Kati ya watu hao 162, abiria walikuwa 155, marubani 2 na wafanyakazi wa ndege hiyo 5. Watu 157 ni raia wa Indonesia, 3 raia wa Korea Kusini, 1 kutoka Malaysia na 1 raia wa Singapore.
Imeelezwa kuwa kabla ya ndege hiyo kupoteza mawasiliano, rubani aliomba kubadili uelekeo wa kawaida kutokana na hali mbaya ya hewa.
Ndege hiyo ilifanyiwa matengenezo kwa mara ya mwisho Novemba 16, 2014 kama ilivyokuwa imepangwa.
Rubani wa ndege hiyo ana uzoefu wa saa 6,100 angani huku msaidizi wake akiwa na uzoefu wa saa 2,275.
Miongoni mwa abiria 155 waliokuwa kwenye ndege hiyo, 138 ni watu wazima, 16 watoto na 1 mama mjamzito.
QZ8501 imetoka Indonesia saa 11: 27 alfajiri na ilitarajiwa kuwasili Singapore saa 2:37 asubuhi.
Read More »
Robin van Persie wa Manchester United akijaribu kufunga bao lililookolewa na kipa Hugo Lloris wa Spurs.
Patashika wakati wa mtanange wa leo.
Mchezaji wa Tottenham, Nacer Chadi (kulia) akiruka juu kuwania mpira na Antonio Valencia wa Manchester United.
TIMU za Tottenham Hotspur na Manchester United zimeshindwa kutambiana
baada ya kutoka suluhu katika mechi yao ya Ligi Kuu England
iliyomalizika kwenye Uwanja wa White Hart Lane hivi punde.VIKOSI VYA LEO
Tottenham: Lloris, Chiriches, Fazio, Vertonghen, Davies, Mason, Stambouli; Chadli, Eriksen, Townsend, Kane
Waliokuwa benchi: Vorm, Dier, Walker, Lamela, Dembele, Paulinho, Soldado
Manchester United: De Gea, Jones, McNair, Evans, Valencia, Carrick, Rooney, Mata, Young, Van Persie, Falcao
Waliokuwa benchi: Lindegaard, Rafael, Smalling, Shaw, Fletcher, A.Pereira, Wilson
Read More »
BREAKING NEWS: MWISHONI MWA MWAKA 2014: NDEGE YA AIRASIA QZ8501 YAPOTEA IKIWA NA WATU 162 INGIA HAPA KWA HABARI KAMILI
11:41 0 commentsNDEGE ya AirAsia, QZ8501 iliyokuwa na watu 162 ikitokea Indonesia kwenda Singapore imepoteza mawasiliano leo asubuhi.
Kati ya watu hao 162, abiria walikuwa 155, marubani 2 na wafanyakazi wa ndege hiyo 5. Watu 157 ni raia wa Indonesia, 3 raia wa Korea Kusini, 1 kutoka Malaysia na 1 raia wa Singapore.
Imeelezwa kuwa kabla ya ndege hiyo kupoteza mawasiliano, rubani aliomba kubadili uelekeo wa kawaida kutokana na hali mbaya ya hewa.
Ndege hiyo ilifanyiwa matengenezo kwa mara ya mwisho Novemba 16, 2014 kama ilivyokuwa imepangwa.
Rubani wa ndege hiyo ana uzoefu wa saa 6,100 angani huku msaidizi wake akiwa na uzoefu wa saa 2,275.
Miongoni mwa abiria 155 waliokuwa kwenye ndege hiyo, 138 ni watu wazima, 16 watoto na 1 mama mjamzito.
QZ8501 imetoka Indonesia saa 11: 27 alfajiri na ilitarajiwa kuwasili Singapore saa 2:37 asubuhi.
Read More »
Vanessa ameshinda tuzo ya Best Female Artist in East Africa [Msanii bora wa kike Afrika Mashariki ] huku Diamond akishinda Tuzo Ya Best Male Artist in East Africa [ Msanii bora wa kiume Africa Mashariki] . Tuzo ya Diamond ilipokelewa na Peter Msechu ambaye pia alikuwa kwenye kuwania tuzo hizo.
Read More »
00:36
0
comments
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewatimua wanachama wake 42 wakiwemo wagombea walioshindwa kupita kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa hivi karibuni.
Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho, kutimuliwa kwa wanachama wake hao ni hatua ya chama hicho kujisafisha kutokana na kile kinachodaiwa kwamba baadhi ya wagombea hao wanatuhumiwa kufanya hujuma wakati wa mchakato wa uchaguzi serikali za mitaa, vitongoji na vijiji uliofanyika Desemba 14, mwaka huu.
Akitangaza uamuzi huo mjini humo, Katibu wa Chadema Jimbo la Korogwe Mjini, Ezekiel Mbwilo alisema wahusika waliotimuliwa uanachama wanatuhumiwa kwa kukubali vitisho na wengine kurubuniwa kwa fedha za wapinzani wao, hatua iliyowalazimu kwenda kuondoa majina yao katika hatua za mwisho kuelekea kwenye kinyang’anyiro hicho.
“Tuligundua kuwa baadhi ya wahusiska walijihusisha na hujuma mbalimbali dhidi ya chama chetu, ikiwamo kukubali kupewa fedha na wapinzani wao ili wajiondoe. Tangu awali, tulishakubalina kwamba ikibainika watu waliofanya hujuma tutawatimua kundini na hapa ndipo tunahitimisha lile tulilokubaliana,” alisema.
Mbwilo alitaja maeneo wanayotoka wanachama hao waliotimuliwa na idadi yao kwenye mabano ni Kwamsisiwatu (6), Mahenge (10), Kitifu (25) pamoja na mmoja kutoka Manundukati ambaye alidai kwamba mhusika huyo aliamua kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi ukiwa katika hatua za mwisho baada ya kurubuniwa na wapinzani wa chama hicho.
Akizungumzia vitisho alivyodai vilitolewa baadhi ya wanachama wa vyama vingine dhidi ya wagombea wa Chadema, Mbwilo alisema tayari amewasilisha taarifa hizo kwenye vyombo vya usalama na katika jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi.
Read More »
Mwanadada asiyeishiwa matukio Bongo, Baby Madaha.
MWANADADA
asiyeishiwa matukio Bongo, Baby Madaha ameibuka na kutoa kali ya mwaka
kwamba anapenda mapenzi kuliko kitu kingine chochote duniani.
Akichezesha taya na paparazi wetu, Baby Madaha alisema ‘hobi’ yake ni
mapenzi japokuwa anapenda muziki lakini haifikii jinsi anavyoyapenda
mapenzi kwani yanampumzisha akili yake na kumfurahisha moyo wake pia.
“Ukweli napenda mapenzi kuliko kitu chochote ila sipendi kuzinguliwa
na wanaume, ninapenda muziki, filamu lakini haviwezi kufikia mapenzi
kwani ndiyo kila kitu kwangu na yananipa starehe kuliko kitu chochote
hapa duniani,” alisema Baby Madaha.
Read More »
STAA wa filamu Bongo, Wastara Juma, ametamka hadharani kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na msanii yeyote ndani ya Kundi la Bongo Movie.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Wastara alisema kuna maneno mengi yanasemwa kuwa ana uhusiano na mtu ndani ya kundi hilo kitu ambacho si sahihi, atamuanika mrithi wa marehemu Sajuki siku si nyingi.
“Unajua muda utafika tu lakini kwa hivi sasa sina bwana wala sihitaji mtu yeyote ndani ya Kundi la Bongo Movie na mtu ambaye ataishi na mimi muda ukifika nitawatambulisha na kila mmoja atamjua na siyo mtu kunitabiria au kubuni nitamuweka wazi muda si mrefu,” alisema Wastara.
Read More »
LAAANA!!! Watu wakutwa wakifanya mapenzi kwenye gari maeneo ya fukwe za bahari INGIA HAPA KUONA PICHA NA HABARI KAMILI
15:59 0 comments
kutokana na maadili picha ni mbaya sana ndo maana imetuia vigumu kuziweka picha zote kuhusiana na ili tukio la kufunga mwaka ambapo watu wamekutwa wakifanya mapenzi kwenye gari katika fukwe za bahari .... TUNALINDA MAADILI JAMANI
Read More »
Balaaa!!! La Sikukuu: Changudoa Atopeza Fahamu Baada Ya Kuzidisha Wanaume Ingia Hapa Kuona Picha Zote Za Tukio Zima
18:37 0 comments
MSICHANA mmoja
aliyetambulika kwa jina moja la Jenipher, anayedaiwa kujiuza katika
maeneo ya Shivaz na Kaloleni jijini hapa, amekutwa akiwa amepoteza
fahamu kando ya barabara, katika harakati za kujipatia chochote kipindi
hiki cha sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.
Akiwa
pembeni ya barabara, Jenipher anayeelezwa kuwa maarufu mjini hapa,
anadaiwa kuwa siku hiyo alizidisha idadi ya wanaume aliotoka nao, kwa
ajili ya kujipatia kipato cha kutosha ili aweze kuburudika vizuri wakati
wa sikukuu ya Krismasi.
Baadhi
ya mashuhuda wanaomfahamu msichana huyo walisema kwamba katika kipindi
cha wiki nzima iliyopita, alikuwa akisaka wanaume kwa bidii na kwamba
alikuwa tayari kwa ajili ya kutoa huduma hiyo mahali popote.
“Unajua
hapa kila mtu na mambo yake, huyu Jenipher siku zote tupo naye ila wao
huwa hawaendi kulipia gesti, ila wanafanya ngono popote hata mtaroni,
kwenye ukuta ilimradi huyo mwanaume yupo tayari, ila usiku alizidiwa na
wanaume na hakuwa amekula,’’ alisema mmoja wa dada poa aliyekataa kutaja
jina lake.
Mmoja
wa wamiliki wa baa iliyo maeneo hayo, aliyeomba hifadhi ya jina lake,
alisema wasichana wengi wanaojihusisha na biashara hiyo wamekuwa na
tamaa kiasi cha kushindwa kujali afya zao, kwani baadhi yao huacha hata
kula chakula, badala yake, hunywa pombe aina ya viroba.
Hadi paparazi inaondoka eneo hilo, bado binti huyo alikuwa yupo eneo hilo akiwa hajitambui.
Read More »
MTOTO WA ANNA TIBAIJUKA AWATUKANA WATANZANIA HUKU AKIMTETEA MAMA YAKE KWA KUCHOTA PESA ZA ESCROW
18:24 0 comments
Kagem Tibaijuka.
WAKATI Rais
Jakaya Kikwete akiwa amemuwajibisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka kufuatia kumegewa mgawo wa fedha za
Tegeta Escrow, binti anayedaiwa kuwa mwanaye, amejikuta akipata wakati
mgumu baada ya kumtetea mama yake kupitia mitandao ya kijamii.

Katika
Mtandao wa Twitter, binti huyo aliyejitambulisha kwa jina la Kagem
Tibaijuka, alimtetea mama yake akisema fedha zilizowekwa kwenye akaunti
yake zilikuwa ni safi na halali na kwamba ziliwekwa kwa nia njema ya
kuwasaidia kielimu watoto wa kike
“My
mum did nothing wrong except wanting to help young girls get an
education. A school built with my late father. Accepted a donation,”
(Mama yangu hakufanya kosa lolote isipokuwa alitaka kuwasaidia wasichana
kupata elimu. Shule ilijengwa na marehemu baba yangu. Mchango
ukakubaliwa)yalikuwa ni moja ya maneno yake katika mtandao huo wa
Twitter.

Aidha,
aliwashambulia wanawake walioonekana kushangilia wakati Rais Kikwete
alipotangaza kumuwajibisha mama yake, akiwaambia kuwa anawashangaa
kushangilia anguko la mwanamke mwenzao na kwamba hata wao iko siku
yatawakuta ya kuwakuta.
Lakini
katika mitandao mingine ya kijamii, ikiwemo Facebook na Jamii Forum
inayotembelewa na watanzania wengi, walimshambulia binti huyo kwa
kumwelezea kama mtu aliyelewa fedha na kwamba mama yake alistahili
kuondolewa kwenye nafasi yake, ikiwa ni pamoja na kushtakiwa.
Wachangiaji
walioonekana kuchukizwa na utetezi wa binti huyo kwa mama yake,
walisema licha ya Profesa Tibaijuka kuondolewa, pia watu wote
waliotajwa, wakiwemo Waziri Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu, Eliakim
Maswi nao walistahili kuondolewa katika nafasi zao.
Mtandao
huu ulimtafuta mama Tibaijuka kupitia simu zake mbili za mkononi, ili
kuzungumzia maoni yake baada ya kukutwa na ajali hiyo ya kisiasa pamoja
na kumuuliza kama Kagem ni bintiye, lakini moja iliyopatikana, iliita
kwa muda mrefu bila kupokelewa. Hata hivyo baadaye simu hiyo ilipopigwa,
ilionekana imezimwa.
Aidha
Kagem mwenyewe, ambaye ofisi zake zinadaiwa kuwa eneo la Kijitonyama
jijini Dar es Salaam, naye hakupokea simu yake ya mkononi aliyopigiwa na
hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, hakujibu.
Jumatatu
iliyopita, Rais Kikwete alizungumzia suala hilo la fedha zilizodaiwa na
Bunge kuwa ni za umma, kuchukuliwa isivyo halali katika akaunti
iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania. Wakati Mwanasheria Mkuu, Jaji
Frederick Werema alijiuzulu mwenyewe na mama Tibaijuka kuwajibishwa,
viongozi wengine waliodaiwa kuhusika na fedha hizo wanaendelea
kuchunguzwa na hatua stahiki dhidi yao zitachukuliwa.
Read More »
Mzee Yusuf akiwadatisha mashabiki kwa ngoma zake kali.
Mzee Yusuf akicharaza gitaa.
Idris Sultan akimtambulisha kwa mashabiki wa Dar Live mshikaji wake aliyekuwa naye kwenye mjengo wa BBA, Samantha wa Afrika Kusini.
Mzee Yusuf akikandamiza kinanda wakati wa shoo yake Dar Live.
Mzee Yusuf na vijana wake wakifanya yao stejini.
Mzee Yusuf akionyesha ujuzi wa kucharaza gitaa chini kwa chini.
MFALME wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' usiku wa Krismasi amewadhihirishia mashabiki wake kuwa ni mfalme baada ya kufanya makamuzi ya hatari katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar kwenye Tamasha la Wafalmelililodhaminiwa na VODACOM pamoja na COCACOLA.
Staa huyo aligonga ngoma zake zote na kuzikonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliofurika katika uwanja huo wa burudani.
Mbali na Diamond, Mfalme wa Taarab nchini, Mzee Yusuf naye alifanya shoo kali na kuwapagawisha mashabiki waliofika kwa wingi kuliko siku zote katika ukumbi huo wa kisasa wa Dar Live.
Read More »
Subscribe to:
Posts (Atom)
