video: mwanamke adakwa akitaka kuchepuka na mume wa mtu...wamnyoa nywele kisha kukalia chupa

'
Nimeona hii video nikasikitika sana.... Jamani jamani jamani hii haikubaliki hata kidogo ni kinyume na Haki za Binadam... Yesu Ruwa... yaani umkalishe mwanamke mwenzako kwenye chupa???? na nywele zake umenyoa juu???

Najua uchungu wa Mume na ninajua mchepuko unavyomwaga sumu ndani ya Familia, najua sana na hizo kesi ni nyingi mnooo kwa sasa... nyingi ni wanaume wametelekeza nyumba zao na kuishia kwa michepuko.... unakuta nyumba kama hiyo imegeuka siria kwa vita vya kila aina....PAMOJA NA HAYA YOTE BADO NASEMA ADHABU KAMA HII HAIKUBALIKI JAMENI....Nchi yetu inaongozwa kwa Taratibu na sheria, tusichukue sheria mkononi kina mama wenzangu jamani... aiseeee....
ninachoweza kusema ni kwamba sisapoti kilichofanyika kwa Mume kumsaliti mke na pia siungi mkono alichofanyiwa huyu dada anaetuhumiwa kukwapua mume....

Ninajaribu kuangalia sisi kama Wanawake, tunachangia vipi kuepusha Ukatili na Udhalilishaji wa sisi kwa sisi????

Naomba kupata mtazamo wako juu ya sakata hili, na zaidi ya hapo tutazame jambo hili kwa jicho la tatu...usikurupuke kwa kweli maana hii ni hatari sana...
Ebu vaa viatu vyao kidunchu... naomba ushauri ungekuwa ni wewe 'unaetoa adhabu' ungefanyaje au ungekuwa ni wewe 'unaepewa adhabu' ungefanyaje kutoka ndani ya moyo wako, ikiwa mume au mke amekusaliti???? na ukamjua anaekuibia

0 comments: