Man U yamsajili kipa wa Barcelona
Victor Valdes akisaini kuichezea Man U.
MANCHESTER, England
KLABU ya Manchester United imethibitisha kumsajili kipa wa zamani wa Barcelona, Victor Valdes kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
Valdes
mwenye umri wa miaka 32, alikuwa akifanya mazoezi na klabu hiyo tangu
Oktoba, mwaka jana baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu
akisumbuliwa na maumivu ya goti.
Valdes
ameeleza kuwa amefurahishwa na usajili huo na yupo tayari kufanya kazi
na kipa chaguo la kwanza la timu hiyo, David de Gea ambaye ni raia
mwenzake wa Hispania.
0 comments: