VIGOGO WIZARA YA UJENZI WAMKIMBIA MAGUFULI!


 Waziri ya Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli.
Baadhi ya vigogo katika Wizara ya Ujenzi inayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli (pichani), wameikimbia wizara hiyo na kwenda sehemu nyingine kwa kile walichodai ni uongozi wa kibabe na unyanyasaji katika idara ya usalama barabarani na mazingira.
Uchunguzi uliofanywa na paparazi wizarani hapo umebaini kuwa katika idara hiyo inayoongozwa na Julius Chambo kama Kaimu Mkurugenzi imekimbiwa na vigogo watatu, Juma Kijavara, Omari Kinyange na Samson Nkundineza ambao wameondoka wizarani hapo ndani ya mwezi mmoja, Desemba mwaka jana.
Vyanzo vyetu vya habari ndani ya wizara hiyo vinadai kwamba tangu Chambo ahamishiwe katika idara hiyo akitokea kituo cha mizani Himo mkoani Kilimanjaro, utendaji wa kazi umekuwa ukisuasua kwa kile kinachodaiwa kuwa ni uongozi wa kidikteta pia wameona kama amewekwa hapo kiupendeleo kwa vile mambo ya utawala hajui.
Katika idara hiyo inayoongozwa na Chambo ilikuwa na wahandisi wanne lakini baada ya kuondoka kwa hao watatu alibakia mmoja na inasemekana wameletwa wengine kufidia walioondoka.
Kuhama kwa vigogo hao kumewatia hofu wafanyakazi waliobaki na inasemekana kuwa baadhi yao wanataka kuondoka.
Aidha baadhi ya wafanyakazi wamelalamikia kipindi kirefu alichopewa kukaimu nafasi hiyo.
“Huwezi kukaimu ofisi kwa muda mrefu namna hiyo  hapa kuna tatizo,” alisema mhandisi mmoja kwa sharti la kutoandikwa jina lake mtandaoni.
Aliongeza kuwa kama wizara haitafanya mabadiliko stahiki kuna wahandisi watatu wataondoka hivyo wizara kupoteza wataalamu wazoefu kitu ambacho kitaleta shida kubwa wizarani hapo.
paparazi alipomtafuta Chambo ofisini kwake alikiri kuondoka kwa vigogo hao na akadai kuwa ni mmoja tu ndiye aliyemuaga lakini wengine hawakufanya hivyo.
“Mimi naamini wameondoka kwenda kutafuta maslahi zaidi, kuhusu madai mengine mimi siwezi kuzungumzia masuala ya wizara, nendeni kwa katibu mkuu,” alisema Chambo. Naye katibu mkuu wa wizara hiyo, Musa Lyombe alipohojiwa alisema wafanyakazi hao wameondoka Desemba mwaka jana lakini hata yeye ameshangazwa na kuondoka kwao.
“Nafikiri kuna jambo na kuna umuhimu wa kulichunguza suala hili kwa karibu, wao walikuja kwangu nikijua wanafuata maslahi, kwa nini itokee katika idara hiyo moja?” alihoji.

0 comments:

SHAMSA: NALALA NA MUME WANGU LOKESHENI


Staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford.
STAA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford amesema kuwa mara kadhaa anapokuwa lokesheni akishuti filamu mume wake, Dickson Matoke huwa anamfuata na kulala naye hadi asubuhi huku akiamini kufanya hivyo kunachangia kutochepuka.
Akizungumza na paparazi, Shamsa alisema kuwa kitendo cha mumewe kumfuata haina maana kwamba wanavunja sheria zao bali hilo analifanya kwa kuwa yeye ni mke wa mtu na huwa anapewa chumba chake maalum.
“Mara nyingi ninapokuwa lokesheni kama si mbali na nyumbani basi naenda kumuona mume wangu na mtoto lakini kama ni mbali kidogo mume wangu huwa anakuja na kulala na mimi chumbani kwangu, asubuhi anaondoka naendelea na kazi yangu,” alisema Shamsa.

0 comments:

AJALI YA GARI YAUA WATATU KOROGWE

 



AJALI hii mbaya ilitokea juzi (Jumapili) katika Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga ambapo watu watatu wanadaiwa kupoteza maisha.
Dereva wa gari hili lililopata ajali amelazwa katika Hospitali ya KCMC, Moshi akiendelea na matibabu.

0 comments:

Picha na Orodha ya washindi wa tuzo za FIFA Ballon d’Or 2014.


cr 2

Tuzo za Ballon d’Or zimefanyika 12 Jan 2014 ambapo wachezaji bora wa mwaka wamepokea tuzo kutoka shirikisho la soka ulimwenguni FIFA Kupitia Fifa Ballon d’Or.
Tuzo ya mchezaji bora duniani imeshindwa na Cristiano Ronaldo, alikuwa akiwani na Lionel Messi na mlinda mlango Manuel Neur.
Cristiano Ronaldo ameshinda kwa asilimia 37.66 ya kura zote akimshinda Lionel Messi  mwenye asilimia 15.76% na Manuel Neuer mwenye asilimia 15.72%.
Tuzo ya goli bora ameshinda James Rodriguez .

Tuzo ya mwanasoka wa kike ameshinda Nedine Kassler.
Tuzo ya mlinda mlango bora ameshinda Manuel Neur .
Tuzo ya kocha bora ameshinda mjerumani Joachim Law  .
Kikosi bora cha FIFA kimetajwa kuwa na hawa wachezaji . Neuer; Lahm, Ramos, David Luiz, Thiago Silva; Di Maria, Iniesta, Kroos; Messi, Ronaldo, Roben
cr 1
ronald

0 comments: