
Nina
mke na watoto 3 wote tunafanya kazi. Tulipozaa mtoto wa pili wife
alianza kupunguza umuhimu wa tendo la ndoa sijua ni kwa kuzoea au
kuchoka.
Tumewekana
vikao vyetu binafsi ili kila mmoja abainishe ni vichocheo gani
vinakosekana ili tuviongeze kuboresha mchezo. Wote siyo walevi na tuko
karibu kifamilia.
Ukifuatilia
labda mke wangu ana mtu sipewi taarifa zozote mbaya. Sasa tatizo ni
kitu gani sijui. Ukimwuliza naye anakwambia mume wangu nivumilie
nitajitahidi ila baada ya mwezi anarudi kule kule.
Usipochombeza anaweza kupitiliza hata mwezi bila kukumbushia .
Hali
hii imenisumbua kwa muda sana .Ili kuepuka kugombana na kuepuka kwenda
nje kupata UKIMWI basi nikaamua nimweleze binti ambaye anatusaidia kazi
nyumbani na akaonyesha kunisikitikia kwani mi si mtu wa baa useme
ningetafuta huko na pia naogopa UKIMWI.
Binti
akasema anaweza kunisaidia lakini kwa masharti kwamba ataendelea
kuniheshimu mimi pamoja na wife ili chochote kisishtukiwe.
Kwa
mtazamo wangu hata kama mtaniona mjinga ni kwamba huyu binti anatumika
kuokoa jahazi la sivyo ningekwenda huko na huko kutafuta viruka njia
ambao wangeniweka mahali pabaya zaidi.
Tumeanza
mahusiano vizuri na tunaendelea kiasi kwamba hata wife asipokuwa tayari
mwezi mzima sipati shida na hii imenisaidia kuepuka ugomvi uliokuwa
unatokana na tendo la ndoa kutokuwa zuri.
Je wadau katika hali kama hii ambayo mke anakuwa namna hii kwa ninachokifanya nimekosea au niko sawa??
Kama unafikiri nimekosea nipe ushauri kuhusu njia mbadala na jiweke kwenye hali yangu kabla hujazungumza chochote.
0 comments: