INGIA HAPA KUSOMA MADHARA YA KUFANYA MAPENZI OFISINI WATOTO AWARUHUSIWI WAKUBWA TU

Yatambue madhara ya kufanya mapenzi ofisini

Kula nanasi kunahitaji nafasi, wengi wamekuwa wakishawishika kufanya mapenzi katika eneo la kazi kutokana na kupendana ama vishawishi mbali mbali kutoka kwa kinadada hususani katika mavazi. Sina maana mbaya ninaposema kina dada kwasababu wengi wao ndio wanaoacha sehemu zao nyeti wazi, kwamfano kuvaa nguo fupi sana na kuvaa vitop vinavyoonyesha sehemu kubwa ya maziwa wazi.

Kwa asilimia miamoja watu wengi wanaofanya mapenzi kwa kuiba katika maeneo kama ya ofisini huwa hawakumbuki kuvaa kinga kutokana na mihemumko mikali na ya haraka kuliko kawaida wanayokuwa nayo kwa wakati huo. Ni vyema kujihadhali ma mihemuko hii kwani madhara yake ni makubwa.

Mihemuko hii huwakumba watu wote hata ambao wako katika ndoa, kutokana na vishawishi vya mwenzake basi anajikuta amezama katika saa za kazi. Tabia hii ikifanyika mara tatu huanza kuwa kama sehemu ya majukumu ya wezi hawa wa mapenzi. Kinadada wanaovaa nguo fupi katika makazi ya watu huenda wakawa wanafanya hivyo kwasababu ya fasheni, wengine kutafuta mvuto kwa wafanyakazi wenzie, lakini kwa wanaume huwa ni kishawishi kimoja kikubwa sana.

Kumbuka unapaswa kuishinda faragha yako na kujitambua kuwa hupaswi kufanya mapenzi na mke wa mtu au mume wa mtu. Unapoona vishawishi kama hivi jaribu kuwa bize na kazi, chukulia poa tu japokuwa wadada wengi huwa na njia mbali mbali za kukufanya ukanasa kirahisi kwa mfano kama mnakumbuka skendo ya Monica Lewinsky na aliyekuwa rais wa Marekani wakati huo walichokifanya ofisini na baadae kuja kuwa ni skendo kubwa sana.

Hasara ya mapenzi hayo ya kiwizi wizi katika masaa ya kazi ni kupata maambukizi ya Ukimwi bila kufahamu kwani utakuwa umemzoea mfanyakazi mwenzio kwa jinsi alivyo smati katika kazi, hivyo hutafikilia kama anawatu wengine nje ya kazi. Pia kuna maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ambayo kwa wanawake hujificha kwa muda kabla ya kuonekana haraka kama wanaume.

0 comments:

WAJUA KUWA WANAUME ‘HANDSOME’, WANAWAKE WAREMBO NI SHIDA KWENYE NDOA SOMA HAPA KWA HABARI KAMILI




Katika hali ya kawaida, kila mtu anapofikiria suala la kutafuta mpenzi kwa mwanaumelazima ataangalia msichana mrembo, mwenye muonekano mzuri huku suala la tabia likiwa halipewi umuhimu sana.Hata kwa wanawake nao huwa wanaangalia wanaume ‘handsome’ ambao hata wakiwa wanatembea pamoja mtaani watavuta macho ya watu na kusifiwa.

Mimi sidhani kama wanaoangalia vigezo hivyo wanakosea hasa kama wanatafuta wapenzi na wachumba watakaotengeneza njia ya kuelekea kwenye ndoa.
Naomba katika hili nieleweke kwamba, suala la muonekano wa mtu si kigezo tosha cha kumruhusu awe sehemu yako katika maisha ya ndoa. Wapo ambao ni ‘handsome’ na warembo lakini kiukweli hawastahili kupewa nafasi ya kuingia nao kwenye ndoa.
Tatizo la wanaume ‘handsome’

Utafiti nilioufanya ambao siyo rasmi unaonesha kwamba, ni wachache sana waliooa wanawake wazuri na wakaishi muda mrefu tena kwa furaha na amani.
Tunachotakiwa kujua katika hili ni kwamba, kuna baadhi ya wanaume ambao wanajijua wanapendwa sana na wanawake kutokana na muonekano wao. Kwamba ni warefu, ni watu wa mazoezi, wana sura nzuri na sifa nyinginezo.
Wenye sifa hizi ni chaguo la wanawake wengi. Kutokana na hilo sasa, wapo ambao wana kaulimbukeni f’lani ka’ kushindwa kutulia na mwanamke mmoja. Wanaweza kuingia kwenye ndoa lakini bado wakashawishika kutembea na wanawake wengine kwa kuahidiwa fedha na vitu vingine.Mbaya zaidi, wanaume wa dizaini hii watakuwa wanajisahau kwamba nyumbani wana wake zao ambao wamewakabidhi mioyo yao na hawatarajii kusalitiwa.Hapo ndipo tatizo litakapoanzia na kumfanya hata mke mwenyewe ajute kuingia kwenye ndoa na mwanaume ‘handsome’. Sisemi kwamba wanaume ‘handsome’ wote ni tatizo kwenye ndoa, la hasha!
Wapo ambao ni watulivu, wasio viruka njia, kwamba wakipenda mmoja wamependa na hata wakishawishiwa na wengine, husimamia hisia zao na kuangalia heshima yao mbele ya jamii.

Tatizo ni kwamba, kuna ambao kwa muonekano huwezi kuwajua lakini ukishakubali ndoa utashangaa usumbufu utakaopata.
Utaona mumeo ana marafiki wengi wa kike na ukimuuliza anasema ni marafiki tu. Mara utamuona anabadilisha magari na ukifuatilia utaambiwa ni magari ya mwanamke f’lani mwenye nazo. Hapo sasa ndipo utajua kwamba kumbe hujapenda peke yako, wapo wengine waliopenda na wakapewa nafasi kutokana na ushawishi wao.

Ndiyo maana nasema kuolewa na mwanaume ‘handsome’ tena ambaye ni limbukeni, utapata tabu sana. Utaambulia ile sifa tu ya kwamba umeolewa na mwanaume mzuri lakini kumbe hafai kuitwa mume!
Wasichana warembo nao!

Jaribu kuchunguza utabaini kuwa, asilimia kubwa ya wanaume wanaoteswa na ndoa zao, wameoa wasichana warembo lakini wasiojua thamani ya ndoa. Watakuwa wanaona sifa kuolewa lakini bado hawajui namna ya kuzitunza ndoa zao.
Watakuwa warahisi kushawishiwa na wanaume wakware na wakati mwingine wakiona wanatongozwa sana kutokana na uzuri wao, wanavimba vichwa.Wanakuwa si watulivu kwenye ndoa zao, siyo watiifu kwa waume zao na wanafanya hivyo wakiamini kwamba hata wakiachika, watapata wanaume wengine wa kuwaoa.
Ndiyo maana huwa nasema mara kwa mara kwamba, ukitaka kuoa ni lazima uangalie mwanamke mzuri unayemuona wewe. Lakini usiishie hapo, angalia na tabia zake ili usije ukaingia kwa mtu ambaye hawezi kukupa furaha ya ndoa uliyotarajia.
Katika hili naomba nihitimishe kwa kusema kwamba, ukitaka kuingia kwenye ndoa epuka sana kuangalia muonekano wa mtu. Tukijichanganya macho yatatuingiza mkenge!Unaweza kumuona msichana mzuri, mwenye figa na sura ya kuvutia au mwanaume ‘handsome’, mwenye sifa zote za kupendwa na kila mwanamke lakini kumbe linapokuja suala la ndoa, hamna kitu!  
Ni suala la wewe kuwa makini sana hasa pale unapotafuta mpenzi au mchumba! Achana na ile tabia ya kutafuta sifa kwamba eti ‘kapo’ yenu inavutia, swali ni je, anaiheshimu ndoa na siyo macho juujuu? 

0 comments:

OHOO! MTUMISHI WA MUNGU ANASWA NA MKE WA MTU INGIA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI


Mtumishi Fredrick Kishindo ‘Badoo’ akijistili kwa kanga baada ya fumanizi hilo.

Ohoo, ama kweli dunia imekwisha! Mtumishi wa Mungu (Muinjilisti) ambaye kipindi chake cha dini kinarushwa katika kituo kimoja maarufu cha televisheni Bongo (Jina tunalihifadhi) aliyefahamika kwa jina la Fredrick Kishindo ‘Badoo’ hivi karibuni alipata aibu ya kufungulia mwaka 2015 baada ya kunaswa na mke wa mtu chumbani.
Ilikuwaje?
Awali chanzo cha habari kilichoomba hifadhi ya jina lake kilieleza kuwa, Januari 11, mwaka huu Muinjilisti huyo anayesifika kwa kuhubiri watu waache dhambi alionekana akinyata kuingia kwenye nyumba ya mke wa mtu huyo iliyopo Sinza jijini Dar huku kukiwa na taarifa kuwa, mume wa mwanamke huyo alikuwa safarini.
Wifi mtu atonywa
Ikaelezwa kuwa, kufuatia mazingira hayo wifi wa mwanamke huyo alitonywa juu ya taarifa za Badoo kuingia kwenye nyumba ya kaka yake, maelezo yaliyomshitua hivyo kulazimika kuelekea eneo la tukio.
Baada ya wifi mtu huyo kufika nyumbani kwa kaka yake na kuhakikishiwa kuwa Badoo yuko ndani, aliuliza namna ya kuwapata mapaparazi ambapo mmoja wa majirani alimpatia namba ya simu, akawapigia.
...Akivaa shati huku kitendea kazi chake(Biblia) kikiwa nyuma yake.
Polisi washirikishwa
Katika kuhakikisha usalama katika eneo hilo, wifi huyo pia aliwasimamisha polisi waliokuwa doria na kuwatonya juu ya uzinzi unaofanyika nyumbani kwa kaka yake na kwa kuwa kazi ya askari ni kulinda raia na mali zao, walitoa ushirikiano.
Muinjilisti, mke wa mtu live
Polisi waliongozwa na wifi mtu huyo hadi kwenye chumba ambacho madhambi yalikuwa yakitendeka, walipoingia walikuta mke wa mtu na mtumishi huyo wa Mungu wakiwa kama walivyozaliwa.
Aibu iliyoje!
Baada ya kuona ‘picha imeungua’, mtumishi huyo alisikika akisema kuwa amepata aibu ambayo hakuitarajia huku akiomba asipigwe picha wala kufanyiwa kitendo kibaya bali apewe nafasi ya kujitetea.
Aidha mke wa mtu aliyenaswa akimsaliti mumewe alionekana kutahayari na aliishiwa nguvu zaidi alipomuona wifi yake aliyekuwa amefura ile mbaya.
Mchungaji huyo akijitetea baada ya fumanizi hilo.
Utetezi wa mtumishi wa Mungu
Kufuatia kunaswa huko, Badoo alijitetea kwa kujichanganya, awali alisema aliitwa na mwanamke huyo kwa ajili ya kuongea mambo ya biashara na kwamba eti walivua nguo kutokana na hali ya joto iliyokwemo chumbani humo.
Kana kwamba alihisi kajichanganya, Muinjilisti huyo aligeuza utetezi na kusema aliingia majaribuni baada ya kushawishiwa na ibilisi kisha mwanamke huyo hakumwambia kuwa ana mume.
sikie utetezi wake
“Jamani naomba mnisamehe, si kosa langu bali ibilisi ndiye aliyenishawishi na huyu mwanamke hakuniambia kama ana mume. Hapa aliniita kwa ajili ya biashara flani.
“paparazi nawajueni lakini niko chini ya miguu yenu, naomba msiitoe habari hii mtandaoni ntawapa chochote.
Mke wa mtu akijifunika kwa aibu.

Licha ya utetezi wake huo, mapaparazi walisimamia weledi wa kazi yao na kumweleza kuwa, rushwa kwao ni mwiko, mpaka
 wanaondoka eneo la tukio, mke wa mtu huyo alikuwa akiendelea kumuomba msamaha wifi yake huku Muinjilisti naye akijaribu kutuliza mambo yasifike mbali akidai kuwa, mke wake, ndugu na marafiki wakijua ataaibika.
Ni fundisho
Paparazi limefikia hatua ya kuiandika habari hii ili iwe fundisho kwa watu wengine ambao wamekuwa na tabia ya kuvuruga ndoa za watu ikiwa ni pamoja na kufanya mambo mengine ambayo ni kinyume na maadili. 

0 comments:

Mahakama yatoa siku saba hati ya Halima Mdee kurekebishwa


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa siku saba kwa upande wa Jamhuri kufanya marekebisho ya hati ya mashitaka katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee (35) na wenzake wanane.
 
Hakimu Mkazi Janeth Kaluyenda alitoa amri hiyo jana wakati akitoa uamuzi wa ombi la washitakiwa hao kufutiwa mashitaka. Akitoa uamuzi huo, Hakimu Kaluyenda alisema amesikiliza hoja za pande zote mbili na kupitia kesi mbalimbali hivyo aliamuru hati ya mashitaka ifanyiwe marekebisho ndani ya siku saba.
 
Katika ombi lao washitakiwa kupitia kwa Wakili wao Peter Kibatala waliiomba Mahakama iwafutie mashitaka ya kufanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kutembea kwenda kwenye Ofisi ya Rais kwa kuwa lina mapungufu kisheria.
 
Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka, wakidaiwa Oktoba 4, 2014 katika Mtaa wa Ufipa, bila kuwa na uhalali walikiuka amri halali ya kutawanyika iliyotolewa na Mrakibu wa Polisi (SP), Emmanuel Tillf kwa niaba ya Jeshi la Polisi

0 comments:

FASHENI: HIZI CHUPI (G-STRING) MPYA ZA KIKE NI SHIDAA......[ KWA WANAWAKE TU..]

Kama kawaida tasnia ya FASHENI inabadirika kila siku...Lakini huu ujio wa hizi  CHUPI zinazoitwaShibue Strapless Panty ni Nouma......

Hizi wameziita ni chupi za miujiza, kwani zimetengenegwa kwa MATIRIO ambayo huweza kukabiliana na  mabadiliko ya  MAKAO MAKUU katika hali yoyote ile.....hehehee....

hivyo kumfanya mwanamke awe COMFOTABO  (Kama unavyojua tena makao makuu kuna mengi pale)

Tofauti na chupi zingine aina ya G-String chupi hizi huvaliwa kuanzia juu ya Uke na mpaka kwenye mwisho wa uti wamgongo...Jionee picha  hapa.. Then niambie kwa kucomment hapa chini unaona vipi.. 


Uvaaji wake sasa
nishiidaah....

0 comments:

VIDEO: JIFUNZE JINSI YA KUFANYA MAPENZI KWA USAHIHI KATIKA VIDEO HII INGIA HAPA


0 comments:

MAITI YASAFIRISHWA JUU YA KERIA INGIA HAPA

Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwekwa vizuri kwenye keria ya gari tayari kwa safari.

DUNIANI kuna matukio! Tofauti na utaratibu uliozoeleka, katika hali ya kushangaza, wanandugu wamelazimika kusafirisha maiti juu ya keria ya basi kutoka Arusha hadi Lushoto, Tanga kutokana na ukata.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo chanzo kilieleza kuwa, wanandugu hao ambao hawakuwa tayari kuanika majina yao, walifikia hatua hiyo ili waweze kuenea kwenye basi moja aina ya Toyota-Coaster kwenda Lushoto, mkoani Tanga.
Waombolezaji wakiupandisha mwili wa marehemu (ndani ya jeneza) juu ya gari.

“Waliona kama wangeweka maiti ndani ya gari, wangelazimika kutoa siti mbili hivyo wasingetosha, baadhi ya ndugu walishauri kwamba mwili wa marehemu uwekwe juu ya keria ili waombolezaji waweze kuenea,” kilisema chanzo.
Chanzo hicho kilizidi kushusha data kuwa, kabla ya wanandugu kukubaliana kusafirisha juu ya keria mwili huo, uliibuka ubishani mkubwa kwani kuna baadhi waliafiki kitendo hicho lakini wengine hawakuafiki.“Kuna ambao walikataa na kusema si jambo la busara kuiweka maiti juu ya keria lakini mwisho wa siku walizidiwa kwa hoja na wale walioshauri iwekwe juu kwani tatizo lilikuwa kwenye fedha za kukodi gari jingine.

“Walishajikusanya kusanya hadi dakika za mwisho, fedha walizopata zilitosha kukodi gari moja hivyo hawakuwa na jinsi japo ambao hawakuafiki, walihofia kuwa huenda wasifike salama huku wengine wakichungulia pembeni kila wakati wakihofu huenda jeneza linaweza kuanguka,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo pamoja na kutofautiana huko kwa wanandugu, walifanikiwa kusafiri salama hadi Lushoto na kufanikiwa kumpumzisha mpendwa wao.

0 comments:

Dk Slaa kupanda ‘kizimbani’ leo SOMA HAPA


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibroad Slaa, leo anatarajiwa kupanda kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Hai kutoa ushahidi katika kesi ya jinai inayomkabili kijana aliyejifanya Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samatta.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Hai, Dennis Mpelembwa alisema jana kuwa Dk Slaa amethibitisha kuitikia wito huo wa Mahakama.
Katika ushahidi uliotolewa mahakamani, Dk Slaa akiwa Mtendaji Mkuu wa Chadema, ndiye anayedaiwa kushughulikia suala la mshtakiwa kutaka kuwatapeli viongozi wa Chadema.
Tayari Jaji Samatta na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wamekwishatoa ushahidi wao katika kesi hiyo inayoendeshwa na mawakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Katika ushahidi wake, Jaji Samatta alikana kumfahamu mshtakiwa Abeid Adam Abeid (22) na kwamba namba ya simu iliyotumiwa kujitambulisha kwa Dk Slaa na Lema kuwa ni Jaji Samatta siyo yake.
Kwa upande wake, Lema alidai mshtakiwa huyo alimtumia meseji mbalimbali akijitambulisha kwake kuwa ni Jaji Samatta na kwamba angemsaidia katika rufaa yake ya kuvuliwa ubunge ya mwaka 2012.
Upande wa mashtaka, ukiongozwa na Wakili wa Takukuru, Susan Kimaro ulidai mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya Aprili na Mei 2012. Mtuhumiwa alikana mashtaka hayo na leo upande wa mashtaka unatarajiwa kufunga ushahidi wao baada ya Dk Slaa na shahidi mwingine ambaye hajatajwa, kutoa ushahidi wao.

0 comments:

Baada ya anna tibaijuka kuchafuka kisiasa ona halima mdee alivyomponda




























0 comments:

Kingunge: Waliojitokeza kuwania urais CCM hawana sifa


Mwanasiasa mkongwe nchini Mzee Kingunge Ngombare Mwiru akizungumza na wanahabari

Harakati za kuwania urais ndani ya CCM zimeingia katika hatua mpya baada ya mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale - Mwiru kuibuka na kudai kuwa wote waliojitokeza kuwania nafasi hiyo hawana sifa kwa kuwa wanatumia fedha kutaka kuingia Ikulu.
Kauli ya mwanasiasa huyo ambayo imekuja siku moja kabla ya Kamati Kuu ya CCM kukutana leo mjini Unguja na moja ya ajenda ikitajwa kuwa suala la maadili, inaweza kuwa mwiba mchungu kwa wanasiasa hao ambao wanaongezeka kila kukicha.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kingunge alisema: “Kuna suala la kukosa uadilifu, kuna suala la matumizi ya pesa na nikwambie ukweli, hao wanaotangaza urais wote wanatumia pesa, wanatumia faulo mbalimbali na wananchi wanajua.”
Kwa miezi kadhaa sasa, baadhi ya makada wa CCM wamekuwa wakitajwa kufanya harakati kichinichini na wengine kushiriki shughuli za wazi zinazoashiria kuwa wanataka kuwania nafasi hiyo ya juu. Hadi sasa makada wanne tayari wameweka wazi nia yao hiyo.
Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba kwa nyakati tofauti walitoa kauli zinazowashutumu makada wengine wa chama hicho kwa matumizi makubwa ya fedha katika kushawishi uungwaji mkono.
Hata hivyo, kauli za wanasiasa hao zimedaiwa kuwa ni fitina za kisiasa kwa kuwa wagombea wote wanatoa fedha, bali wanazidiana viwango tu.
Mbali na Makamba na Membe, wanaCCM wengine waliotangaza au kutajwa kuwania urais ni Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Wengine ni mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
Kauli ya Kingunge aliyoitoa kupitia Televisheni ya ITV, imekuja wakati wanasiasa sita miongoni mwa hao wanaotajwa wakikaribia kumaliza miezi 12 ya uangalizi kutokana na onyo kali dhidi yao lililotolewa na Kamati Kuu ya CCM Februari 18, mwaka jana baada ya kuwatia hatiani kwa makosa ya “kuanza kampeni mapema na kufanya mambo ambayo ni kinyume na maadili ya chama na ya jamii.”
Wanaotumikia adhabu hiyo ni Lowassa, Sumaye, Njeleja, Makamba, Wasira na Membe.
Akisisitiza hoja yake hiyo bila kutaja majina, Kingunge alisema makada hao wamekuwa wakitumia fedha nyingi kujitangaza na kutengeneza ushawishi wa kukubalika kwa wananchi jambo ambalo ni kinyume na maadili ya uongozi.
Kingunge alisema mwanasiasa yeyote anayehitaji uongozi hapaswi kutumia fedha kushawishi wananchi wamchague.

0 comments: