MATONYA: NAKUTAFUTA POPOTE ULIPO JAYDEE KWA KUNIDHARIRISHA KWA KUSAMBAZA PICHA NIKIWA SIJITAMBUI
STAA aliyewahi
kukamata vilivyo kwenye anga ya muziki wa Bongo Fleva, Shabani
Ramadhani ‘Matonya’ ameibuka na kumvaa mwanadada Judith Wambura ‘Jide au
Lady Jaydee’ akidai amemdhalilisha kwa mashabiki wake.
Staa aliyewahi kukamata vilivyo kwenye anga ya muziki wa Bongo Fleva, Shabani Ramadhani ‘Matonya’
Akizungumza
na paparazi wetu, Matonya alisema anamtafuta Jide popote alipo ili
amuulize kinaga ubaga kwa nini aliamua kuposti picha kwenye mitandao
yake ya kijamii ikimuonesha akiwa hajitambui pasipo kumtaarifu.
Mwanadada Judith Wambura ‘Jide au Lady Jaydee’.
“Nimeumizwa
sana na Jide kwa kitendo chake cha kuamua kunidhalilisha kwa kiasi
hicho tena akijua mimi ni mwanamuziki mwenzake na kama kuna kitu aliona
simfurahishi kwenye mwenendo wa maisha yangu basi alikuwa wazi kuniita
na kunikalisha chini na siyo kama uamuzi alioutumia wa kunianika kwenye
mitandao,” alisema Matonya.
Matonya
alifafanua kuwa picha hiyo alipigwa katika video yake mpya lakini Jide
akaichukua na kuiweka mitandaoni pasipo kumuuliza.
Matonya akiwa mtungi.
“Ile
picha aliyoitumia kunidhalilisha ilikuwa ni ya video yangu ya wimbo
mpya unaoitwa Homa ya Jiji ambayo itatoka hivi karibuni, sasa yeye
ameweka mitandaoni na kusababisha watu wanidharau kwa kuona nimelewa
chakari, asiponiomba radhi nitahakikisha namfikisha mahakamani,” alisema
Matonya.
Kupitia
ukurasa wake wa Facebook, Jide aliiposti picha ya Matonya akiwa amelala
na kusindikiza na ujumbe ulioonesha kama hamjui msanii huyo hali
iliyosababisha mashabiki wengi kumsema vibaya Matonya.
0 comments: