Polici Wasema “Panya Road” 36 watiwa mbaroni Dar

polici
Msemaji wa jeshi la polisi SSP Advera Bulimba

Jeshi la polisi nchini linawashikilia vijana 36 wa kundi maarufu Panya Road wanaodaiwa kufanya vurugu na kupora mali za watu na kusababisha taharuki katika jiji la Dar es salaam huku baadhi ya wananchi wakitoa maoni tofauti kuhusiana na tukio hilo.
Akitoa ufafanuzi wa taharuki hiyo msemaji wa jeshi la polisi SSP ADVERA BULIMBA ambaye mbali na kuwatoa hofu wananchi kuwa hali hiyo haitajitokeza tena amesema jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na vikundi vyovyote vinavyotaka kuvuruga amani ya nchi.
Pia amesema kwamba endapo polisi wasingewadhibiti vijana hao mapema tangu wakiwa makaburini baada ya kumzika mwenzao aliyeuawa na wananchi baada ya kuiba hali ingekuwa mbaya zadi.
Kufuatia tukio hilo baadhi ya wananchi wa maeneo ya Magomeni ambako vurugu zilianzia wameelezea namna zilivyoanza hadi kusababisha watu kuanza kukimbia hovyo na wengine kuacha maduka yao wazi na taarifa kusambaa maeneo mengine.
Katika maeneo ya Mwananyamala na Ubungo baadhi ya waliozungumzia sakata hilo wameitaka serikali kuangalia makundi ya vijana na ikiwezekana wapatiwe elimu ya ujasiriamali bure ili waweze kuendesha maisha.
Wananchi wengine wameshauri vijana wasiokuwa na kazi mitaani wapelekwe jeshini wakafundishwe stadi za kazi pamoja na uzalendo ili kuepuka vitendo hivyo.
Taharuki hiyo ilitokea usiku wa tarehe 2 Januari, 2014 chanzo kikiwa ni kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la MOHAMED AYUB kuuawa na wananchi tarehe mosi mwaka huu katika maeneo ya Tandale kwa Mtogole kwa tuhuma za wizi ambapo tarehe 2 maziko yalifanyika na taarifa zilizolifikia jeshi la polisi zilidai kuwa baada ya maziko vijana wenzake walijipanga kufanya fujo ili kulipiza kisasi.

0 comments:

David Moyes Azungumzia Ushindi dhidi Ya Barcelona Na Jina Alilopewa Baada.

moyes
David Moyes ambaye kwa sasa ni kocha wa klabu ya Real Sociedad amesema “Kushinda dhidi ya Barcelona ni jambo ambalo aliwaza kwa muda mrefu bila kujua atalifanikisha vipi na hatakama itawezekana
Kwenye mechi yake ya kwanza dhidi ya Barcelona, Moyes ambaye alikuwa manager wa Manchester United alifanikiwa kushinda kwa bao moja bila.
Moyes alisema “Ushindi huu umemkumbusha wakati alivyokuwa manager wa Everton, wakati anashinda dhidi ya timu kubwa kama Arsenal, Liverpool na Man United ” yMoes alifukuzwa man utd baada ya miezi kumi kwenye nafasi ya Sir Alex Ferguson.
Mtangazaji maarufu wa soka kutoka Span amembatiza David Moyes jina la ‘Braveheart‘.

0 comments:

Mwanasheria Mkuu Mpya wa Serikali Mhe.George Masaju amewaomba Watanzania wajenge imani na serikali yao

sheria
Mwanasheria Mkuu Mpya wa Serikali Mhe. George Masaju amewaomba Watanzania wajenge imani na serikali yao huku akiahidi kushughulikia kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Mheshimiwa Masaju amesema hayo leo muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais Tanzania Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo uliokuwa ukishikiliwa na Jaji Frederick Werema ambaye alijiuzulu kutokana na kashfa ya ufisadi wa Escrow.
Kwa mujibu wa Masaju, maeneo ambayo atayaangalia ni pamoja na suala na kilio cha muda mrefu cha wanachi na wabunge la kutaka uwazi katika mikataba mbalimbali ambayo serikali imekuwa akiisaini kwa niaba ya wananchi.

0 comments: