HII SASA NI HATARI BUSU LA MWANAUME KWA MWANAUME KWENYE TELEVISION YA TAIFA LAZUA KIZAA ZAA
Watu wa jinsia moja wakipigana busu
Waandaaji
wa kipindi maarufu cha tamthilia nchini Angola wameomba radhi baada ya
sehemu ya Tamthilia hiyo iliyoonyesha wapenzi wa jinsia moja wakibusu
kuamsha ghadhabu miongoni mwa watazamaji.
Televisheni ya Taifa imesema imesitisha Matangazo ya Tamthilia ya Jikulumessu kwa sababu za kiufundi.
Watazamaji
wengi wanaona kuwa kipindi hicho kilivuka mipaka kwa kuonyesha wanaume
wakibusu, ingawa haijatangazwa kuwa mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja
nchini Angola ni haramu.
Kipindi hicho kilikuwa kinatengenezwa na Kampuni moja inayomilikiwa na Mtoto wa Rais.
Jose
Eduardo Paulino dos Santos,Msanii maarufu nchini humo amekuwa
akishutumiwa kunadi vitendo vya mahusiano ya jinsia moja miongoni mwa
Jamii ambayo imekuwa katika misingi ya kuheshimu maadili na dini.
Kampuni yake,imesema inapitia tena vipindi vyake na imeomba radhi kwa kuwakera Watazamaji.
Kipindi
cha Jikulumessu huangazia maswala yanayogusa jamii kama vile ndoa za
mitara, mahusiano ya jinsia moja, biashara ya ngono kwa ajili ya kuzua
mjadala kwenye jamii.
0 comments: