'Sangoma' akutwa akimiliki SMG, risasi nane
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha
Mganga
wa kienyeji, Zacharia Ngobeko (35), amekamatwa na polisi mkoani hapa
baada ya kukutwa akimiliki SMG na risasi nane kinyume cha sheria.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha, alisema tukio hilo
lilitokea juzi saa 1 jioni, baada askari polisi kufanya msako nyumbani
kwake na kukamata silaha hiyo ikiwa na risasi zilizokuwamo kwenye
magazine.
Kamugisha
alisema baada ya kumhoji, alidai silaha hiyo ilitumika kufanya mauaji
mbalimbali yakiwamo ya kumuua, Mary Kashidye, Februari 8, mwaka huu, kwa
kumpiga risasi kutokana na ugomvi wa kiwanja kati yake na Jumanne
Maige.
Aidha,
alisema mauaji hayo yalifanyika baada ya kukodiwa vijana wawili, Andrew
Buteye (38) na Daudi Luchemela (40), kutekeleza mauaji hayo, kisha
kurejesha silaha hiyo kwa mganga huyo.
Kamanda
Kamugisha alisema silaha hiyo kupitia vijana hao ilitumika katika tukio
la unyang’anyi wilayani Kahama baada ya kumpora Manyangu Mboje, Sh.
Milioni 1.5, dukani kwake Februari 13, mwaka huu.
Hata
hivyo, alisema baada ya kuwahoji watuhumiwa wote walikiri kuhusika na
matukio hayo ya mauaji na unyang’anyi kwa kutumia SMG hiyo na kisha
kuihifadhi kwa mganga huyo huku wakikiri kufanya matukio mengine mkoani
Mbeya mwaka 2010 na 2012.
Alisema
watuhumiwa hao, pia walikiri kufanya uhalifu wilayani Sengerema mkoa wa
Mwanza 2014, kwa kupora Sh. milioni 39. Watuhumiwa wote wanatarajiwa
kufikishwa mahakamani wiki ijayo kujibu mashitaka yanayowakabili.
0 comments: