JOKATE: DIAMOND HANA AKILI TIMAMU SOMA HAPA KWA HABARI KAMILI

Staa wa urembo, muziki, filamu na ujasiriamali Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ au ‘Jojo’ amemrushia maneno makali aliyewahi kuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa hana akili timamu kufuatia maneno aliyotoa kuwa enzi za uhusiano wao, eti mwanadada huyo alikuwa akichenga kumzalia mtoto.
Staa wa urembo, muziki, filamu na ujasiriamali Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ au ‘Jojo’.
MAHOJIANO
Katika mahojiano maalum ya hivi karibuni kupitia Kipindi cha Mtu Kati cha Runinga ya GlobalTV Online chenye makao yake makuu ndani ya Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga-Mwenge, Dar, Diamond alitoa madai kuwa, amekuwa akihaha kupata mtoto.
Alisema kwamba, katika harakati zake hizo, warembo ambao alishatoka nao kimapenzi akiwemo Jokate walikuwa wakimchezea mchezo mchafu ili wasimzalie kwa kuwa alikuwa akiwaambia anahitaji mtoto kwa udi na uvumba.
MZOZO MKUBWA
Hata hivyo, madai hayo ya Diamond yalizua mzozo mkubwa kwenye mitandao ya kijamii huku warembo hao wakipigwa za uso hivyo kutafuta namna ya kujitetea.“Hao akina…(wanatajwa warembo wa Diamond) watakuwa wana matatizo ya uzazi siyo bure.
“Ndiyo maana Dangote (Diamond) ameona bora aende kwa Zari (msanii wa Uganda, Zarinah Hassan) ambaye tayari ana mwanga wa kuzaa (ana watoto watatu),” ilisomeka sehemu ya maoni juu ya madai hayo ya Diamond kwenye Mtandao wa Instagram.
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ akiwa na Diamond.
SIKIA MADAI YA DIAMOND
Diamond alifunguka: “Jokate na Wema (Sepetu) nilitamani sana wanizalie lakini walikuwa wakichengachenga, mambo mengine ujue si ya kuzungumza lakini inauma.”
JOKATE AJIBU MAPIGO
Kufuatia tuhuma hizo nzito huku kukiwa na madai pia, kwamba Jokate aliwahi kupigwa mimba ‘akaipanchi’, mwanadada huyo alipotafutwa na mwandishi wetu kujibu ‘shitaka’ linalomkabili alianza kwa kumshangaa staa huyo wa Ngoma ya Ntampata Wapi inayokimbiza kwa sasa.
Jokate alisema anamshangaa Diamond kuyazungumza maneno hayo hadharani na inaonesha asivyokuwa na akili timamu au ambayo haijakomaa.
JOJO ASHUKA NA MISTARI
“Diamond atuache, kila siku anatuzungumzia, hana akili timamu.
“Inadhihirisha kweli hana akili kwa kuwa mtu mwenye akili zake timamu hawezi kwenda kwenye chombo cha habari na kueleza hayo aliyoyasema,” alisema Jokate akionesha kukasirishwa na maneno ya Diamond.
Wema akiwa na Diamond.
WEMA HATAKI MALUMBANO
Ukiacha Jokate na Wema ambaye naye aliwekwa kwenye kapu moja la kuchenga kumzalia, hakutaka kumjibu Diamond kwa kuwa hataki malumbano au makuu na mtu.
PENNY ALISHAJIBU
Pia jamaa huyo alimzungumzia aliyekuwa mwandani wake mwingine, Penniel Mwingilwa ‘Penny’ kuwa yeye alitoa mimba zake mbili kwa visingio tofauti.Katika majibu yake kupitia gazeti tumbo moja na hili, Risasi Jumamosi, toleo la wiki iliyopita, Penny alisema kuwa Diamond awe mkweli na aseme tatizo lake kwani anavyojua yeye hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba.
NENO LA MHARIRI
Baada ya kila mmoja kupata nafasi ya kufunguka kivyake, ni vyema sasa malumbano yakaisha na kuuanza mwaka 2015 kwa kuchapa kazi ili kujiletea maendeleo binafsi na taifa kwa jumla.

0 comments:

ASKOFU AELEZA ALIVYOINGIZIWA MAMILIONI YA ESCROW INGIA HAPA KUPATA HABARI KAMILI

Askofu Nzigilwa
Ziliwekwa akaunti binafsi, adai ni za kanisa
 Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa, amevunja ukimya kuhusu mgao wa Sh. milioni 40 alioupata kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VIP Engineering & Marketing Limited, James Rugemalira.

Ukimya wa Askofu Nzigilwa unatokana na sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Akaunti hiyo ilifunguliwa baada ya waliokuwa wanahisa wa Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ikiwamo VIP kuingia katika mgogoro na Shirika la Umeme nchini (Tanesco).
Taarifa kwa vyombo vya habari jana ilisema fedha alizopewa Askofu Nzigilwa na Rugemalira, zilikuwa za matoleo kwa ajili ya maendeleo ya Kanisa.
Alisema kiutaratibu siyo vibaya kwa waumini kutoa michango na matoleo kwa Kanisa na watumishi wake.
Katika taarifa hiyo ambayo Askofu Nzingilwa alipotafutwa alithibitisha kwamba ni yake, alifafanua kuwa alifahamiana na familia ya Rugemalira tangu akiwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Makongo Juu, Dar es Salaam na hata baada ya kuteuliwa kuwa Askofu Msaidizi wameendelea kushirikiana na kuwasiliana katika masuala mbalimbali ya kikanisa na kijamii.
“Samahani nipo kwenye kazi fulani hatuwezi kuongea kwa sasa. Ni kweli kuna taarifa nimeitoa leo kwa Tumaini Media na nimewaambia waitume pia kwa vyombo vingine vya habari,” alisema Askofu Nzingilwa alipowasiliana na NIPASHE kwa kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms).
Askofu Nzingilwa katika taarifa hiyo aliyoisaini juzi, alisema mwanzoni mwa Februari 2014, Rugemalira alimuomba namba ya akaunti yake ya benki ya Mkombozi ili aweke matoleo yake.
Alisema aliombwa akaunti yake na Rugemalira mapema Februari, mwaka jana na kwamba hakuwahi kufahamu kiasi cha fedha kilichowekwa kwenye akaunti yake hadi alipoangalia taarifa ya benki Februari 27, mwaka jana iliyoonyesha aliingiziwa Sh. milioni 40.4.
“Niliwasiliana na Rugemalira na kumwambia nimeona kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti yangu, naye akaniambia hayo ni matoleo yake ambayo anaamini yatasaidia katika shughuli zetu za kitume na kichungaji. Nikamshukuru kwa ukarimu huo mkubwa,” alibainisha Askofu huyo.
Alisema matoleo hayo yalipokelewa kwa moyo mnyofu kutoka kwa mtu anayefahamika kwa ukarimu wake katika kusaidia Kanisa na watumishi wake.
“Kampuni anazomiliki na biashara anazofanya Rugemalira kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, haviwezi kumpa shaka mtu anayemfahamu kuhusu uwezo wake au kampuni yake kutoa mchango mkubwa kama huo,” alisema.
Alisema ni desturi ya kawaida katika Kanisa kwa waamini kutoa michango na matoleo mbalimbali kila mmoja kwa kadri ya uwezo na ukarimu wa moyo wake na kwamba matoleo ya waamini hutumika katika shughuli za uinjilishaji na uendeshaji wa Jimbo, Parokia na taaisi zake.
Askofu huyo aliongeza kuwa hutumika katika miradi maalum iliyokusudiwa na matoleo hayo na kwa kadri ya matakwa na lengo la mtoaji.
“Nilipokea matoleo hayo kwa roho safi na moyo mweupe na wa shukrani kama tunavyofanya siku zote tunapopokea ukarimu wa michango na matoleo ya waamini wetu. Na tangu matoleo hayo yalipotolewa Februari, mwaka jana, hakuna mamlaka yoyote iliyowahi kuniuliza ,” alifafanua na kuongeza:
“Nawaomba waamini tuendelee kujitoa kwa hali na mali katika kulijenga Kanisa la Mungu; kila aliyepewa talanta na Mungu aitumie kwa kuzalisha matunda mema ili kulijenga kanisa letu na hatimaye kuurithi ufalme wa mbinguni.”
Hata hivyo, alisema Kanisa hilo litaendelea kuwa mstari wa mbele katika kutetea haki, ukweli na uadilifu, na halitarudi nyuma wala kukaa kimya katika kukemea maovu katika jamii.
UHUSIANO NA FAMILIA YA RUGEMALIRA Alisema familia ya Rugemalira ni waumini wakatoliki wanaosali katika Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Rozari Takatifu, Makongo juu katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam na kwamba ni washiriki wazuri katika shughuli za ibada na wamekuwa na moyo mkubwa wa ukarimu katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo ya Kanisa ndani na nje ya jimbo.
“Binafsi, nimeifahamu familia hii muda mrefu kutokana na majitoleo yao katika shughuli za Kanisa na uhusiano baina yangu na familia hiyo ulizidi kuimarika pale alipopangwa kufanya huduma za kichungaji katika Parokia ya Makongo Juu nikiwa Paroko Msaidizi, mwaka 2008,” alibainisha na kuongeza:
“Kipindi hicho ilikuwa katika harakati za ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba ya mapadre na mikakati ya ujenzi wa Kanisa jipya la Parokia na walikuwa wachangiaji wazuri katika kufanikisha.”
Hata hivyo, aliwaomba waumini wa kanisa hilo kuendelea kujitoa kwa hali na mali katika kulijenga Kanisa la Mungu.
Aidha, Askofu huyo alisema utume wa kanisa siku zote umekuwa ukiwezeshwa na kutegemezwa kwa nguvu ya Mungu Roho Mtakatifu anayeliongoza kanisa katika ukweli wote, na kwa sadaka, matoleo na michango mbalimbali ya hali na mali kutoka kwa waamini na watu wengine wenye mapenzi mema waliopo ndani na nje ya nchi.
“Kwa waumini kutoa michango na matoleo kwa kanisa na watumishi wake ni jambo la kawaida katika desturi za imani yetu tangu nyakati za mitume,” alisema Askofu Nzigilwa.
KASHFA YA ESCROW Mei, mwaka jana, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, aliibua kashfa ya kuchotwa kwa zaidi ya Sh bilioni 306 katika akaunti ya Tegeta Escrow, ambayo ilipingwa vikali na baadhi ya wabunge na viongozi wa serikali na Mbunge huyo kutakiwa kufuta kauli kwa kulidanganya Bunge.
Mbunge huyo aliendelea na msimamo wake na kutaka Bunge kuunda kamati ya kuchunguza sakata hilo.Juni mwaka jana, Bunge liliagiza Ofisi ya CAG kufanya ukaguzi wa fedha hizo na ripoti yake kuwasilishwa Bungeni.
Baada ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kukamilisha kazi yake, ripoti hiyo ilikabidhiwa kwa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), chini ya uenyekiti wa Zitto Kabwe.
Kamati hiyo ilifanya uchunguzi na kuweka wazi ripoti na mapendekezo yake ya awali ambayo yalizua mjadala mkali bungeni kiasi cha kutishia Bunge kushindwa kufikia maamuzi ya pamoja na baadaye Spika Anne Makinda, aliunda kamati ya maridhiano ambayo ilikubaliana katika maazimio yaliyowasilishwa Bungeni na Zitto.
Novemba 26, mwaka jana, Zitto, aliwasilisha ripoti iliyowataja viongozi wa dini, serikali na watu wengine waliopokea fedha za Tegeta Escow.
Viongozi wa dini waliotajwa na Zitto kiasi cha fedha walichopokea kwenye mabano ni Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini (Sh. milioni 80)  Askofu Eusebius Nzigirwa na Padri Alphonce Twimanye Simon (Sh. milioni 40.4), ambao walipewa fedha hizo kupitia Benki ya Mkombozi.
VIONGOZI WA SERIKALI WALIOWAJIBIKA Desemba 16, mwaka jana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, alijiuzulu nafasi kutokana na ushauri alioutoa.
Desemba 22, mwaka jana, Rais Jakaya Kikwete, alimfukuza kazi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ambaye katika kashfa hiyo alipokea kiasi cha Sh. bilioni 1.6, huku akimuweka kiporo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Desemba 23, mwaka jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alimsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.
VIONGOZI WENGINE WALIOPATA MGAWO Viongozi waliopata mgawo wa Rugemalira Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (bilion 1.6); Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (milioni 40.4); Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona (milioni 40.4); Mbunge mstaafu Paul Kimiti (milioni 40.4); Msajili wa zamani wa Hazina na Mjumbe wa Bodi ya Tanesco, Dk. Enos Bukuku (milioni 161.7).
Wamo pia Jaji Profesa Eudes John Ruhangisa (milioni 404.25) na Jaji Aloysius Mujulizi (milioni 40.4).
Watumishi wa umma ni aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa wa Rita, Philip Saliboko (milioni 40.4); aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Emmanuel Ole Naiko (milioni 40.4) na Mtumishi wa TRA, Lucy Appolo (milioni 80.8).


CHANZO: GAZETI LA NIPASHE

0 comments:

Safari ya vijana wa 3 kutoka nzega waliotembea siku 37 kufikisha ujumbe kwa Rais Kikwete wakamatwa na polisi

 Vijana watatu kutoka  nzega wametembea kwa miguu kwa siku 37  hadi jijini dar es saalam kwa lengo la kutaka kwenda kumuona Rais Jakaya Kikwete kufikisha malamiko yao ikiwenmo kukithiri kwa vitendo vya rushwa na ubadilifu wa rasilimali za umma lakini safari ya vijana hao ikaishia mikononi mwa polisi baada ya kukadi agizo halali la  mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh. Jordan Rugimbana la kuwataka wafuate taratibu za kumuona kiongozi huyo wa nchi.
Vijana hao ambao  walivamia magunia na kusema kuwa wamevaa hivyo ikiwa ni ishara ya kuonyesha uchungu wa namna ambavyo rasilimali za taifa zisivyowanufaisha wazawa.
 
Baadhi ya wananchi walioshuhudia  matembezi hayo  wamewataja vijana hao kama ni wazalendo ambao ujumbe wao unawagusa mamilioni ya watanzania ambo hawana ujasiri na uwezo wa kufanya kitendo cha  kijasiri kama hicho.
 
Baada ya vijana hao kufika kwa mkuu wa wilaya walifanya mazungumzo naye ambapo mkuu huyo aliwtaka wafuate taratibu za kumuona  rais na kusisitiza kuwa matembezi hayo yalipaswa kuishia hapo.
 
Kufuatia maagizo hayo vijana hao hawakukubaliana na agizo  hilo na kusema wao bado ni yao ya kwenda ikulu Ipo pale pale na ndipo walipioanza safari nyingine kuelekea huko na kabla ya hapo walitoa matamko yao mbele ya ofisi ya mkuu wa wilaya kablya ya kukamtwa na kupelekwa kituo cha polisi magomeni.
 

0 comments:

BREAKING NEWS: JENGO LAANGUKA MCHANA HUU NA KUJERUHI WATU MJI MKONGWE, ZANZIBAR

Kikosi cha Uokoaji kikitoa huduma ya kwanza kwa majeruhi katika eneo la tukio.

JENGO moja llililopo eneo la Mji Mkongwe, Zanzibar limeporomoka na kujeruhi watu kadhaa leo majira ya saa tano asubuhi. Idadi kamili ya majeruhi katika ajali hiyo bado haijafahamika.


Muonekano wa jengo hilo baada ya kuanguka.


TUTAWALETEA HABARI KAMILI HIVI PUNDE

0 comments:

IDARA YA POLISI NDIO TAASISI INAYOONGOZA KWA KUCHUKUA RUSHWA ZAIDI NCHINI TANZANIA... IDARA YA MAHAKAMA INAFUATA

Idara ya polisi ndio taasisi inayochukua hongo zaidi nchini Tanzania kulingana na ripoti ya ufisadi katika jumuiya ya Afrika mashariki.

Ripoti hiyo inasema kuwa maafisa wa polisi walipokea asilimia 25 ya hongo zote zilizotolewa kwa wafanyikazi wa taasisi za uma mwaka uliopita.

Ya pili ni idara ya mahakama,ambayo wafanyikazi wake walitia mfukoni asilimia 18 ya hongo,huku mashirika yalio na majukumu ya usajili na utoaji wa leseni yakiwa katika nafasi ya tatu kwa asilimia 10.

kwa mujibu wa gazeti la The Citizen, Idara ya Polisi nchini Tanzania imetajwa kuwa ya tatu kwa ufisadi katika jumuiya ya Afrika mashariki.

Polisi wa Uganda wanaongoza wakifuatiwa na wale wa Kenya katika nafasi ya pili na wale wa Burundi wakiwa katika nafasi ya nne.

Kulingana na ripoti hiyo maafisa wa polisi wa Rwanda ndio wasiochukua hongo ya juu Afrika mashariki.

Utafiti huo ulifanywa mwezi Julai na Agosti mwaka uliopita na shirika la lenye na maslahi ya kimaendeleo barani afrika ForDIA likishirikiana na Jukwaa la uwazi nchini tanzania Trafo.

0 comments:

NYALANDU AANZA KAMPENI ZA RAIS 2015 KANISANI, AMHUSISHA JK NA MAJINI SOMA HAPA KWA HABARI KAMILI

Jana kwenye ibada ya mkesha wa kuupokea mwaka mpya uliooneshwa live star TV, Waziri Nyalandu alijitokeza wazi na kuongea kikampeni akiomba waumini wa dini ya Efata kumchagua kuwa Rais.

Isitoshe, Nyalandu aliongelea utawala wa Rais Kikwete kuwa ni utawala unaolindwa na majini saba, ingawa hakufafanua alimaanisha nini, lakini alishangiliwa sana na waumini wa Efata.


Anayejiita nabii na mtume Mwingira, naye aliongeza kuonesha wazi kuwa Nyalandu ndie chaguo lao.


My take: Huo ni udini wa wazi kabisa. Nyalandu ameanza kutumia kanisa analosali kuomba kura za waumini wake.


Kuna maneno ambayo yamemkosea adabu Mwenyekiti wa CCM, Professa Kikwete, kwamba analindwa na majini saba. Sina hakika kama maneno hayo ni rasmi ndani ya CCM au ni ya kanisa la Mwingira.


Wadau karibuni.

0 comments:

NIKKI MBISHI ATANGAZA KUACHA MUZIKI KWA SABABU HANUFAIKI CHOCHOTETE SOMA HAPA KWA HABARI KAMILI

hhhRapper Nikki Mbishi leo ametangaza kuwa ameacha muziki.
Rapper huyo ameelezea uamuzi wake wa kuachana na muziki kutokana na kutokunufaika chochote na kwamba hawezi kuendelea kuwa mtumwa mwa kiwanda cha muziki.

“I’m glad to say I’ve officially decided to quit music….Wishing all the best to the slaves and victims of Music industry,” ametweet rappe huyo. “Nitaziachia tracks zangu zote ambazo hazijatoka for free then SITOINGIA TENA STUDIO kufanya wimbo(MUZIKI BASI).”

“The Industry is designed to frustrate the cats with high degrees of talents and intelligence. Ngwea,Langa,Geez mlale pema wanangu. I will remain as a music fan…and u guys need to find me some hip hop heads to listen to…asanteni,” ameongeza.

“Bora kuwa JAMBAZI kuliko MWANAMUZIKI. Tusije kushikiana bunduki bure maana milango ya kutoka kimaisha ni mingi na muziki ni burudani na biashara sio vita. Industry full of stupid and Illiterate but rich and famous. Mpaka lini tutauza UNGA kwa kivuli cha kuwa WASANII?”

0 comments:

Ingia Hapa Kutazama Picha Za Kimahaba Za V Money Na Jux Unautafsiri Vipi Ukaribu Wao Huu ? 2015 Ndio Hii.


jux
Ni miongoni mwa maswali mengi yanayoulizwa kuhusu wapenzi wa bongo fleva, Vanessa Mdee na Jux, Je ni wapenzi au marafiki tu ? Kwenye interview tofauti nilizofanya nao kila mara V Money husema kuwa ” Me na Jux ni marafiki sana, na tumekuwa hivi kwa muda mrefu” . Je mwaka 2015 wataweka wazi kuwa kinachoendelea kati yao ni zaidi ya Urafiki ?
vanesaa 4 vanesaa 5
vanessa 2 vanessa

0 comments: