UPDATES: NDEGE YA AIRASIA QZ8501 ILIYOPOTEA NA WATU 162 SOMA HAPA KWA HABARI KAMILI

Kikosi cha wanamaji nchini Indonesia kikisali kabla ya kuanza zoezi la kuitafuta Ndege ya AirAsia QZ8501 katika bandari ya Pangkal Pinang kwenye kisiwa cha Sumatra.

 Kikosi cha wanamaji kikiwa kazini kuitafuta ndege iliyopotea.

Ndugu wa watu waliokuwa kwenye ndege iliyopotea wakifarijiana huku wengine wakilia kwa uchungu.

ZOEZI la kuitafuta Ndege ya AirAsia QZ8501 iliyopotea ikiwa na watu 162 ikitokea Indonesia kwenda Singapore jana limeendelea leo asubuhi.
Taarifa zilizopatikana kutoka eneo la utafutaji ndege hiyo zinadai kwamba mabaki ya AirAsia QZ8501 yameonekana baharini na kuna uwezekano ndege hiyo ipo chini ya bahari.
Saa 11:36 asubuhi, Ndege ya AirAsia QZ8501 iliondoka Indonesia.
Saa 12:12 asubuhi rubani aliomba kuipandisha ndege mpaka futi 38,000 kutokana na hali mbaya ya hewa.
Saa 12:16 asubuhi AirAsia ilikuwa bado inaonekana kwenye rada.
Saa 12:18 asubuhi AirAsia QZ8501 ikapoteza mawasiliano na rada na mpaka sasa bado haijapatikana.

0 comments:

Mashindano ya Miss Tanzania Yasimamishwa kwa Miaka Miwili

taji
Shindano la Miss Tanzania limesimamishwa kwa muda wa misimu miwili ili kutoa fursa kwa waandaaji wa shindano hilo kurekebisha baadhi ya kasoro ambazo zimekuwa zikilalamikiwa mara kwa mara.
 
Akizungumza na Mpekuzi Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa Godfrey Mngereza amesema kuwa serikali kupitia baraza hilo imefikia umamuzi huo kutokana na malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wadau mbalimbali na wapenzi wa shindano hilo.
 
Amesema imefika wakati sasa waandaji warekebishe masuala kadhaa ili kuondoa malalamiko na manung’uniko miongoni mwa wadau ili kulipa heshima shindano hilo, pia liweze kuheshimika na kila mtu.
 
Mngereza ameongeza kuwa, serikali kupitia wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imelipa dhamana baraza hilo kisheria kushughulikia masuala yote yanahusu sanaa na Utamaduni hivyo baraza hilo lina mamlaka ya kuingilia kati endapo litajiridhisha kuwa kuna masuala hayaendi sawasawa.
 
Kuhusu masuala wanayotakiwa kuyarekebisha, Mngereza amesema kuna mambo mengi hayako sawa katika mchakato mzima kuanzia katika ngazi ya vitongoji, na baraza limekuwa likipata malalamiko karibu kila mwaka lakini kwa mwaka huu malalamiko yamekuwa mengi zaidi.
 
Mngereza amesema “Kama imefikia wakati hadi mshindi wa shindano mwenyewe analazimika kuvua taji lake kwa shinikizo, ina maana kuna tatizo, kwahiyo tumewapa muda ili wakaangalie upya mchakato mzima na wafanye marekebisho” 
 
Kuhusiana na sakata la umri wa aliyeshinda shindano hilo kwa mwaka 2014 Sitti Mtemvu, Mngereza amesema kuwa suala la kuthibitisha umri wa mrembo huyo linafanyiwa kazi na Mamlaka husika ambayo ni RITA, na kwamba BASATA haihusiki nalo kabisa.
taji
 
Amemalizia kwa kusema kuwa mrembo  Lilian Kamazima aliyetwaa taji hilo baada ya kuvuliwa na Sitti Mtemvu ataendelea kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia kwa mwaka 2015 kama ilivyopangwa, lakini hakutakuwa na mashindano mengine kwa kipindi cha miaka miwili ndani ya Tanzania kuanzia ngazi ya vitongoji.

0 comments:

MAUWAJI: KIJANA MMOJA APIGWA RISASI YA SHINGO AKIWA CLUB MAISHA, INGIA HAPA KWA HABARI KAMILI.

Kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, leo usiku amepigwa risasi ya shingo na watu wasiojulikana wakati akiingia Club Maisha ilioko Oyster Bay jijini Dar es salaam.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa tano(5) usiku ambapo kijana huyu akiwa na rafiki zake wanne(4) wakiwa ndio wanashuka kwenye gari yao waliokuja nayo, walijikuta wamevamiwa na watu wawili wasiojulikana na yeye kupigwa risasi ya shingo kisha watu hao kutokomea kusikojulikana. 

Shuhuda wa tukio hilo alisema aliwaona watu wawili walioshuka kwenye gari ndogo nyeusi ilifunga breki kwa kasi kwani walionekana walikuwa mwendo kasi sana, kisha kuwavamia watu waliokuwa wanashuka kwenye gari ilikuwa imepaki muda mfupi baada ya kufika eneo hilo. 

shuhuda huyo aliendelea kwa kusema alisikia sauti ndogo ya kitu kilicholia "pyuuu!!!" bila ya kuelewa ni nini na kisha kufuatiwa na kelele nyingi za watu hao waliokuwa wamevamiwa.

Waliotenda tukio hilo walitoweka mara moja eneo la tukio baada ya watu kujaa eneo ambalo kijana huyo alipigwa risasi alikuwa ameanguka chini.

Polisi walifika eneo la tukio na kukuta kijana huyo ameanguka chini na damu nyingi zikiwa zimemtoka sehemu za shingoni na kifuani huku akiwa amewekewa nguo shingoni ili damu isiendelee kutoka ambapo ilisemekana ilikuwa ikitoka nyingi sana, walimpakia kwenye gari yao kumuwahisha katika hospitali ya jirani ya mwananyamala, lakini kijana huyo alifia njiani akikimbizwa kuelekea hospitali
Tukio hili linaonekana nila kulipiza kisasi ingawa taarifa kamili bado hazijajulina, endelea kufatilia blog yetu kujua mwendelezo wa tukio hili la kusikitisha.

0 comments:

aliyekuwa Waziri wa Kilimo zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad AJIUNGA RASMI NA CHAMA CHA WANANCHI (C.U.F) leo

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akimpongeza Mhe. Mansour Yussuf Himid baada ya kuamua kujiunga na chama hicho na kumkabidhi rasmi kadi ya CUF katika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja

Aliyekuwa Mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mansour Yussuf Himid,amejiunga rasmi na chama cha wananchi CUF.

Mhe. Mansour ambaye amewahi kuitumikia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushika nyadhifa mbali mbali ikiwemo ya Waziri wa Kilimo, amechukua uamuzi huo leo kwenye mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja.
Mwanachama mpya wa CUF Mansour Yussuf Himid akizungumza na wanachama wenzake , baada ya kujiunga na chama hicho katika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja

Baada ya kukabidhiwa kadi ya CUF na Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, Mhe. Mansour amesema ameamua kujiunga na CUF baada ya kubaini na kuridhika kuwa chama hicho kimebeba matumaini mapya ya wazanzibari.

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho katika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja

Mhe. Mansour ambaye tayari alishateuliwa na chama hicho kuwa mshauri wa mikakati wa Katibu Mkuu wa CUF, amechukua kadi hiyo akiwa miongoni mwa wanachama wapya 108 waliojiunga na CUF kwenye mkutano huo.

Mapema akizungumza kwenye mkutano huo, Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, amempongeza Mhe. Mansour kwa kuamua kujiunga na chama hicho hadharani, na kukiita kitendo hicho kuwa ni cha kijasiri.

Akizungumzia mafanikio ya chama hicho, Maalim Seif amesema kimepata mafanikio makubwa katika mwaka unaomalizika wa 2014, na kutangaza maazimia mapya ya chama hicho kwa mwaka 2015.

Wanachama wa CUF wakionyesha kuunga mkono uamuzi wa Mansour Yussuf Himid kujiunga rasmi na chama hicho kwenye viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja. 

Ametaja mafanikio yaliyopatikana kuwa ni pamoja na kuendelea kukubalika kwa chama hicho katika pembe zote za Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Kuhusu maazimio ya Chama hicho kwa mwaka 2015, Maalim Seif amesema kimejipanga kuhakikisha kuwa kinashinda kwa asilimia kubwa katika uchaguzi mkuu ujao na kuweza kuongoza serikali ya umoja wa kitaifa.

Hata hivyo amewataka wanachama wasibetweke kutokana na mafanikio yaliyopatikana, bali waongeze nguvu kuhakikisha kuwa malengo ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao yanafikiwa.

Ameongeza kuwa CUF pia kimejipanga kuimarisha uchumi na kujenga Zanzibar mpya itakayokuwa ya matumaini kwa Wazanzibari wote.

Katika hatua nyengine, Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema katika uchaguzi mkuu ujao hatowazuia vijana kutetea haki yao iwapo watadhulumiwa.

“Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 nilifanya kazi kubwa ya kuwazuia vijana wasifanye vurugu pale hoteli ya Bwawani. Mwanzo niliwatuma wasaidizi wangu waende kuwaondosha lakini hakuna aliyesikia hadi nilipokwenda mwenyewe, tena waliondoka kwa shingo upande kabisa. Kwa hivyo uchaguzi mkuu ujao sina namna yoyote ya kuwazuia vijana kutetea haki yao”, alifafanua Maalim Seif.

Kabla ya mkutano huo Maalim Seif alifanya ziara ya kukagua uhai wa chama hicho katika vijiji vya Michamvi, Bwejuu, Jambiani na Paje ambako aliweka mawe ya msingi kwenye matawi ya chama hicho, pamoja na kupandisha bendera kwenye barza ya DAY OUT ya Paje.

Nyalandu atangaza rasmi kugombea Urais kupitia CCM 2015 HABARI KAMILI IPO HAPA

WAZIRI wa maliasili na utalii na mbunge wa jimbo la Singida kaskazini(CCM) ,Lazaro Samwel Nyalandu, ambaye ametangaza rasmi kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.

WAZIRI wa maliasili na utalii na mbunge wa jimbo la Singida kaskazini(CCM) ,Lazaro Samwel Nyalandu,ametangaza rasmi nia ya kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Nyalandu ametangaza nia hiyo leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ilongero Jimbo la Singida kaskazini.
Alisema baada ya kutafakari kwa muda mrefu na kujikagua kwa kina,ameona anao uwezo wa kutosha wa kuweza kupokea kijiti kutoka kwa rais anayemaliza muda wake mwakani kwa mujibu wa katiba.
“Kujikagua huko ni pamoja na kutafakari jinsi alivyoweza kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM katika vipindi vitatu (miaka 15) akiwa mbunge wa jimbo la Singida kaskazini.Katika kipindi hicho cha ubunge,nimeweza kutumia zaidi ya shilingi bilioni mbili katika kufanikisha kuchangia miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo za afya,maji na barabara”,alisema Nyalandu.
Alisema wakati ukifika,Watanzania kutoka sehemu mbalimbali za nchi wakiongozwa na wakazi wengi wa kutoka jimbo la Singida kaskazini,kwenda Dodoma kuchukua fomu za kuwania urais.
“Watanzania waliokwisha onyesha nia ya kuwania urais mwakani,nawaomba sote tuonyeshe kazi tulizozifanya katika kuwahudumia Watanzania,ili waweze kutupima vizuri waweze kujijengea mazingira mazuri ya kuchangua rais atakayewafaa kwa kuwaletea maendeleo endelevu”,alisema.
Nyalandu alisema kuwa anakishukuru Chama Cha Mapinduzi,kwa maandalizi yake mazuri ya kuhakikisha chama kinapata mwanaCCM safi,mwadilifu na mchapa kazi atakayepeperusha bendera ya chama katika kinyang’anyiro cha kuwania urais mwakani.

chanzo: gazeti la mwananchi

0 comments: