Wauza madini watatu wauawa kinyama


ENEO la Mjohororoni wilayani Hai, mkoa wa Kilimanjaro jirani na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kando ya barabara ya Moshi/Arusha, linazidi kuwa na rekodi mbaya ya matukio ya mauaji.

Hapa ndipo aliuawa mfanyabiashara bilionea wa madini aina ya Tanzanite Erasto Msuya (43) kwa kupigwa risasi zaidi ya 10 kifuani mwaka juzi- na sasa miili mitatu ya watu wanaodhaniwa kuwa wachimbaji wa madini hayo mkoani Arusha, imeokotwa ikiwa na michubuko midogo na wengine damu ikitoka Puani.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, amethibitisha tukio lakini akaahidi kutoa taarifa kamili baadaye.
Paparazi limeelezwa kuwa tukio hilo limetokea leo asubuhi  majira ya 2:000 katika eneo hilo maarufu kama kwa Wasomali.
Vijana hao wanaodaiwa kuwa na umri kati ya miaka 28 na 32 walikutwa katika eneo hilo na msamaria mwema ambaye baadaye alitoa  taarifa kituo cha Polisi Bomang’ombe.
Mtoa taarifa wetu, amesema kuwa miili hiyo baada ya kuondolewa eneo hilo na polisi, ilipelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mawenzi kwa ajili ya kuhifadhiwa lakini ilishindikana kutokana na chumba cha kuhifadhia maiti kujaa.

0 comments: