Ile issue ya Escrow, hii ni taarifa ya Kiongozi mmoja kujiuzulu leo December 16 Soma Hapa Kwa Habari Kamili

Werema


Wiki chache zilizopita wakati Kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikiendelea, macho ya watu wengi na masikio yalikuwa na hamu ya kutaka kuujua mwisho wa sakata la Escrow.
Wakati watu wengi wakisubiri maamuzi yatakayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kuhusiana na Ripoti juu ya issue ya ubadhilifu wa fedha kwenye akaunti ya Escrow, leo December 16 kuna taarifa iliyotufikia muda mfupi iliopita kuhusu kiongozi mmoja wa Serikali kujiuzulu.


 Taarifa iliyoripotiwa na kituo cha ITV inasema aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu siku ya leo na barua yake tayari imefika Ikulu ambapo Rais Kikwete ameridhia maamuzi hayo na kumshukuru kwa uamuzi huo kwa kuwa ushauri wake kuhusiana na suala la Tegeta Escrow haukueleweka.

0 comments:

Sasa ametangaza rasmi kustaafu soka… Na huku ndiko anakoelekea kwa sasa… Ingia Hapa Kwa Habari Kamili

Theirry-Henry-in-action-o-007 Kwenye ulimwengu wa soka leo kuna story kubwa ambayo imeenea Duniani kutokana na staa mkubwa wa soka na mkongwe kutangaza kustaafu soka na kujiunga na shughuli nyingine.
Kwa wale wapenzi wa soka Thierry Henry sio jina geni kwao, amekuwa nyota ambaye ameng’aa kwenye mchezo huo kwa muda mrefu sana akichezea vilabu mbalimbali ikiwemo Arsenal na Barcelona.
download
Jamaa ametangaza rasmi kustaafu soka dakika chache zilizopita na kusema kuwa kuanzia mwakani ataanza kujishughulisha kama Balozi wa Sky Sports huku akisema kuwa anajisikia furaha kuchezea vilabu vikubwa na pia anaamini anajiunga na kituo kikubwa cha Television na mattarajio yake ni kuwa mchambuzi bora wa michezo kwenye kituo hicho.

0 comments:

Uganda In Burundi Out ndani ya Simba Sc. Soma Hapa Kwa Habari Kamili

simba okwi


Ni kama vile klabu ya Simba ina mapenzi na taifa la Uganda baada ya klabu hiyo kukamilisha jumla ya wachezaji watano raia wa kigeni ambao wanatoka kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki .

Simba imetangaza na kuthibitisha kuwa wachezaji wake watano wa kigeni kwa msimu huu ni Emmanuel Okwi, Daniel Serunkumma, Simon Serunkumma, Joseph Owino na Juko Mursheed.
Emmanuel Okwi na Joseph Owino ni wawili kati ya wachezaji watano raia wa Uganda walioko Simba.
Emmanuel Okwi na Joseph Owino ni wawili kati ya wachezaji watano raia wa Uganda walioko Simba.
Wachezaji wawili kati ya hao (Okwi na Owino ) na watatu wengine (Serunkumma Simon, Dany na Juko) wamesajiliwa katika kipindi hiki ambapo dirisha dogo la usajili liko wazi.
Nafasi za wachezaji watatu hao raia wa Uganda zimekuja kujaza nafasi za wachezaji wawili toka Burundi ambao ni Amisi Tambwe na Pierre Kwizera pamoja na Mkenya Paul Mungai Kiongera .
Dnny Sserunkumma ni raia mwingine wa Uganda aliyeko Simba.
Danny Sserunkumma ni raia mwingine wa Uganda aliyeko Simba.
Kiongera bado ataendelea kuwa mchezaji wa Simba hadi atakapopona jeraha lake la goti ambapo amekwenda kufanyiwa upasuaji nchini India huku Tambwe na Kwizera wakiwa wameachwa moja kwa moja .
Mrundi  Perre Kwizera ameachwa baada uongozi wa Simba kutoridhishwa na kiwango chake.
Mrundi Perre Kwizera ameachwa baada uongozi wa Simba kutoridhishwa na kiwango chake.

Mkenya Paul Kiongera ameachwa japo Simba itamtumia msimu ujao.
Mkenya Paul Kiongera ameachwa japo Simba itamtumia msimu ujao.
Mrundi mwingine aliyeachwa ni mfungaji bora wa msimu uliopita Amisi Tambwe.
Mrundi mwingine aliyeachwa ni mfungaji bora wa msimu uliopita Amisi Tambwe.


0 comments:

Simba yaongeza nguvu kwa kusajili beki, unajua anatoka timu gani? Soma Hapa

simba_logo_med_hr


Katika usiku ambao umekuwa na movement nyingi za wachezaji na makocha , klabu ya Simba imekamilisha usajili wa beki wa pembeni toka timu ya Mtibwa Sugar, Hassan Kessy.

Beki huyo ambaye ametokea kuwa mmoja kati ya wachezaji wa kutumainiwa kwenye klabu hiyo ya wakata miwa wa huko Manungu Turiani mkoani Morogoro, anaungana na wachezaji wapya waliosajiliwa katika kipindi hiki cha dirisha dogo ambao ni Simon Sserunkuma, Danny Sserunkuma, na Juko Murshid wote kutoka Uganda.
Kessy ambaye ametajwa kuwa moja kati ya wachezaji wanaokaribia kuwa mmoja ya wachezaji wa Timu ya Taifa Stars alichezea Mtibwa kwa mara ya mwisho katika mchezo wa kirafiki ambao ilifungwa na Azam Fc 3-1.
hassan kessy
Beki huyu anasajiliwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu yaliyofanyika chini ya usimamizi wa viongozi wa Simba wakiongozwa na Geoffrey Nyange Kaburu na Kiongozi wa Mtibwa, Jamal Bayser.
Tetesi zaidi zinasema kuwa Simba imemsajili beki huyo kwa thamani ya shilingi milioni 30.

0 comments:

Maamuzi ya Timu ya Yanga juu ya Mbrazil Emerson…

Moja ya vichwa vya habari vilivyokuwa vimepambwa na habari kumhusu Emerson.
Taarifa za usajili na kuachwa wachezaji zinazidi kuingia na safari hii inasemekana kuwa kiungo Mbrazil Emerson amekuwa mhanga wa kwanza wa kuondoka kwa kocha Mbrazil Marcio Maximo baada ya mchezaji huyo kuachwa na Yanga.
Mbrazil huyo anaondoka Yanga baada ya kucheza mechi moja pekee dhidi ya Simba ambako Yanga ilifungwa 2-0.
Emerson alishindwa kuwaridhisha mashabiki wa Yanga ambao wengi walionyesha kukerwa na uwezo mdogo wa kiungo huyo katika dakika 45 alizocheza kwenye mechi dhidi ya Simba.
Emerson alikuja nchini siku chache zilizopita ambapo alipaswa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mshambuliaji Genilson Santos Santana Jaja ambaye hakurudi baada ya kuondoka nchini kufuatia kusimama kwa ligi.
emerson

0 comments: