tambwe amesajiliwa na Yanga baada ya kuachwa na Simba.
Tambwe amesajiliwa na Yanga baada ya kuachwa na Simba.
Tambwe alikuwa mfungaji bora wa ligi msimu uliopita ambapo alifunga mabao 19 kwenye ligi lakini alishindwa kuwika msimu huu baada ya kutopewa nafasi ya kutosha chini ya Patrick Phiri.
Simba imemuacha Tambwe baada ya kumsajili Danny Serunkuma toka Gor Mahia ya nchini Kenya .
Yanga imekamilisha usjaili huu saa chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa kama ilivyopangwa na Tff .

Read More »

HAUSIGELI ALIYEMTESA MTOTO UGANDA AHUKUMIWA MIAKA 4 JELA

0 comments

 Jolly Tumuhirwe (22).

HAUSIGELI aliyenaswa kwenye video akimtesa mtoto nchini Uganda, amehukumiwa kwenda jela miaka minne katika mahakama moja nchini humo.


Jolly Tumuhirwe wakati akimtesa mtoto Arnella mwenye miezi 18.

Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe (22) aliiambia mahakama kuwa anajutia kile alichokifanya na anaomba msamaha kwa familia na jamii nzima.
Amehukumiwa kwa kosa la kumtesa mtoto Arnella mwenye miezi 18.

Read More »

ROLENE STRAUSS WA AFRIKA KUSINI ASHINDA TAJI LA MISS WORLD 2014

0 comments


Miss World 2014, Rolene Strauss wa Afrika Kusini.
Rolene Strauss wa Afrika Kusini ameshinda taji la Miss World 2014 jijini London usiku huu, Edina Kulcsar wa Hungary akishika nafasi ya pili na Elizabeth Safrit wa Marekani akichukua nafasi ya tatu.

Read More »

Hii Sasa Kali Check Video ya Mfanyakazi wa hoteli alivyonaswa akipekua vitu vya mteja chumbani Ingia Hapa Kwa Habari Kamili

0 comments
Screen Shot 2014-11-12 at 8.46.26 PM
Ni jinsi mfanyakazi wa hoteli alivyorekodiwa na camera ya Laptop ya mteja alieiacha kwenye chumba cha hoteli na kuacha funguo reception, baada aliporudi akajionea jinsi mfanya usafi huyo alivyopekua na kugusagusa vitu vyake.

     VIDEO IPO HAPO CHINI CLICK KUITAZAMA


Read More »

Ni Happiness Watimanywa… Tanzania kwenye rekodi nyingine kubwa Miss World 2014 Soma Hapai Kwa Habari Kamili

0 comments

Happyz iiiWatanzania wameamua kwamba tukiamua tunaweza, good news kutoka London Uingereza, ambako yanafanyika mashindano ya Miss World mwaka 2014.
Happiness Watimanywa, mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano hayo ameshare na sisi taarifa nyingine nzuri kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Happiness kaandika hivi; Hey guys. Siwezi amini kuwa tumefika namba 2. Tuongeze bidii maana nchi nyingine pia wako bize na kura. Lets do this Tanzania!!!! Naamini pamoja tutafika. #votevotevote #PigaKuraSasa#DownloadTheApp#HuuNiMwakaWetu“– @happinesswatimanywa
Happyz

Happyz II Happyz IIii

Zoezi la upigaji wa Kura litasitishwa leo December 14, jioni ambapo Fainali hizo zitakuwa zinafanyika London, Uingereza.
Unaweza kuendelea kumpigia kura mshiriki huyo ili arudi na Taji la Miss World 2014.

Read More »

Jamani Jamani Hivi ndivyo Whatsapp imevunja ndoa ya wawili hawa…

0 comments

whatsapp2 
Wiki chache baada ya WhatsApp kutambulisha mfumo mpya ambapo iwapo unamtumia message mtu inakuonyesha alama ya tick mbili za kijani na pia inaonyesha muda ambao mtu uliyemtumia message hiyo ameisoma, tayari kuna ndoa ambayo imeingia matatizoni kutokana na hilo.
Mwanaume mmoja Saudi Arabia ametoa talaka kwa mkewe kutokana na kitendo cha mwanamke huyo kutokujibu message aliyomtumia WhatsApp.
Mwanaume huyo amesema kitendo kilichomkasirisha zaidi ni pale aliporudi nyumbani na kumkuta mke wake akiwa busy anachat na marafiki zake kupitia mtandao huo wakati message aliyomtumia yeye hakuijibu.
dreamstime_s_36639295-600x399
Jamaa huyo ameona kama kitendo hicho ni dharau kubwa na hakuwa tayari kuendelea na ndoa hiyo ambayo imedumu kwa miaka miwili tangu ifungwe.

Read More »

Mke afumaniwa, amgeuzia kibao mme wake Polisi… Unajua kilichomfanya amsaliti?

0 comments
Black-Couple-in-Bed-PFJamaa mmoja alisababisha kizaazaa baada ya kuvamia chumbani ambako mtu na mkewe walikuwa wamelala.
Fununu zinasema jamaa huyo baada ya tukio hilo alimhoji mkewe kwamba huyo aliyeingia bila hodi chumbani kwao wakiwa wamelala ni nani?
Baada ya jamaa huyo, Calvin Murapata kutoridhishwa na majibu ya mke wake Nomagugu Ncube alimpiga na kumchania nguo, ambapo mwanamke huyo alifungua mashtaka kituo cha Polisi, Zimbabwe.
Mwanamke huyo aliwahi kushinda taji la mitindo katika nchi hiyo, amekiri kuwa na uhusiano na jamaa huyo aliyevamia chumbani humo kutokana na mume wake kuwa busy.
Ncube amefungua mashtaka kudai fidia ya nguo alizochaniwa.

Read More »

List kamili ya Walioshinda Tuzo za TASWA 2013/2014 iko hapa, yupo aliyechukua Jumla ya Tuzo tatu

0 comments
gold-star-award-375x250Siku ya jana December 12 kulikuwa na Sherehe za Utoaji wa Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania mwaka 2013/2014, zilizotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ambazo zilifanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, ambapo Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo alikuwa Rais Wa Zanzibar, Dr. Ali Mohamed Shein
Tuzo kubwa ya kwanza iliyotolewa usiku wa jana ni Tuzo ya Heshima ambayo ilitolewa kwa Hayati Sheikh Abeid Aman Karume na kupokelewa na Mama Fatma Karume.
Sheridah Boniface alivunja Rekodi kwenye sherehe hizo baada ya kutoka na jumla ya Tuzo tatu, Tuzo ya Jumla ya Mwanamichezo Bora 2013/ 2014, tuzo ya Mwanamichezo Bora Chipukizi na Tuzo ya Mchezaji Bora wa Soka Wanawake.
Wachezaji wa Azam, Erasto Nyoni na Kipre Cheche baada ya kupokea tuzo zao.
Wachezaji wa Azam, Erasto Nyoni na Kipre Cheche baada ya kupokea tuzo zao.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Gofu Wanawake imechukuliwa na Madina Iddy.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Gofu imechukuliwa na Nuru Mollel.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Gofu Wanawake imechukuliwa na Madina Iddy.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Gofu ya Kulipwa imechukuliwa na Hassan Kadio.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Kikapu Wanaume imechukuliwa na Lusajo Samweli.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Kikapu wanawake imechukuliwa na Sajda Ahmed Lyaimaga.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Wavu Wanaume imechukuliwa na Kelvin Peter Severino.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Wavu Wanawake imechukuliwa na Teddy Abwao.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Magongo Wanaume imechukuliwa na Yohana Wilson.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mpira wa Magongo Wanawake imechukuliwa na Kidawa Seremala.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Soka Wanaume imechukuliwa na Erasto Nyoni.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Tenisi Walemavu imechukuliwa na Novatus Emmanuel Temba kwa upande wa Wanaume.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Tenisi Walemavu imechukuliwa na Rehema Selemani Saidi kwa upande wa Wanawake.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Olimpiki Maalum imechukuliwa na Blandina Blasi kwa upande wa Wanawake.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Olimpiki Maalum imechukuliwa na Raphael Kalukula kwa upande wa Wanaume.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Nje anayechezea Tanzania imechukuliwa na Kipre Cheche.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mtanzania anayechezea nje imechukuliwa na Mbwana Samatta.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mpira wa Mikono Wanaume imechukuliwa na Hemed Saleh.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mpira wa Mikono Wanawake imechukuliwa na Veronica Mapunda.
Tuzo ya Mwendeshaji Bora wa Baiskeli imechukuliwa na Richard Laizer kwa upande wa wanaume.
Tuzo ya Mwendeshaji Bora wa Baiskeli imechukuliwa na Sophia Adson kwa upande wa wanawake.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ngumi za Ridhaa imechukuliwa na Bondia Suleiman Kidunda.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa ngumi za Kulipwa imechukuliwa na Bondia Francis Cheka.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Tenisi Wanaume imechukuliwa na Omary Sulle.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Tenisi Wanawake imechukuliwa na Rehema Athumani.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kike mchezo wa Judo imechukuliwa na Grace Alfonce Mhanga.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kiume mchezo wa Judo imechukuliwa na Geofrey Edward Mtawa.
Tuzo ya Mwanariadha Bora wa Kike imechukuliwa na Zakia Mrisho.
Tuzo ya Mwanariadha Bora wa Kiume imechukuliwa na Alfonce Felix.
Tuzo ya Muogeleaji Bora wa Kike imechukuliwa na Catherine Maswa.

Read More »

Matokeo ya Simba vs Yanga – picha na idadi ya watu waliozimia uwanjani vipo hapa

0 comments
Screen Shot 2014-12-13 at 7.09.29 PMTimu ya Simba imeibuka na ushindi baada ya kuichapa timu ya Yanga 2-0 huku timu ya Yanga wakiambulia kuondoka na maumivu ya kushindwa kufurukuta kwa bao hata moja.
Wafungaji wa magoli kutoka timu ya Simba ni Awadh Juma na Elias Maguri ambapo mabao yote yamefungwa katika kipindi cha kwanza.
Kwa mara ya pili tena timu ya SIMBA wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa Nani Mtani Jembe baada ya kutwaa ubingwa huo mwaka jana walipoichapa Yanga bao 3 -1.
Kwa upande wa zawadi Simba wamefanikiwa kutwaa milioni 92 huku Yanga wakiondoka milioni 7.
 Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia bao la pili lililofungwa na Elias Maguli katika dakika ya 40 ya kipindi cha kwanza. Mabao yote ya Simba yamefungwa katika kipindi cha kwanza huku bao la kwanza likifungwa na Awadh Juma katika dakika ya 30.
 Mashabiki wa Simba wakishangilia moja ya mabao yaliyofungwa na timu yao.
 Andreu Coutihno, akimiliki mpira katikati ya mabeki wa Simba…
Mchezaji mpya wa Yanga, kutoka nchini Liberia, Kpah Sherman. akisomba kijiji cha mabeki wa Simba…. Hadi mpira unaisha jumla ya mashabiki wasiopungua wanne wa Yanga walikuwa wameshazimia uwanjani. 
Mashabiki wa Simba waliojaza kwenye dimba la uwanja wa taifa – PICHA ZOTE KWA NIABA YA SUFIAN MAFOTO
                                     Umati wa wana jangwani leo taifa

Read More »

PICHA: WEMA SEPETU NA VAN VICKER WAFANYA MOVIE GHANA, INAITWA ‘DAY AFTER DEATH’ INGIA HAPA

0 comments

Wema Sepetu amesafiri hadi jijini Accra, Ghana kwenda kushoot filamu mpya na msanii mashuhuri nchini humo, Van Vicker.

Filamu hiyo inaitwa ‘Day After Death’, na inaongozwa na  Vicker mwenyewe. Pia mtoto wa kike wa msanii huyo ataigiza kwenye filamu hiyo ambayo Vicker anaiita kitu chake kikubwa kijacho.

Kupitia Instagram, muigizaji huyo wa Ghana amemsifia Wema kwa jinsi anavyojituma kwenye filamu hiyo na anafurahi kufanya naye kazi.
 
“#MyNextBigThing I am excited abt our Ghana Tanzania collaboration. You finally landed. Today was day 1. Good stuff. I love the way you are passionate abt what you want and u get it done. Enjoy workin with you. watch for Day After Death (D.A.D) #DayAfterDeath starring Wema @wemasepetu and me van vicker. I am directing again ya’ll and acting. It’s challenging but I love the challenge. Hey it’s my daughter’s j’dyl debut in films as an actor,” ameandika Van Vicker.
  

“Watch out for #DayAfterDeath (D.A.D) starring @wemasepetu and myself..#DirectorMode Tanzania and Ghana goin on the map for this award winning thriller,” ameongeza kwenye picha nyingine.

Read More »

Dunia na maajabu yake… Hii ni ya gari kutembea kwa tairi mbili tu! Itazame HAPA VIDEO

0 comments
6fc
Huenda wewe ukawa mmoja ya watu ambao wanaogopa michezo ya hatari.
Ipo michezo ambayo hata ukiona mtu anaifanya nafsi yako inakiri kwamba kamwe hauwezi kuifanya.
Hii nmeikuta Youtube, jamaa wa Saudi Arabia wanaendesha gari kwa kutumia tairi mbili peke yake, na kali zaidi ni kwamba wengine wanajiamini na hata kubadilisha tairi za gari wakati ikiwa inatembea.
Video nimekuwekea hapa halafu nitafurahi kuona comment yako mtu wangu.

Read More »

ZARI SEXTAPE: MY EX LOVER LEAKED IT

0 comments

Zari has today morning  blamed her ex lover for leaking the sextape.


zaris
“Life goes exs gotta stay exs and stop doing things for renege,” Zari tweeted shortly after The Red Pepper published pictures of her sextape.
For exclusive pictures and a clear description of how Zari moans in bed, Please hurry and Grab Red Pepper copies of Friday and Saturday from the nearest vendor.

READ MORE ON: ugandaonline.net

Read More »

WATU 2 WAPIGWA NA KUVULIWA NGUO NA KUBAKI UCHI NYUMBANI KWA WEMA, NI MAFUNDI WAKE WALIODAIWA KUIBA...MZIKI WAPANDISHWA MPAKA MWISHO KUMBE KICHAPO KINATEMBEZWA NDANI ILI MAJIRANI WASISIKIE!!

0 comments
Nyumba ya wema 1
Wema akiwa ndani kwake

Nyumbani kwa Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu, Wema Sepetu, kumetokea tukio la kushangaza la watu wawili wanaodaiwa kuwa mafundi, kupigwa na kudhalilishwa kwa kuachwa uchi wakidaiwa kuhusika na wizi.

Akizungumza na paparazi jana, jirani wa Wema aliyetambulika kwa jina la Mama Steve, alisema tukio hilo lilitokea Ijumaa majira ya saa 5 asubuhi mpaka saa 9 jioni.
“Waliopigwa na kulazwa chini uchi wa mnyama ni mafundi ambao wanakujaga kila siku kumtengenezea Wema nyumba yake,” amesema mama huyo. “Sasa baada ya kumaliza kazi yao wakaondoka, baada ya kuondoka wakaitwa tena na kuambiwa kuna simu imeibiwa ndani, ndo mtiti ukaanza.”
“Petit akatumwa akachukue mabaunsa 7 na baada ya kufika wakapandisha muziki mpaka mwisho ili sisi tusisikie nini kinaendelea huko ndani. Sasa kuna mtu alikuwa anapita hapa kwenye geti lao akasikia mtu analia sana ikambidi akachungulie ndo akamkuta fundi watu wawili wamelazwa chini uchi wa mnyama wanapigwa na hawana nguvu kabisa! Ndo yule jamaa kwakuwa alikuwa anamjua yule fundi akaita watu wakaanza kugonga geti ili wafungue lakini hawajafungua geti. Tukawa tunasikia sauti ya Wema ikisema ‘jamani waacheni hao mtawaua’ lakini anasema hivyo wakati yeye inaonyesha ndo alikuwa kinara wa matukio hayo.

Wema ana roho ya kikatili sana. Amefanya matukio mengi lakini hivyo hapana! Yaani kama anataka usalama wake anatakiwa ahame vinginevyo vijana watamfanyika tukio la kinyama sana,” ameongeza mama huyo.
“Baada ya watu kuwa wengi sana pale nje ndo geti likafunguliwa watu wakaingia na kuwachukua wale vijana wakiwa hawajitambui na wapo uchi ndo wakapelekwa hospitali. Sasa baada ya kupelekwa hospitali polisi wa kituo cha Mabatini na wao wakagonga geti wakawa hawataki kulifungua polisi wakapindukia na kuingia ndo wakawakamata baadhi ya watu na kuondoka nao. Hilo ndo tukio alilolifanya mwanadada wenu ambaye anadai alikuwa Miss Tanzania,” alisema Mama Steve.

Pia shuhuda mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mama Samira, alisema amesikitishwa na tukio hilo la kinyama. “Hii ni tabia yake, hata wafanyakazi wake wa ndani anao kaa nao saa zingine anawapiga makofi! Kwakuwa ni ndani kwa ndani sisi majirani hatufuatilii, lakini kwa hilo na sauti yake tumeisikia japo watu wake wanadai hakuwepo,” alisema.
Baada ya taarifa hiyo, paparazi ilimtafuta mjumbe wa nyumba kumi, Mwarami ambaye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akidai hataki kuliongelea sana kwakuwa limeshafika katika kituo cha polisi Mabatini. Pia paparazi ilifika katika kituo cha polisi Mabatini ili kujua nini kinaendelea katika tuhuma hizo lakini iliambiwa kumuona mkuu wa kituo ambaye hata hivyo hakuwepo kwa muda huo.
Mtu wa karibu wa Wema, Petit Man aliyetajwa kuhusika kwenye tukio hilo, ameiambia paparazi kuwa watu hao walipigwa lakini hawakuvuliwa nguo. “Yeah kuna tukio limetokea,lakini hakuna mtu aliyevuliwa nguo,” alisema Petit na baada ya hapo alikata simu.
Unaweza kumsikiliza Mama Samira hapo chini.

Read More »

BEAUTY WITH DRYNESS: DESCRIBING ZARI’S SKYPE SEXTAPE

0 comments

Zari was thumped by her hubby Ivan


Zari was thumped by her hubby Ivan

Ugandans now have a reason to believe that not all that glitters is gold after watching Zari’s Skype sextape.

Red Pepper online understands that Zari’s Skype sextape was recorded last year.
In the Skype sextape, Zari is seen satisfying herself with a Dildo.
She was heard hissing and moaning whenever she inserts the dildo in her unshaven eclipse.
Oh, oh, yeah! Moaning is a way for people to communicate or express excitement and pleasure; Zari must have had total pleasure during the Skype sex session.
Women moan as a signal to let their partner know that the sensation feels good.
Zari uttered hissing sounds and made her body move freely as if she lost control and allowed herself to be part of the sexual and satisfying experience.
The worst turnoff in the Skype sextape, Zari tops the list of the driest babes on the planet.
As she slowly inserted her dildo in the bearded eclipse, we expected to see El Niño flowing uncontrollably from her eclipse. Zari is a walking combination of Kalahari and Sahara deserts.
Her dryness confirmed that she has low libido or she was not sexually aroused.
The other turnoff was her bushy eclipse that could be mistaken as Mabira forest.

Read More »

Tuzo nyingine aliyoshinda Diamond Platnumz Nigeria. Na soma davido alichokiandika Kuhusiana na Tuzo Hii Aliyoshinda Diamond

0 comments


tuzoDiamond Platnumz ameshinda tuzo nyingine ambayo hizi zilikua zikitolewa Lagos nchini Nigeria ambazo hizi hazikuwa na utaratibu kama wa tuzo zingine kwa kupiga kura.
Baada ya kushinda tuzo hiyo ambayo ilienda kupokelewa na Meneja wake Salaam,Diamond alipost maneno haya>>’Thanks God,we have cheated another one on the future Awards Africa in Lagos Nigeria…#samenight Thank you Allah’
Tuzo hizi zinaitwa The Future Awards Prize in Entertainment ambapo kipengele alichokuwa akiwania Diamond alikuwa na wakali mbalimbali akiwemo Panshack au Ice Prince jina lake la zamani wa Nigeria na Michael Kwesi wa Ghana.
dngria

Read More »

Historia nyingine kubwa ya Tanzania imeandikwa fainali ya #BBAHotshots 2014

0 comments
IdrisLeo ni siku ya 63 tangu yaanze mashindano ya Big Brother Africa, ndiyo siku ambayo imefanyika fainali ya #BBAHotshots kwa mwaka huu 2014.
Labda nikukumbushe kwamba Tanzania ndiyo nchi pekee iliyokuwa imebakiwa na mshiriki wake ndani ya Jumba la BBA katika ukanda wa Afrika Mashariki na tuliona namna ambavyo mastaa wengi wakitoa support kubwa kwa mshiriki huyo ambaye ni Idris.
Hatimaye usiku huu wa Desemba 07 historia nyingine imeandikwa Afrika, ambapo mwakilishi huyo kafanikiwa kuibuka mshindi.

Read More »

MTUHUMIWA WA UGAIDI ARUSHA AFARIKI MIKONONI MWA POLISI

0 comments

Hatimaye Abdulkarimu Thabiti Hasia aliyekuwa akituhumiwa kwa ugaidi, amefariki katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru alipokuwa amelazwa kwa miezi sita akiwa mikononi wa polisi.
 
Taarifa ya kifo cha Hasia aliyekuwa mmoja wa maimamu wa Msikiti wa Geti la Mbao Mbauda, ilitolewa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Arusha wakati kesi ya mtuhumiwa huyo na wenzake saba ilipotajwa.
 
Hasia aliyekuwa ni mshtakiwa wa pili katika kesi ya kushambulia baa maarufu ya Arusha Naighty Park, alikuwa akikabiliwa na makosa 16 ya ugaidi, amefariki bila kufikishwa mahakamani hata siku moja.
 
Ilielezwa mahakamani hapo jana, mbele ya Hakimu Hawa Mguruta kuwa mtuhumiwa huyo alifariki Desemba mosi, akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.
 

Hata hivyo, wakati taarifa hiyo ikitolewa, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Augostino Komba alieleza kutokuwa na taarifa hiyo, hivyo mahakama iliagiza kubadilishwa hati ya mashtaka.

Baadhi ya ndugu wa marehemu walieleza kwamba tangu alipokamatwa na kupata kipigo katika mahojiano na polisi, Hisia alikuwa amelazwa hadi kifo chake.
 
Kifo cha mtuhumiwa huyo kimekuja wakati kuna malalamiko ya watuhumiwa wengine kupigwa na kujeruhiwa na polisi katika mahojiano na bado wapo gerezani.
 
Septemba 4 mwaka huu, mtuhumiwa huyo alisomewa mashtaka 16 ya ugaidi akiwa amelazwa hospitalini baada ya kupata fahamu.
 
Kabla ya kusomewa mashtaka hayo, marehemu alikuwa ameshalazwa hospitalini hapo kwa takriban miezi minne na awali ilishindikana kusomewa mashtaka kutokana na kutokuwa na fahamu.
 
Kesi ya watuhumiwa wengine wa ugaidi inatarajiwa kutajwa tena Desemba 19 kutokana na kutokamilika kwa upelelezi na watuhumiwa hao walirejeshwa rumande.

Read More »

POLISI NA RAIA WATWANGANA BAADA YA KUFUMANIANA

0 comments
WAKAZI wawili wilayani hapa, wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga baada ya kujeruhiwa katika mapigano kati yao na askari Polisi, baada ya kumshika ugoni mmoja wa askari katika hoteli moja maarufu mjini hapa.
Tukio hilo lilitokea juzi usiku baada ya mmoja wa vijana hao, kumkuta askari akijivinjari na mkewe, ndipo alipomshirikisha ndugu yake na kuibuka mapigano makali ya kurushiana makonde yaliyosababisha baadhi yao kujeruhiana vibaya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha, alisema tukio hilo limetokea baada ya askari, Sajenti Edward kufumaniwa akiwa na mke wa mmoja wa vijana hao aliyejulikana kwa jina la Paschal Matonange (26).
Kamugisha, alisema baada ya kufumaniwa akiwa na mwanamke huyo chumbani, vijana hao walianza kumshushia kipigo huku wakimpiga picha akiwa uchi, hali iliyosababisha vurugu kwenye hoteli hiyo iliyopo nje kidogo na mji wa Kahama.
Kamanda huyo, alisema baada ya vurugu hizo wasamalia wema walijaa eneo hilo na baadhi yao kupiga simu kituo cha polisi ambako askari walifika kujaribu kutuliza vurugu hizo bila mafanikio.
Alisema katika kutuliza ghasia hizo, yalizuka mapigano makubwa kati ya vijana hao na askari polisi, hali iliyosababisha kujeruhiwa kwa baadhi ya askari na vijana hao ambao wamelazwa katika hospitali ya Halmashauri ya Mji.
Aidha, waliolazwa ni pamoja Marco Matonange (27), na mdogo wake Paschal Matonange ambaye ndie mme wa mwanamke huyo aliyefumaniwa akiwa na askari.
Hata hivyo, Kamugisha alisema jeshi lake litamchukulia hatua za kinidhamu askari aliyefumaniwa na mke wa mtu, ambaye pia yumo kwenye kikosi maalumu cha kufanya uchunguzi wa makosa ya jinai, kwa kuwa kufanya hivyo ni utovu wa nidhamu.
“Kimsingi sisi kama polisi hatuhusiki na masuala ya ugoni na askari kwenda pale kwenye tukio hawakwenda kwa ajili ya kufumania, bali walikwenda kwa ajili ya kutuliza ghasia lakini ilikuwa ni kazi kuwakamata hao vijana, mpaka sasa pamoja na wao kujeruhiwa pia baadhi ya askari wamejeruhiwa,” alisema Kamugisha.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya, alisema suala hilo  kwa kutumia nafasi yake ya uenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, analifanyia kazi kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi.
“Ni kweli tukio hilo ninalo, vyombo vyangu vya usalama vinalifanyia kazi ikiwemo uchunguzi ili kujua hasa chanzo chake kilichosababisha kuwepo kwa mapigano hayo,” alisema Mpesya ingawa mmoja wa majeruhi hao alidai mkuu huyo ndie aliyewakoa wakati wakipata kipigo kituo cha polisi baada ya kupiga simu kwa mkuu wa polisi Wilaya (OCD).
Akizungumzia tukio hilo katika Hospitali ya Mji wa Kahama, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, aliyefika kuwapa pole majeruhi, alisema jeshi la polisi linatakiwa kufanya kazi kwa misingi ya sheria.
Mgeja, alimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP), Ernest Mangu, kuhakikisha anafanya uchambuzi wa askari wake wasiokuwa na nidhamu ambao hutekeleza majukumu yao kwa vitisho, hali inayosababisha wananchi kukosa imani nao.
Mganga mkuu wa Hospitali ya Mji wa Kahama, Deogratius Nyaga, alisema hali za majeruhi hao zinaendelea vizuri.

Read More »

LILE SAKATA LA MWANAFUNZI ALIYEFANYA MTIHANI MARA MBILI NA KUONYESHWA MAJIBU AFUTIWA MATOKEO‏ YAKE YOOTE RASMI

0 comments

BABA YAKE AMBAYE NI MRATIBU ELIMU KATA AVULIWA   WADHIFA

MWALIMU MKUU ALIYESHIRIKIANA NAYE APEWA ONYO KALI

BAADA ya Mtandao huu kuibua tuhuma na mwanafunzi Monica Masunga kufanya mtihani wa darasa mara mbili katika shule tofauti mbili zilizo kata moja mwanafunzi huyo sasa amefutiwa matokea ya mtihani wa darasa la saba mwaka huu 2014.

Uchunguzi wa Mtandao huu ulibaini kuwa mwanafunzi Monica Sayi Masunga (15) ambaye baba yake ni Mratibu Elimu kata katika kata ya Kakubilo 
alimaliza darasa la saba mwaka jana katika shule ya msingi Kakubilo ambapo bada ya matokea kutoka hakuwa amefaulu mtihani huo .

Matokeo ya Monica katika mtihani wa mwaka jana yalionesha Somo Kiswahili alipata alama C,Kiingereza D, Maarifa alama C, Hisabati D, na Sayansi alipata alama D hivyo wastani wake kwa masomo yote ukiwa alama D ambao haukumwezesha kufaulu.

Uchunguzi zaidi ulibaini kuwa mwanafunzi huyo aliingizwa kinyemela na kusajiriwa kuwa mtahiniwa wa mtihani wa darasa la saba mwaka huu 2014 akifanya mtihani huo katika shule ya msingi Kawawa ambako alisajiriwa kwa jina la Monika silya Masunga akitofautishwa kidogo na jina la mwaka jana alilofanyia mtihani.

Mwanafunzi huyo alionekana shule ya msingi Kawawa siku ya mtihani ambako muda wote kabla ya mtihani alikuwa nyumbani bila kusoma hali iliyowafanya hata wanafunzi wa shule hiyo kushangaa kuwa na mtahiniwa mwenzaoambaye hawakuwahi kumuona katika shule hiyo ,walimu kwa maelekezo ya Mratibu huyo walionywa kutomtilia shaka.

Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Geita baada ya chapisho la habari hii ulilazimika kutuma ujumbe wa maafisaelimu wawili Stephene Mase Afisaelimu taaluma na Heri Bihemo Afisaelimu ya Watu wazima ambao walifika shule ya msingi Kakubilo alikofanyia mtihani mwaka janana kisha shule ya msingi Kawawa alikofanya mtihani mwaka huu.

Walibaini viashiria vya kuwepo udanganyifu na ukiukwaji mkubwa maadili kutokana na kukuta mwanafunzi huyo kuonekana kufanya mtihani mara mbili kinyume kabisa na sheria ya elimu ya mwaka 1978.

Baada ya kufikisha tarifa hiyo Afisaelimu wa wilaya Deus Seif alilazimika kuunda tume kutoka Ofisi ya ukaguzi wa shule kwa ajili ya kwenda kufanya uchunguzi wa kina kisha kutoa majibu ya uchunguzi wa kwa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya .

Uchunguzi wa tume hiyo ulibaini kuwa mwanafunzi huyo ni kweli alifanya mtihani mara mbili katika shule mbili tofauti kwa maagizo ya Mratibu Elimu Kata Masunga akiwa baba wa mwanafunzi huyo kwa kubadilisha taarifa ili ionekane Monica alianzia darasa la kwanza s/m Kawawa .

Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri ya wilaya ya Geita Ally Kidwaka alisema amepokea taarifa ya uchunguzi huo kwa masikitiko makubwa kutokana na jinsi elimu inavyochezewa tena na watu waliopewa dhamana ya kuongeza sekta hiyo muhimu kwa ustawi wa taifa letu.

Alisema tume ilipomhoji mwalimu mkuu aliyekuwa shule ya msingi Kawawa Chobabona Michael ambaye kwa sasa alihamishiwa shule ya msingi Njingami ambaye ndiye alimsajiri mwanafunzi huyo kinyemela ili aweze kufanya tena mtihani mwaka huu alikiri mbele ya tume kufanya udanganyifu huo.

Aidha Mkurugenzi huyo alisema hata mratibu huyo wa elimu naye alikiri mbele ya tume kutoa maelekezo kwa mwalimu mkuu wa shle ya Kawawa kuhakikisha mtoto wake Monica anasajiriwa kufanya mtihani akikiri kukiuka taratibu za kielimu ambako alimwelekeza Afisaelimu wa wilaya kuchukua hatua kali.

Alipofuatwa na Mtandao huu kuelezea jinsi alivyopokea matokea ya uchunguzi huo Afisaelimu Deus Seif alilimwagia sifa Mtandao huu kwa kuifumbua macho wilaya hiyo juu ya hujuma zinazofanywa za kuzalisha wasomi feki na kufanya wasiostahili kufaulu mitihani.

Alisema maamuzi yaliyochukuliwa dhidi ya Mratibu elimu kata huyo ni kwamba amevuliwa wadhifa wake huku mwalimu Chobabona aliyekubali kukiuka sheria ya Elimu amepewa barua ya onyo kali ,akisema pia kuwa mwanafunzi huyo ambaye alikuwa amefaulu matokea yake yamefutwa.

Matokeo ya mwanafunzi Monica ambaye pia alikiri kuoneshwa majibu ya mtihani katika mtihani wa mwaka huu Kiswahili ana alama B, Eglish D,Maarifa C, Hisabati D na Sayansi ana alama C Wastani wake wa jumla ni alama C.

Monica alianza darasa la kwanza katika shule ya msingi Buligi mwaka 2007 kabla ya kuhamia shule ya msingi Kakubilo mwaka 2011 akiwa darasa la tano ambako aliandikishwa kwa namba 4548 ambapo mwak jana alikwa miongoni mwawanafunzi 78 wa shule ya msingi kakubilo waliofanya mtihani akitumia namba ya mtihani PS 2404051/062.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kakubilo Magessa Mashabala alisema Monica alikuwa mwanafunzi wake tokea 2011alipohamia hapo akitokea shule ya msingi Buligi alikoanzia darasa la kwanza ambako kabla ya kupandishwa cheo baba yake alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Buligi.

Aliposajiriwa kinyemela shule ya msingi Kawawa Monica alipewa namba za usajiri 530 na kuonekana kuwa alianzia hapo darasa la kwanza hadi darasa la saba namba yake ya mtihani mwaka huu ikiwa ni PS 2404064/O83.

Kitabu cha mahudhurio ya kila siku ya wanafunzi cha shule ya msingi Kawawa kilionesha Monica amehudhuria siku zote shuleni bila kukosa hata siku moja huku ikionesha wazi kuwa kilitkitabu kipya cha mahudhurio na kumwingiza Monica kisha kuweka alama ya vema kuonesha hakuwahi ukosa shule hata siku moja.

Mbaya zaidi mwanafunzi huyo kwa maelekezo ya baba yake yake aliaidiwa kufanya mtihani ambap alikiri kupewa majibu ambayo ndiyo yalimsaidia kufaulu mtihani wa mwaka huu.

Alipozungumza na Mtandao huu Monica alikiri kupewa majibu ambapo alisema yeye baada ya kufeli mtihani mwaka jana akijijua uwezo wake kiakili kuwa mdogo alimuomba baba yake kumtafutia cherahani ili mapeleke akijifunze ushonaji.

Alisema baba yake alimwambia asubiri ataenda kufanya tena mtihani na kwamba angesaidiwa japo alisema alimsihi baba yake kuwa yeye hawezi kabisa kuyamudu masomo ya sekondari.

"Ilipofika mwezi wa saba mwaka huu baba aliniambia niende nikipime sare ya shule na nijiandae kufanya mtihani katika shule ya msingi Kawawa ilipobaki siku ya mtihani nilikuta tayari nimeandaliwa dawati langu nikaingia chumba cha mtihani ambapo niliuwa naletewa majibu " alisema Monica .

Read More »

ZITTO: NINA SHARTI MOJA TU KURUDI CHADEMA

0 comments

DAR ES SALAAM. HARUFU YA KUISHA KWA MGOGORO BAINA YA ZITTO KABWE NA CHAMA CHAKE CHA CHADEMA INANUKIA, LAKINI MBUNGE HUYO WA KIGOMA KASKAZINI ANATAKA KUWAPO NA MAZUNGUMZO KUBAINI TATIZO ILI ATAKAYEBAINIKA KUWA ALIFANYA MAKOSA AWE TAYARI KUOMBA RADHI HADHARANI.

Zitto alikiri bungeni kuwa amekuwa “akimiss” harakati zilizokuwa zikifanywa na vyama vya upinzani wakati wa Bunge Maalumu la Katiba, harakati zilizozaa Umoja wa Katiba ya Wananchi na kufurahia kuhudhuria kwa mara ya kwanza vikao vya umoja huo.
Zitto, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alipata fursa ya kuingia vikao vya Ukawa wakati wapinzani walipoungana tena kupambana dhidi ya wizi wa fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow, sakata ambalo liliwekwa bayana na kamati yake baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila kulifikisha bungeni, lakini hakudokeza lolote kuhusu Chadema.
Hata hivyo, mapema wiki hii, Zitto, ambaye Novemba mwaka jana alivuliwa nyadhifa zote kwenye chama hicho kwa tuhuma za kukihujumu, lakini akafanikiwa kulinda uanachama wake baada ya kufungua kesi mahakamani na kufanikiwa kupata amri ya kuzuia asijadiliwe.
Baada ya kuongoza PAC kuchunguza wa tuhuma za Escrow na kufanikiwa kulishawishi Bunge kufikia maazimio manane ya kuwashughulikia kisheria wahusika kwenye uchotwaji huo wa fedha, kumekuwapo na wito kutoka kwa baadhi ya wafuasi wa Chadema kutaka pande hizo mbili zimalizane.
“Kabla ya jambo lolote kufanyika, ili kukata kiu ya Watanzania wanaotaka kuona tunaondoa tofauti zetu, ni lazima kusema ukweli na kila upande kuwa tayari kuomba radhi hadharani pindi ikibainika ulifanya makosa,” alisema Zitto alipotakiwa kuzungumzia harakati hizo za kumrejesha Chadema.
“Ukweli wangu ndani ya Chadema ni nini? Lakini mimi ninaona sina kosa ndani ya Chadema. Ninachotaka mimi nielezwe ukweli bila chembe ya shaka makosa yangu mimi ni nini,” alisema na kuongeza:
“Nitakuwa tayari kuomba radhi hadharani kama ikibainika nilifanya makosa na kama ikibainika chama kilifanya makosa, nacho kiwe tayari kuomba radhi hadharani na ukweli uwe mbele katika maridhiano.
“Kama hakutakuwa na ukweli itakuwa vigumu kupata mwafaka. Mimi sina tatizo. Nirudie nilivyosema bungeni kuwa nina-miss sana (ninapenda sana kuwamo kwenye) harakati za mageuzi kipindi hiki za kuiondoa CCM madarakani.”
Katika mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kuvuliwa nyadhifa zote, Zitto alisema: “Natambua kuwa wapo ambao wangependa kutumia nafasi zao kudhoofisha mapambano ya siasa za demokrasia nchini mwetu. Napenda wanachama wa Chadema na wapenda demokrasia watambue kuwa, mimi bado ni mwanachama mwaminifu wa chama hiki.
“Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina; waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu; na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka.”
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ambaye binafsi aliguswa na mzozo huo, hakuwa tayari kuzungumzia kumaliza matatizo baina ya chama na Zitto.
“No comment (sina maoni) kwa hilo. Siwezi kuzungumzia suala hili katika media (vyombo vya habari),” alisema Mbowe
Hoja ya kutaka Zitto arejeshwe Chadema imekuwa ikisambaa katika mitandao ya kijamii na kwa baadhi ya wanasiasa baada ya kuonekana kuwa karibu na viongozi wa chama chake wakati Kamati ya PAC ilipoibua ufisadi wa Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow wiki iliyopita.
Wakati akihitimisha mjadala wa sakata la Escrow, mbali na kueleza bayana kuwa alifurahia kuhudhuria vikao vya Ukawa kwa mara ya kwanza, Zitto alikwenda mbali na kumpongeza “kwa namna ya pekee” Mbowe kwa jinsi walivyoshirikiana katika sakata hilo.
Zitto alisema hilo lilikuwa ni jambo la kitaifa ndiyo maana wabunge wote wa upinzani bila kujali vyama vyao waliungana.
Alisema mara baada ya sakata hilo kumalizika watu mbalimbali wamekuwa wakizungumzia kufanyika kwa maridhiano ili awe sehemu ya Ukawa na kwamba haoni tatizo.
“Katika hili, kipekee namshukuru kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani kwa kuniunga mkono katika sakata hili,” alisema Zitto.
Kuhusu taarifa za kujiunga kwake na chama kipya cha ACT-Tanzania alisema: “Hizo ni taarifa ambazo hazina ukweli wowote.”
Kuhusu kesi aliyofungua mahakamani dhidi ya Chadema, Zitto alisema:
“Nilifungua kesi kwa sababu ya kulinda uanachama wangu, lakini mazungumzo yakifanyika na kujua kosa langu ni nini, nitaifuta kesi hiyo na kuanza upya harakati.”
Zitto.
Kuhusu taarifa za kujiunga kwake na chama kipya cha ACT-Tanzania alisema, “Hizo ni taarifa ambazo hazina ukweli wowote.”

Kuhusu kesi aliyofungua mahakamani dhidi ya Chadema, Zitto alisema: “Nilifungua kesi kwa sababu ya kulinda uanachama wangu, lakini mazungumzo yakifanyika na kujua kosa langu ni nini, nitaifuta kesi hiyo na kuanza harakati.”
MWANANCHI

Read More »

"NAJISIKIA RAHA KUKAA UCHI NIWAPO NA MPENZI WANGU"....JOKATE ASEMA

0 comments

Modo ambaye pia anafanya muziki na ujasiriamali, Jokate Mwegelo amefunguka  kuwa, awapo chumbani na mpenzi wake huwa anasikia raha kutovaa chochote.

Akizungumzia maisha yake ya kimapenzi na mwanadada paparazi, Jokate alisema haoni aibu kusema akiwa faragha na mpenzi wake hapendelei kuvaa kitu kwani ni eneo la kujiachia.
 

“Kwa kweli nikiwa chumbani na mpenzi wangu sipendi kuvaa kitu kabisa,” alisema Jokate kwa kifupi.

Read More »

RAIA WA PAKISTAN AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 60 JELA KWA KOSA LA KUSAFIRISHA TWIGA WANNE HAI KWENDA QATAR.

0 comments
Moshi/Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Kilimanjaro, jana imemhukumu raia wa Pakistan Ahmed Kamran kifungo cha miaka 60 jela baada ya kumtia hatiani kwa makosa manne ikiwamo kusafirisha twiga wanne hai kwenda Qatar.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Simon Kobelo, ambaye pia aliamuru kutaifishwa kwa mali zote za mtuhumiwa huyo zilizopo katika ardhi ya Tanzania.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana baada ya kutolewa hukumu hiyo, Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa alisema kilichofanyika ni kutaka kuonyesha haki imetendeka, huku Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira, James Lembeli akisema kuwa kumsaka mtuhumiwa huyo ni sawa na mchezo wa kuigiza.
Hata hivyo, tayari Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) juzi limewataka Watanzania kusaidia katika kumsaka Kamrani, huku likitangaza kuanzisha operesheni iliyoipa jina la Infra Terra ikilenga kuwanasa watuhumiwa uharamia zaidi ya 139 katika nchi 36 duniani.
Mchungaji Msigwa alisema kuwa kilichofanyika ni kiini macho kwa kutaka kuonyesha kuwa haki imetendeka. Alisema haiwezekani Ahmed apatikane na kosa pekee yake wakati mchakato wa kusafirisha wanyama unaonyesha watu wengi wakiwamo viongozi walishiriki kutekeleza biashara hiyo.
“Hata kama wangemfunga miaka 200 haisaidii kitu, hapo mahakama imefanya kazi yake lakini Serikali inafanya kiini macho,” alisema Msigwa.
Msigwa ambaye pia ni Mbunge wa Iringa Mjini, alisema kitendo cha mahakama kuthibitisha kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa na vibali halali kinaonyesha kuwa kuna baadhi ya watu walishiriki kumtorosha ili wasitiwe nguvuni.
“Isingewezekana ndege iingie nchini bila wakubwa kujua ilikuja kufanya nini?” alihoji.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli alisema kumsaka mtuhumiwa Kamran Ahmed anaona huo ni mchezo kwa sababu mtuhumiwa huyo raia wa Pakistan alishatoroka awali kisha akapatikana, lakini katika hali ya kushangaza akapewa tena dhamana.
Lembeli alisema hatua ya kuruhusu dhamana ya pili kwa mtuhumiwa huyo inatia shaka kuwa kuna jambo lisilo la kawaida lililomwezesha kutoroka kwake.
“Hivi kwa nini walimpa dhamana wakati alishatoroka mara ya kwanza na huyu mwandishi Temba aliyemdhamini sijui alianzia wapi, najua hamfahamu lakini amejiingiza kwenye matatizo ya kujitakia,” alisema Lembeli.
Kuhusu ndege inayodaiwa kutumika kusafirisha wanyama hao, ambapo mahakama imethibitisha kuwa ilikuwa na vibali vyote halali vya kuingia nchini kwa safari ya kidiplomasia, Lembeli alisema Wizara ya Mambo ya Nje ieleze kwa kina jambo hilo lilitokeaje.
“Mimi katika hilo sitaki kuzungumza sana, ila nafikiri kuna haja ya kujiridhisha kuwa kibali hicho cha kidiplomasia ni cha aina gani, kilitolewaje, kisha majibu tutakayopata ndipo tutajua nini kilitokea,” alisema Lembeli.
Alipotafutwa kwa njia ya simu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na naibu wake, Mahmoud Mgimwa, simu zao ziliita bila kupokelewa.
Hukumu ya kesi hiyo ilitolewa bila mtuhumiwa wa kwanza (Kamran) kuwapo mahakamani baada ya kutoroka tangu Februari mwaka huu wakati kesi yake ikiwa katika hatua za mwanzo za usikilizwaji.
Katika hukumu hiyo, hakimu Kobelo aliwaona washtakiwa wengine wanne, Hawa Mang’unyuka, Martin Kimath na Michael Mrutu kuwa hawana kesi ya kujibu na kuwaachia huru.
Hakimu Kobelo alisema hakuna ubishi kuwa raia huyo wa Pakistan (Kamran), ndiye aliyekuwa wakala katika biashara hiyo na ambaye ndiye aliyewasafirisha wanyama hao kwa kutumia ndege kubwa ya Jeshi la Qatar. Kobelo alisema ndege hiyo ilikuwa na vibali vyote halali vya kuingia nchini kwa safari ya kidiplomasia kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA).
Hakimu Kobelo alisisitiza kuwa ndege iliyobeba wanyama hao ilikuwa na hadhi ya kidiplomasia na ilifuata taratibu zote na kuruhusiwa na mamlaka za nchi ikiwamo Wizara ya Mambo ya Nje.Uchambuzi wa ushahidi huo unaonyesha raia huyo wa Pakistan, aliruhusiwa na mamlaka za Tanzania kukamata wanyama kwa kutumia leseni za kampuni mbili zinazomilikiwa na Hawa.
Hata hivyo, mshtakiwa huyo hakuwa na kibali cha kusafirisha wanyama hao kwenda nje ya nchi na kwa kuwa alitoroka, mahakama haikuweza kupata uthibitisho wake kama alikuwa na kibali.
Kutokana na uchambuzi huo, mahakama imemtia hatiani raia huyo wa Pakistani kwa makosa manne ambapo kila kosa amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.

Read More »