NDOA YA LULU YABUMA:ADAI ANAETAKA KUMUOA AWE NA SIFA HIZI...SOMA SIRI HIYO HAPA IKO HAPA


Mwigizaji wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’. 

BAADA ya kuwa na malengo ya kuolewa mwaka 2014, mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameibuka na kusema imeshindikana lakini hajilaumu wala hamlaumu mtu yeyote kwa kutotimiza suala hilo kwani anaamini Mungu ndiye anayewezesha kila kitu.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Lulu alisema mwaka 2014 alikuwa na malengo mengi likiwemo suala la ndoa lakini kwa kuwa Mungu ndiye muweza, atapanga upya suala hilo na anaamini litakuja kutimia.
“Ndoa ni mipango ya Mungu, huwezi kulazimisha hata siku moja, sisi wanadamu huwa tuna mipango yetu lakini ili ifanikiwe lazima kuwe na baraka za Mungu,” alisema Lulu.

Akizidi kupiga stori na paparazi wetu, Lulu alisema kwa mwaka huu na mwakani hawezi kuweka malengo ya ndoa kwani bado kuna mambo yake hajayaweka sawa hivyo suala la kuolewa ataliweka hadharani baada ya miaka miwili ijayo.
‘Lulu’ akipozi.

“Sina mpango hata kidogo kwa mwaka huu wala mwakani labda baada ya hii miaka kupita ndiyo ninaweza kupanga tena suala la ndoa,” alisema Lulu.

Alipotakiwa kumtaja mpenzi aliyenaye kwa sasa, Lulu aligoma kufunguka lakini akakubali kuanika siri za mwanaume anayetaka kuwa mumewe.
“Kwanza nahitaji mwanaume atakayenielewa kwa kila kitu, pia awe na mapenzi ya kweli na atakayeniangalia kama Lulu na siyo kama Elizabeth pekee. Anapaswa kutambua na kusapoti kazi zangu za sanaa,” alisema Lulu.
Kuhusu mikakati yake ya sanaa mwaka huu, Lulu alisema ana mpango wa kuendelea na masomo huku akiwa pia na ‘project’ kubwa mbili ambazo anatarajia kuzifanya.
“Nina project kubwa mbili mwaka huu, muda utakapofika kila mmoja atazijua maana nitaziweka wazi,” alisema Lulu.

0 comments:

BAADA YA NIKKI MBISHI KUTANGAZA KUACHA MUZIKI, HAYA NDIO MANENO YA CHID BENZ


.
.
Baada ya msanii wa Hip Hop Nikki Mbishi aka Baba Malcom kutangaza kuwa ameacha kufanya kazi ya muziki sasa Chid Benz amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa ameshafanya mazungumzo na msanii huyo  na kumtaka asichukue uamuzi huo mapema kwani hata yeye amepitia katika changamoto hizo.
Chid Benz alichukua nafasi hiyo kuwataarifu mashabiki wa muziki kupitia ukurasa wa facebook na kuandika ‘Nakanusha habari za Nikki mbishi kuacha mziki,nimeongea nae kama kaka na kumgusia mengi,najua amenielewa na nimemwambia asikubali wale wanaomkubali waanze kukubali wengine.mimi nimekumbana na vingi na watu weengi waliaminishwa kama nimeshushwa kimziki,jimefanyiwa mengi ambayo kwa muda ule nsingeweza kuelezea kila mtu nini kinaendelea,so if kikitokea kibaya kinatangazwa mpk kwenye taarifa za habari mbona mziki hauchezwi?ningekua sina nguvu hio nisingesumbua watu kuniweka front page..but bado nipo na nimekomaa.na naishi na naona wanaopewa kipaumbele na najua bado mimi ni mimi.Iron
.

0 comments:

ALICHOKIANDIKA TUNDU LISU KABLA YA WALE VIJANA WATATU KUTOKA GEITA KUKAMATWA NA POLISI



  

Kuna vijana watatu kutoka mkoani Geita,
wanakuja kwa mguu kuja kuonana na rais
Kikwete ikulu, ili kueleza kero zao kuhusu nchi
yao, je? watakaribishwa ikulu? au wataitwa
wahuni na wavuta bangi? nakumbuka rais
amewahi kuwakaribisha watu wengi ikulu kama
Ray c, Diamond, mzee yusufu, n.k, ambao ni
waimbaji majukwaani, wala sio watetezi wa
wanyonge, wengine ni wala madawa ya kulevya
tu, mh. Rais wanakuja hao vijana watatu kutoka
Geita nakushauri uwapokee, otherwise
utaonekana una upendeleo kwa kuwakaribisha
watu unaowataka wakati ikulu sio mali yako. 

0 comments:

BREAKING NEWS: MMILIKI WA VIP ENGINERING RUGEMALIRA AMEFUNGUA KESI MAHAKAMA KUU AKIIDAI SERIKALI BILION SH. 398



Mmiliki wa VIP Enginering, aliyekuwa anamiliki hisa IPTL Ndugu Rugemalira amefungua kesi mahakama kuu akiidai serikali jumla ya Sh. 398 bilion zilizokuwemo/zinazotakiwa kuwemo katika Escrow Account ya Tegete na zilizolipwa kwa kampuni ya PAP na kuleta mjafala mkubwa bungeni.

Katika madai yake, mwenye hisa hatambui malipo yote yaliyolipwa na serikali kwa kampuni ya PAP kwani kampuni hiyo haikuwa na nyaraka halali kutoka kwa msajili wa makampuni BRELA, Taxe Clearance Certificate kutoka TRA, kuandikishwa Tanzania Investment Center na wala mmliki wake kuwa na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini kutoka idara ya Uamiaji.

Katika hoja yake mdai anasema kuwa ni jukumu la serikali kuwahakiki wawekezaji wa nje ili kuwalinda wawekezaji wa ndani pindi tu wanapoingia ubia na wawekezaji wa nje.

Ameendelea kudai kuwa, kwa uzembe huo wa serika kwa kutotimiza uhakiki wake wa kigeni ulisabibisha kampuni yake ya VIP Engineering kuingia ubia na Kampuni Feki na kumsababishia hasara ya sh. Bilion 56 kwani alizimika kuvunja ubia wao na kumfungulia mashitaka mbia mwenza PAP baada ya kugundua ubabahishaji wa uhalali wa kampuni hiyo. Hivyo ameitaka tena serikali kulipa gharama zote alizotumia kuendesha kesi sh.36.8 bilion.

Aidha amedai kuwa aliwafahamisha serikali kutolipa malipo yoyote yaliyokuwemo kwenye account ya Escrow na endapo serikal ingeona kuna haja ya kufanya hivyo basi ilipe kwa VIP au IPTL account ambayo yeye alikuwa signatory.

Katika uwasilishaji wake mahakamani hapo anadai kutofahamu au kutambua kulipwa kwa PAP. Hivyo serikali inatakiwa kulipa tena madai yote kwa VIP au IPTL. Amewapa serikali siku 14 tu toka 1 Januari,2015 kuwa wamelipa malipo yote.

Katika madai hayo, ili kuyadhitisha ameambatinisha :
1. Report ya Mkaguzi mkuu wa hesabu za serika inayodhibitisha baadhi ya pesa kulipwa kwa PAP
2. Mkaguzi mkuu kudhibitisha kuwa mlipwaji hajawahi kusajiliwa kama mlipa kodi wala kupewa Taxe clearance certificate.
3. Report ya mdhibi mkuu wa Rushwa kuthibitisha kuwa kampuni iliyolipwa haikusajiliwa BRELLA na wala haikuwa na sifa au uhalali kufanya kazi yoyote ya ugavi dhidi ya Shirika lolote la Uma.
3. Report ya Bunge kama muhimili mwingine wa nchi kupitia kamati yake ya hesabu za serikali na mashirika ya uma kutodhibitisha/kudhibitisha juu uhalali wa PAP, mmiliki wa kampuni ya PAP na utendaji wake wa kazi.
4. Mapendekezo ya kamati ya bunge kwa serikali dhid ya PAP, mali zake na mmiliki wake.
5. Mapendekezo ya bunge kwa serikali yanayodhibitisha kuwa PAP haikuwa halali.
6. Mapendezo ya bunge kwa serikali juu ya watendaji wote walioshilikiana kwa pamoja ya kuilipa kampuni isiyo halali.
7. Baadhi ya magazeti likiwemo gazeti la serikal kudhibitisha mkuu wa nchi kupokea na kuridhia mapendezo hayo.
8. Magazeti pamoja na la serikali kudhibitisha serikali kwa kuwaadhibu watendaji wote waluofanya udhembe wa kulipa kampuni isiyo halali.
9. Mkanda wa video ya Rais wa nchi katika hotuba yake kukili watendaji wake kuilipa kampuni isiyo halali na kawasimamisha kazi kwa uzembe huo.
10. Barua ya Mwanasheria mkuu wa serikali kwa Rais ya kuomba kujiuzuru kwa kufanya uzembe huo wa kulipa kampuni isiyo halali.
11. Barua ya Rais kwa Mwanasheria mkuu kukubali kujiuzuru kwake kwa kutoa ushahuri wa kulipa kampuni isiyo halali.
Kesi hiyo uenda ikaamsha tena hisia za wananchi juu ya malipo ya Escrow account. Ni mtihani mwingine kwa serikali kwani Bunge na wanachi hawako tayari kuona pesa kama hiyo ikilipwa tena.

0 comments:

KIONGOZI WA CHADEMA ASIMAMISHWA KAZI..MWINGINE APEWA ONYO KALI


Naibu Katibu Mkuu  CHADEMA  Zanzibar,  Salum  Mwalimu akiutubia mkutano wa hazara  mjini  Nansio Wilaya ya  Ukerewe, Mwanza lengo kushukulu wananchi kwa kukipatia ushindi katika uchaguzi wa Serikali  za  mitaa uliopita. Wilaya  hiyo Chadema imepata  viti 47 vya Serikali za vijiji huku ccm  ikipata 27 na CUF viwili.
Ukerewe. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu amemsimamisha kazi mjumbe wa kamati ya utendaji ya chama hicho Wilaya ya Ukerewe, Wilbrod Machemli kwa kushindwa kutimiza wajibu wake, ikiwa ni pamoja na kutotangaza ujio wa kiongozi huyo.
Rungu hilo pia limemkuta katibu wa Chadema wilaya hiyo, Libelatus Mlebele ambaye amepewa onyo kali.
Akizungumzia hatua hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Nansio jana, Mwalimu ambaye ameanza ziara mkoani hapa juzi kwa lengo la kuwashukuru wananchi baada ya kukichagua chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, alisema hakuridhishwa na maandalizi yaliyofanywa na viongozi hao.
Kutokana na hali hiyo, Mwalimu alimwagiza Mwenyekiti wa wilaya wa chama hicho, Jacobo Munyaga kwa gharama zake amwandalie mkutano mwingine kabla ya mwisho wa mwezi ujao.
Mwalimu pia alitilia shaka matumizi ya fedha yaliyotajwa kutumika kutangaza uwepo wa mkutano wake.
Alisema Chadema hakipo tayari kulinda viongozi wazembe na wasiowajibika na kuwaonya wajumbe wa kamati tendaji hasa katibu ambaye bado yupo katika uangalizi wa miezi sita kwa maelezo kuwa anaweza kuondolewa kazini.
Kabla ya kuchukua uamuzi huo, Mwalimu aliwaita mbele wakazi wanne wa kata za Kakerege, Nansio, Nakatungulu na Kagera ambao walikiri kutosikia matangazo ya ujio wake.
Hatua hiyo aliichukua baada ya kuwasili katika Uwanja wa Mongera wa mjini Nansio saa 9:30 alasiri huku kukiwa na idadi ndogo ya watu ikilinganishwa na ziara zake za nyuma.
Mbali na hilo, pia Mwalimu ametumia mkutano huo kukemea matumizi mabaya ya fedha za serikali yanayofanywa na viongozi waandamizi wakati huduma za kijamii zikizidi kuwa mbaya.
Alisema ziara za mara kwa mara za nje ya nchi zisizo za lazima zinazofanywa na Rais Jakaya Kikwete pamoja na viongozi wengine hazina tija kwa taifa.
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Joseph Mkundi akizungumza katika mkutano huo, alisema katika katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wao wamepata mafanikio makubwa.
Alisema mbali na kusimamia vyema matumizi ya fedha za serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, pia halmashauri hiyo imekamilisha mipango ya kununua greda moja la kutengeneza barabara lenye thamani ya Sh400 milioni hivi karibuni chama hiko kimeluwa kikipigania kukishinikiza serikali kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi.
Hata hivyo, alisema mbali ya halmashauri hiyo kupata hati safi ya matumizi ya fedha za umma pia hivi karibuni huko jijini Nairobi Kenya, Halmashauri hiyo ilipata tuzo ya kukidhi vigezo vya sheria ya ununuzi ya umma kati ya wilaya 166 za nchi nzima.


chanzo: gazeti la mwananchi

0 comments:

ATANGAZA KUUZA FIGO KWA SH90 MILION SOMA HAPA KWA HABARI KAMILI


Mkazi wa Morogoro, Andrew Germanis Chimulimuli ametangaza kuingiza sokoni figo yake ambayo amesema anaiuza Sh90 milioni ili kukabiliana na ugumu wa maisha.
Chimulimuli aliyefunga safari kutoka Ifakara, Morogoro hadi jijini Dar es Salaam ili kufanya biashara hiyo alisema ameamua kutoa kiungo chake hicho muhimu kutokana na ugumu wa maisha unaomkabili.
“Nimeamua kujitolea nafsi yangu ili niisaidie familia yangu, kwa sababu mimi si kitu kama sina fedha, ndiyo maana nimejitolea kutoa figo yangu nipate fedha,” alisema Chimulimuli.
Chimulimuli alisema anataka kuiuza figo hiyo kwa gharama ya Sh90 milioni ingawa alikubali kufanya mazungumzo ya kupunguza bei pindi atakapopatikana mteja.
Takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii zinaeleza kuwa kuna wagonjwa 470,000 nchini ambao figo zao zimeshindwa kufanya kazi kabisa na wanahitaji upandikizaji.
Ingawa uamuzi wa Chimulimuli unaweza kuwa msaada kwa Watanzania wenye mahitaji, lakini kimaadili ya afya na kisheria, jambo hilo linakatazwa kufanywa kiholela hadi pale linapofuata taratibu.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Figo Tanzania, Jaji Frederick Werema aliwahi kuliambia gazeti hili kwamba anashangazwa na hatua za baadhi ya watu kuchukua uamuzi wa kuuza figo kwa ajili ya kujipatia fedha.
“Kutoa figo ni kosa la jinai, lakini siyo hivyo tu, kutoa figo ni lazima ufuate taratibu za kisheria na za kitabibu,” alisema Jaji Werema miezi kadhaa iliyopita.
Biashara ya figo
Aprili mwaka jana, gazeti hili lilifanya uchunguzi na kubaini kuwa wapo Watanzania wanaouza figo zao kiholela kwa ajili ya kujipatia fedha.
Gazeti hili liliwasiliana na vijana kadhaa ambao kwa nyakati tofauti walikubali kuwa wanauza figo zao na baadhi wakieleza kuwa tayari walishauza kwa gharama za kati ya Sh50 milioni hadi Sh80 milioni.


Chimulimuli alisema kutokana na ugumu wa maisha, kipato chake kimekuwa kigumu sana na hakiwezi kukidhi mahitaji ya familia.
“Mtu akikuona kwa nje anaweza kukuona kama upo sawa na una maisha mazuri lakini ukweli ni kuwa nina maisha magumu sana,” alisema. Kuhusu hatima yake kiafya, alisema yeye ni msafiri na hawezi kuishi milele na hivyo bora auze figo yake iwe msaada kwa wengine wenye mahitaji.
“Ni bora nifanye kitu cha halali kinachoigharimu afya yangu mwenyewe badala ya kuiba au kufanya uhalifu mwingine,” alisema Chimulimuli.
Uchangiaji wa figo
Daktari bingwa wa figo katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Linda Ezekiel alisema uchangiaji wa figo ni mchakato mrefu na si suala la fedha tu.
Dk Ezekiel alisema mchakato wa kuchangia figo ni mrefu kwani mchangiaji hutakiwa kuwa na kundi la damu linalofanana na mgonjwa.
Alisema vipimo vya afya hufanyika ambapo maradhi yanayoweza kuambukiza kama homa ya ini, magonjwa ya zinaa na Virusi vya Ukimwi, navyo huangaliwa kwa umakini mkubwa.
“Ni lazima tuhakikishe mtu ameridhia kabisa kufanya hivyo na katika hali hiyo ni lazima tumfanyie mtu ushauri wa kisaikolojia na afahamu hatua za utoaji huo sambamba na madhara anayoweza kuyapata,” alisema.
Kuhusu changamoto ya maradhi hayo Dk Ezekiel alisema kusafisha figo ‘dialysis’ ni gharama kubwa ambapo kwa tiba moja mgonjwa hutakiwa kulipa Sh300,000 na tiba hiyo hufanywa angalau mara tatu kwa wiki.
Hata hivyo Dk Ezekiel alisema kwa anayechangia figo na kubaki na moja hawezi kupata madhara kiafya kwani figo moja ina uwezo mkubwa wa kufanya kazi zake.

0 comments:

SAKATA LA ESCROW: KAFULILA AJIPANGA KUPELEKA HOJA BINAFSI KUMNG'OA PINDA SOMA HAPA


SASA kuna kila dalili kuwa mwangwi wa kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow iliyotikisa mkutano wa 16 na 17 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, utaendelea kusikika kwa namna ya kuishinikiza Serikali kuwajibika zaidi.
 
Dalili hizi zimeonyeshwa waziwazi na baadhi ya wabunge hususani waliokuwa vinara wa kupambana na kashfa hiyo ambao hawajaridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Rais Jakaya Kikwete dhidi ya watendaji wa Serikali na viongozi wa kisiasa walioguswa na ripoti ya uchunguzi wa kashfa hiyo.
 
Mmoja wa wabunge walio katika mkakati huo ambao kimsingi unalenga kumng’oa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ni David Kafulila wa Kigoma Kusini.
 
Kafulila katika mahojiano yake na waandishi wa habari alisema hatua zilizochukuliwa na Rais Kikwete kushughulikia maazimio nane ya Bunge haziridhishi na kuongeza kuwa kabla ya kuketi kwa mkutano wa 18 wa Bunge anapaswa kuwa amemfukuza kazi Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
 
Alisema Waziri Muhongo ni muhusika muhimu katika kashfa hiyo, kwa sababu alidiriki kusimama bungeni na kulidanganya taifa kuwa fedha zilizokuwa zimehifadhiwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow hazikuwa za umma hadi uchunguzi wa vyombo vya dola ulipothibitisha pasipo shaka kuwa ni za umma.
 
“Hatufanyi haya kwa lengo la kumkomoa mtu, hapana kabisa. Sisi tuna dhamira ya dhati ya kutetea maslahi ya taifa kwa hiyo hatuko tayari kumuona Rais akiendelea kumuacha kiporo Waziri Muhongo.
 
“Rais anaonekana kusuasua kuchukua uamuzi dhidi ya Waziri Muhongo, sasa kama itatokea akashindwa kutengua uteuzi wake hadi Bunge lijalo tutawasilisha hoja binafsi ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu tukiwa na kusudio la kumng’oa kwenye wadhifa wake, hiyo ndiyo njia pekee ya kumwondoa Waziri Muhongo,” alisema Kafulila.
 
Alipoulizwa iwapo mkakati huo wa kumng’oa Waziri Mkuu Pinda unaungwa mkono pia na wabunge wa CCM, alisema hawezi kuzungumzia msimamo wa wanasiasa wengine hata hivyo, ujasiri waliouonyesha baadhi ya wabunge wa chama hicho wakati wa mjadala uliopitisha maazimio ya Bunge unaondoa shaka ya kupata uungwaji mkono wa kutosha.
 
Mbali na Kafulila, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge wa Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, alipoulizwa msimamo wake kuhusu jambo hilo, akiandika kwa maandishi kupitia barua pepe alisema anaamini Serikali itatekeleza maazimio yote ya Bunge.
 
Ingawa tayari Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue amekwishamsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kupisha uchunguzi dhidi yake kwa kashfa ya Escrow, bado yapo mashinikizo yanayotaka hatua zaidi zichukuliwa kwa mujibu wa maazimio nane ya Bunge.
 
Mbali na Katibu Mkuu Sefue, Jaji Mkuu Othaman Chande bado yuko kimya kuhusu majaji wa Mahakama Kuu walioguswa katika kashfa hiyo.
 
Awali viongozi wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwa nyakati tofauti walikaririwa na vyombo vya habari wakitoa matamshi yenye mwelekeo wa kulishinikiza Bunge kuiwajibisha Serikali iwapo Rais Kikwete hatatekeleza maazimio yote nane ya Bunge.
 
Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba, ndiye aliyekaririwa kwanza akieleza kuwa endapo Rais Kikwete atashindwa kumwajibisha Prof. Muhongo, wabunge walio ndani ya Ukawa watawasilisha hoja na kushawishi wengine kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu sambamba na kuitisha maandamano nchi nzima.


Wakati shinikizo hili likizidi kushika kasi, Rais Kikwete katika hotuba yake ya kufunga mwaka aliendelea kusisitiza msimamo wake wa kumuweka kiporo Prof. Muhongo kwa maelezo kuwa uchunguzi dhidi yake haujakamilika.

0 comments:

HABARI MPYA: BAADA YA FREDRICK WEREMA KUJIUZULU, RAIS KIKWETE AMTEUA MWANASHERIA MPYA WA SERIKALI




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata 

kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

0 comments:

MKURUGENZI WA HALMASHAURI IRAMBA SINGIDA ALIPUKIWA NA BOMU, POLISI WATHIBITISHA..JWTZ WAINGIA KAZINI


Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Iramba Singida, Halima Mpitaamenusurika kifo baada ya kulipukiwa na kitu ambacho kinadhaniwa kuwa bomu la kutengenezwa kienyeji.

Kamanda wa Polisi Singida, Thobias Sidoyeka amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nyumbani kwa Mkurugenzi huyo wakati akijiandaa kwenda kazini, mlipuko huo ulitoka kwenye bahasha ambayo aliipokea juzi kutoka kwa Katibu Muhtasi wake.

Ndani ya bahasha hiyo kulikuwa na ujumbe “Poleni sana, hatuwezi kufanya dili la milioni 90 halafu mkala peke yenu, sisi mkatudhulumu tukawaacha”, baada ya kuisoma alienda nayo nyumbani bila kujua kama kuna kitu kingine ndani.

Wakati akijiandaa kwenda kazini siku ya jana ndipo mlipuko huo ulipotokea, hakuna aliyekamatwa ila Polisi wanaendelea na upelelezi wakishirikiana na JWTZ ili kubaini kama mlipuko huo ulitokana na bomu.

0 comments:

VURUGU KUBWA YATOKEA MAKABURINI SHINYANGA, NDUGU WAPASUA MWILI WA MAREHEMU! SOMA HAPA


Habari tulizozipata hivi punde zinasema kuwa kumetokea vurugu za aina yake katika makaburi ya Masekelo katika manispaa ya Shinyanga wakati wa mazishi ya mwanamke mmoja aitwaye Benadetha Steven(35) aliyekuwa anaishi katika mtaa wa Mapinduzi maarufu mtaa wa Juma Matv katika kata ya Ndala aliyefariki dunia juzi wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Tukio hili limetokea mchana huu wakati wa mazishi ya mwanamke huyo anayedaiwa kufariki dunia kutokana na uvimbe wa tumboni uliokuwa unamsumbua hivyo ndugu wa marehemu kuamua kumfanyia mambo ya kimila ili kuondoa mkosi katika ukoo wao.

Habari zinasema kuwa ndugu wa mwanamke huyo anayetokea Musoma (Mkurya) walikuwa wanataka ndugu yao apasuliwe tumbo wafanye mambo ya kimila makaburini lakini uongozi wa eneo husika wakasema utaratibu huo ungefanyika hospitalini badala ya hadharani watu wakishuhudia.

 Tunaambiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa ameolewa Shinyanga na alipofariki mwili wake ulihifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Mgogoro huo ulianzia nyumbani kabla ya kwenda makaburini,ndugu walitulia na wakati mazishi yanaendelea ndipo ndugu wa marehemu wakaingia kaburini kuzuia wananzengo wasitupie udongo makaburini.

"Mchungaji alipomaliza ibada ya mazishi akaruhusu mwili uzikwe,wananzengo wakaanza kutupia udongo,ghafla ndugu wa marehemu wakaingia kaburini na kuzuia wananzengo,wakatoa mwili wakauchana kwa wembe,wakachinja kuku,wakamwagia damu mwili wa marehemu na kumwingiza kwenye tumbo la marehemu huyo kuku,kisha wakaaanza kuzika upya", shuhuda aitwaye Sijali Jumanne alisema.

"Kitendo cha ndugu kung'ang'ania kufanya mambo yao,kiliwakera wananchi wakaamua kutoka makaburini,na jeshi la polisi limefika eneo la tukio na kuwakamata ndugu wote wa marehemu",aliongeza shuhuda huyo.

0 comments:

PANYA ROAD 36 WATIWA MIKONONI MWA JESHI LA POLISI BAADA YA KUFANYA FUJO JIJINI NA KUZUA TAHARUKI.

Jeshi la polisi nchini linawashikilia vijana 36 wa kundi maarufu Panya Road wanaodaiwa kufanya vurugu na kupora mali za watu na kusababisha taharuki katika jiji la Dar es salaam huku baadhi ya wananchi wakitoa maoni tofauti kuhusiana na tukio hilo.
Akitoa ufafanuzi wa taharuki hiyo msemaji wa jeshi la polisi SSP ADVERA BULIMBA ambaye mbali na kuwatoa hofu wananchi kuwa hali hiyo haitajitokeza tena amesema jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na vikundi vyovyote vinavyotaka kuvuruga amani ya nchi na kwamba endapo polisi wasingewadhibiti vijana hao mapema tangu wakiwa makaburini baada ya kumzika mwenzao aliyeuwawa na wananchi baada ya kuiba hali ingekuwa mbaya zadi.
 
Kufuatia tukio hilo paparazi imezunguka maeneo mbalimbali ya jiji yaliyodaiwa kukumbwa na tafrani hiyo ambapo baadhi ya wananchi wa maeneo ya magomeni ambako vurugu zilianzia wameelezea namna zilivyoanza hadi kusababisha watu kuanza kukimbia hovyo na wengine kuacha maduka yao wazi  na taarifa kusambaa maeneo mengine.
 
Katika maeneo ya mwananyamala na ubungo baadhi ya waliozungumzia sakata hilo wameitaka serikali kuangalia makundi ya vijana na ikiwezekana wapatiwe elimu ya ujasiriamali bure ili waweze kuendesha maisha huku wengine wakishauri vijana wasiokuwa na kazi mitaani wapelekwe jeshini wakafundishwe stadi za kazi pamoja na uzalendo ili kuepuka vitendo hivyo.
 
Taharuki hiyo ilitokea usiku wa tarehe mbili chanzo kikiwa ni kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la MOHAMED AYUB kuuwawa na wananchi tarehe mosi mwaka huu katika maeneo ya tandale kwa mtogole kwa tuhuma za wizi ambapo tarehe 2 maziko yalifanyika na taarifa zilizolifikia jeshi la polisi zilidai kuwa baada ya maziko vijana wenzake walijipanga kufanya fujo ili kulipiza kisasi.

0 comments:

TAZAMA PICHA ZA DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOWAPAGAWISHA MASHABIKI WAKE WA RWANDA SIKU YA MWAKA MPYA INGIA HAPA

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa amebebwa na wacheza shoo wake siku ya mwaka mpya Kigali, Rwanda.

Diamond Platnumz akifanya yake.
Nyomi ya kufa mtu waliofika siku ya shoo hiyo.
Akifanya yake na wacheza shoo wake.
Mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady' mpenzi mpya wa Diamond Platnumz akiwa katika pozi.
Muonekano wa siku ya shoo hiyo.
Diamond Platnumz (katikati) akifanya yake akiwa na Yamoto Bendi.

0 comments:

PANYA ROAD WATIKISA JIJI LA DAR





Kikundi kinachodaiwa kuwa Panya Road wametikisa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na kupora vitu, kujeruhi watu wakiwa na mapanga mikononi mwao maeneo ya Sinza, Tandale, Mwananyamala na maeneo mengineyo usiku wa leo. Maduka na baa zimefungwa na kupelekea polisi kupiga risasi hewani kuwatawanya watu waliokuwa wamekaa kimakundimakundi.
Fujo zaidi zilianzia mchana leo wakati kiongozi wao aitwaye Diamond alipouawa maeneo ya mpakani mwa Tandale na Mwananyamala darajani usiku wa kuamkia mwaka mpya kwa kukatwakatwa na mapanga.
Baada ya kumzika mwenzao leo wakajipanga kwa ajili ya kufanya fujo. Kilichotokea, polisi walikuwa eneo hilo tena ndani ya difenda kwa ajili ya kuhakikisha kuna amani wakati wa maziko.
Maziko yalipokwisha, vijana hao wakatawanyika, ila baadae wakaanza kujikusanya na kuanza kuleta fujo tena baada ya kuhakikisha kwamba polisi wameondoka.

0 comments: