CHADEMA YAMBWAGA ZITTO MAHAKAMANI SOMA HAPA KWA HABARI KAMILI



Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, leo imetupilia mbali shauri lililofunguliwa na Zitto Zubeir Kabwe mwaka jana, akipinga kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kumjadili, kujadili uwanachama wake na cheo chake ndani ya Chadema, akikitaka chombo hicho cha sheria kwa kuweka zuio la muda, kusubiri kwanza rufaa yake aliyokuwa amekata katika Baraza Kuu la Chadema.
Mahakama Kuu iliyoketi chini ya Jaji Richard Mziray, ilikubaliana na hoja za mawakili wa Chadema waliosema kuwa ufunguaji wa kesi hiyo ulikosewa baadhi ya vifungu vya sheria na hivyo kumtaka mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kulipa gharama zote za kesi hiyo. Zitto hakufika mahakamani badala yake alituma mawakili wake.
Wakati Zitto akifungua kesi hiyo Januari mwaka jana, tayari Chadema ilikuwa imewafukuza uanachama Dr. Kitilya Mkumbo na Samson Mwigamba ambao pamoja na Zitto, walituhumiwa kupanga njama za kufanya mapinduzi ya uongozi ndani ya chama hicho. Zitto alikuwa akitetewa na wakili Albert Msando wakati Chadema iliwakilishwa na Tundu Lissu, Peter Kibatala na John Mallya.


0 comments: