Saluni ya Ngono Yafumuliwa jijini Dar......Wahudumu wake ni makahaba, mteja hulipa Elfu 60 kwa tendo moja
Wakati suala la ajira likiwa bado ni kitendawili kikubwa kwa serikali, Jiji la Dar hivi sasa linatisha, baada ya watu kubuni mtindo mpya wa kujipatia fedha kwa kujihusisha na biashara haramu ya ngono katika maeneo yanayotambulika kufanya shughuli nyingine halali.
Uchunguzi wa paparazi huru unaonyesha kuwa zipo saluni nyingi
jijini Dar zinazojishughulisha na biashara ya massage (kuchua) lakini
ndani yake wahudumu wanajiuza hadi miili ambapo wateja wakubwa ni waume
za watu na vigogo serikalini.
Uchunguzi
huo unathibitishwa na tukio moja la hivi karibuni lililonaswa na
polisi katika saluni moja ya kuchua iliyopo eneo la
Kinondoni-Morocco, Dar. Polisi hao walikuwa katika msako baada ya
kudokezwa maovu yanafanyika ndani ya saluni hiyo na paparazi wetu.
Ndani ya saluni hiyo, Polisi walishuhudia mhudumu wa mapokezi ambaye baada ya kuonyeshwa vitambulisho
vya askari wa Jeshi la Polisi, alinywea na kuwaruhusu kupekua chumba
kimoja baada ya kingine, ili kujionea kama kweli nyumba hiyo ilikuwa
ikijihusisha na masuala ya saluni ya uchuaji pekee na siyo vinginevyo.
Katika
chumba cha kwanza, askari hao walimkuta mwanaume mmoja akiwa uchi wa
nyama, lakini mwanamke aliyekuwa naye akiwa amevaa nguo zake, kitu
kilichoashiria kuwa tayari ‘mchezo ulishafanyika’.
Katika hali isiyotarajiwa, baada ya kupitia vyumba vingine vinne na kuvikuta tupu, kilichofuata, polisi walishuhudia mwanamke mwenye asili ya Kisomali akiwa uchi na mwanaume wake, dalili zote zikionyesha kuwa walikuwa wakijiandaa kufanya uzinzi.
Katika hali isiyotarajiwa, baada ya kupitia vyumba vingine vinne na kuvikuta tupu, kilichofuata, polisi walishuhudia mwanamke mwenye asili ya Kisomali akiwa uchi na mwanaume wake, dalili zote zikionyesha kuwa walikuwa wakijiandaa kufanya uzinzi.
Baada ya kuwakuta katika hali hiyo, kiongozi
wa askari hao, aliwauliza kama hiyo ndiyo biashara ya
masaji waliyopata kibali cha kuifanya, lakini wakabakia kujiumauma
pasipo kutoa jibu la kueleweka.
Binti huyo wa Kisomali, ghafla
aliibuka na kuanza kuomba msamaha kwa kitendo hicho, akidai maisha
magumu wanayoishi, ndiyo yanayosababisha waifanye biashara hiyo.
Lakini la kushangaza zaidi, ni pale mwanamke huyo alipodai kuwa
nyumbani alikotoka, ambako ameolewa, pia alimuacha mwanaye mwenye umri
wa miezi minne.
Mwanaume aliyekutwa naye, alipoulizwa biashara hiyo
inafanyika kwa bei gani, alisema makubaliano yake na mwanamke huyo, ni
kutoa kiasi cha shilingi elfu sitini kwa tendo moja!
0 comments: