MSHTUKO! ISLAMIC STATE (IS) WAFUNGUA KAMBI YA MAFUNZO AFRIKA...NI LIBYA!

Wapiganaji wa Islamic State katika jimbo la Anbar,Syria Marchi 2014
Wapiganaji wa kundi la Islamic State wafungua kambi za mafunzo LibyaWapiganaji wa kundi la Islamic State wameanzisha kambi za mafunzo mashariki mwa Libya, amesema mkuu wa kamandi ya Marekani ya masuala ya Afrika. 
Wapiganaji wa Kikurd wakiwa katika mafunzo ya kijeshi kukabiliana na wapiganaji wa Islamic State Septemba 2014 nchini Iraq.Jenerali David Rodriguez amesema kuna mamia ya wapiganaji wa IS wanaopata mafunzo ya kijeshi kwenye kambi zake nchini Libya. 

Amesema kambi hizo zipo katika hatua za mwanzo kabisa, lakini Marekani imekuwa ikiyafuatilia kwa karibu kuona zinavyoendelezwa.

Libya imekuwa katika mgogoro tangu kuangushwa kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011, ambapo makabila mbalimbali, wanamgambo na makundi ya kisiasa, wote wakipigania madaraka.

Makundi mbalimbali ya Kiislam yanawania madaraka mashariki mwa Libya, hukubaadhi yakitangaza kuwa na ushirikiano la kundi la Islamic State, IS. 
Wapiganaji kutoka kikundi cha IS wakipakia mabaki ya kile kinachosemekana kuwa mabaki ya ndege ya Marekani isiyotumia abiria baada ya kukonga katika mnara wa mawasiliano huko Raqqa Septemba 23,2014Akizungumza mjini Washington Jumatano, Jenerali Rodriguez bado haijafahamika ukaribu uliopo kati ya watu wanaopata mafunzo hayo na kundi la IS."Kikubwa ni watu wanaokuja kupata mafunzo na msaada wa vifaa kwa ajili ya kambi za mafunzo kwa sasa," amesema. "kwa sasa mafunzo hayo bado ni ya hatua ya chini sana na tunafuatilia kuona namna hali inavyokwenda." 
Watoto wakikimbia kando ya mlima hukumoshi ukisambaa angani kufuatia mapigano katika eneo hilo la mji wa Kobani, wakati majeshi yanayoongozwa na Marekani kushambulia wapiganaji wa Islamic StateWaandishi wa habari wanasema katika kipindi cha mapinduzi yaliyomwondoa madarakani Gaddafi, wapiganaji wengi waasi waliondoka nchini humo kwenda kujiunga na vikundi vya wapiganaji nchini Syria na baadhi yao wanaaminika kuwa wamerejea nyumbani(Libya).
Serikali iliyochaguliwa imepoteza miji mikuu mitatu ya Libya huku kukiwa na mgogoro wa kisiasa.

Benghazi, mji wa pili kwa ukubwa nchini Libya, uko mikononi mwa wapiganaji wa Kiislam, na bunge linalotambuliwa kimataifa kwa sasa linaendesha vikao vyake katika mji ulioko pwani ya Tobruk mashariki mwa nchi hiyo

Marekani imekuwa ikiongoza washirika wa kimataifa kufanya mashambulio ya anga dhidi ya IS nchini Iraq na Syria katika miezi ya karibuni.

0 comments:

BAADA YA KUPONDWA NA DIAMOND KUWA "HATA ALI SIMUONI" ALIKIBA AMEKWENDA KUSHOOT VIDEO YA WIMBO WAKE ‘MWANA’ AFRIKA KUSINI.. ILI ALE SAHANI MOJA NA DIAMOND

10809648_391264047706717_1301671596_n

Alikiba amesafiri hadi jijini Cape Town, Afrika Kusini kwenda kushoot video mpya.

Inavyoonekana staa huyo amekwenda kushoot video ya wimbo wake ‘Mwana’ uliotoka miezi kadhaa iliyopita.
10809551_1580625418833092_1220378353_n
Kiba ameshare picha kadhaa kwenye Instagram akiwa location huku moja anaonekana akiwa na dancers wa kike.
10847811_873743942649078_2506836612100726369_n


0 comments:

JAJI MKUU ATAKA UWAZI MAHAKAMANI....ASEMA WANAANGALIA UWEZEKANO WA KESI ZENYE MVUTO KUWA LAIVU KWENYE TV


MAHAKAMA inaangalia uwezekano wa kuruhusu vyombo vya habari kurekodi picha na sauti kuwezesha vituo vya radio na televisheni kuripoti habari za mahakama wakati kesi zinaendelea.
 
Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman alisema jana mahakama inajifunza kutoka kwa nchi zinazoruhusu vituo vya redio na televisheni kurekodi na kuripoti habari wakati kesi zinaendelea.
 
Alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jana wakati wa mkutano baina ya Baraza la Vyombo vya Habari na Mahakama uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 
Alisema utaratibu huo utaanza kwa kuripoti kesi za madai zenye mvuto kwa jamii na kwamba utaratibu mzima unapaswa kufanyika kwa umakini mkubwa baada ya mahakama na vyombo vya habari kukaa pamoja na kujadiliana juu ya maadili, uhuru na mipaka ya mhimili wa mahakama na vyombo vya habari ili kuondoa migongano katika kuandika na kuripoti habari za mahakama kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
 
Hivi sasa waandishi wa habari hawaruhusiwi kupiga picha za video wala kurekodi sauti wakati kesi zikiendelea.
 
Badala yake, wanaruhusiwa kuandika habari hizo kisha kuripoti kile walichoandika bila kuonesha mwenendo mzima wa kesi kwa kutumia sauti na picha za video.
 
Jaji Othman alifafanua kuwa ni lazima mahakama na vyombo vya habari kuweka utaratibu wa kuripoti kesi kwa kurusha sauti na picha bila kuvuruga mwenendo wa kesi kwa kukiuka haki hasa za washitakiwa, waathirika na mashahidi kwa kuwa wote wanahitaji haki sawa katika kupata ulinzi na hifadhi kulinda utu wao.
 
“Mfano sio haki kuwaonesha hadharani waathirika wa kesi ya ubakaji, pia mshitakiwa yeyote hawezi kuitwa mwizi au muuaji hadi mwisho wa kesi ambapo mahakama inazingatia ushahidi na kutoa hukumu,” alisema.
 
Aliendelea kusema, “Ukitangaza kuwa mtu ni mwizi kabla ya hukumu, ni kumkosea haki kisheria hivyo ni lazima tuangalie yote hayo kabla ya kuruhusu utaratibu wa kunakili sauti na picha wakati kesi zinaendelea.”
 
Jaji alitoa maelezo hayo wakati wa kuzungumzia mapendekezo yaliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga ambaye alisema ili kuboresha uhusiano wa vyombo vya habari na mahakama, mahakama inapaswa kuwa na msemaji.
 
Mukajanga alipendekeza pia mahakama kuandaa taarifa kwa kutumia sauti na picha za video kuhusu mwenendo wa kesi, kutoa mwongozo wa kutumia simu za viganjani na vifaa vingine vya mawasiliano kwa njia ya digitali.
 

Baraza hilo la kihistoria kati ya mhimili wa Mahakama na vyombo vya habari, limeazimia kuimarisha ushirikiano na kufanya kazi kwa pamoja kwa kuheshimu uhuru na mipaka ya kila mmoja na kuzingatia kuwa wote wanafanya kazi ya kutetea haki za wananchi na wote wamekuwa kimbilio la wanyonge.

0 comments:

UKAWA YAVUNJIKA VIPANDE VIPANDE MKOANI ARUSHA BAADA YA VYAMA VINAVYOUNDA UMOJA HUO KUSHINDWA KUACHIANA NAFASI ZA UONGOZI


 
Vyama vinavyounda Ukawa ni Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, lakini vyote vimesimamisha wagombea katika mitaa ndani ya mkoa wa Arusha, kinyume na makubaliano yaliyosainiwa na viongozi wa kitaifa hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
 
Kitendo hicho kimefanya CCM kutwaa kiulaini uongozi kwenye vijiji 183 kati ya 406.
 
Aidha chama hicho kimeshinda kwa rufaa katika mitaa sita kati ya 155 ambapo Mkoa mzima wa Arusha una vijiji 406 na mitaa 155.
 
 Chadema watetea.
Akizungumzia hali hiyo jana mjini , Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema makubaliano ya viongozi wa juu ya Ukawa ya kuweka mgombea anayekubalika iko pale pale.
 
Alikiri vyama vinavyounda Ukawa kusimamisha wagombea kila kimoja kivyake mkoani Arusha, lakini akasisitiza kuwa, hiyo haina maana kwamba makubaliano yao ya kushirikiana yamevunjwa.
 
Alisema wamefanya hivyo kwa sababu maalumu ambayo wao wanaijua, lakini umoja wao uko pale pale na makubaliano yanaheshimika kwa asilimia kubwa.
 
Mwenyekiti huyo aliwataka wanachama wa Ukawa kutokuwa na wasiwasi, kwani wamefanya hivyo kwa kuangalia ni namna gani watashirikiana katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
 
CCM yatamba
Akizungumza jana ofisini kwake, Katibu wa CCM mkoa wa Arusha, Alphonce Kinamhala alisema ushindi huo unatokana na utekelezaji mzuri wa ilani ya chama ambayo imekuna wananchi wengi mkoani humo.
 
Alisema kwa sasa CCM ina kazi ndogo ya kupambana na vijiji 378 vilivyosalia na kwamba hali inakwenda vizuri na wana uhakika wa kushinda katika vijiji vilivyosalia katika uchaguzi huo wa Desemba 14, mwaka huu.
 
Katibu huyo alisema mbali ya ushindi wa vijiji hivyo, pia CCM imeshinda vitongoji 688 sawa na asilimia 46 kati ya vitongoji 1,483 na kilichobakiwa ni kushindana katika vitongoji 795 pekee.
 
Alisema baada ya kuzindua kampeni zake mwishoni mwa wiki iliyopita, hali inaendelea vizuri na hakuna malalamiko ya kuwapo vurugu kwenye mikutano ya kampeni wilaya zote.
 
Kinamhala amevitaka vyama vya upinzani kufanya kampeni za kistaarabu zitakazotoa nafasi kwa wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura.
 
Alisema wajibu wa kupiga kura ni haki ya msingi ya kila mtanzania mwenye sifa na endapo kampeni zitakuwa na vurugu, wengi watashindwa kujitokeza kupiga kura siku hiyo.
 
“Naomba kutoa mwito kuwa ni jukumu letu sote kufanya kampeni za kistaarabu na sera nzuri zenye ujumbe kwa wananchi ambazo zitawahamashisha wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowaona wanafaa kuwaongoza,’’ alisema.
 
Wakati hayo yakijiri mkoani Arusha, hali hiyo imejitokeza pia mkoani Morogoro katika Kata ya Chamwino, ambako iliripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari kwamba CUF imesimamisha wagombea katika mitaa yote 15 baada ya kushindwa kuafikiana kuachiana mitaa na Chadema.
 
Ilidaiwa na CUF kwamba viongozi wa Chadema walishindwa kuwaachia mitaa mitano, ambayo CUF ina nguvu na kukubalika na wananchi.
 
Ilielezwa kwamba Chadema ilishauriwa kuchukua mitaa 10, lakini ikashindwa kuheshimu makubaliano kwa kusimamisha wagombea mitaa yote.
 
Mmoja wa viongozi wa CUF Kata ya Chamwino, Omari Mwansenga, alikaririwa akisema,“wenzetu wa Chadema wameshindwa kuheshimu makubaliano ya kuachiana mitaa, CUF ina mitaa mitano yenye wafuasi na kukubalika na itasimamisha wagombea.”
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa CUF, Wilaya ya Morogoro Mjini, Abdallah Mambo, alikiri kuwapo migongano hiyo katika umoja huo ingawa alisema suala hilo liko chini ya maelekezo ya viongozi wa vyama washirika ngazi ya wilaya.
 
Makubaliano
Kutoafikiana kwa vyama hivyo, kunakwenda kinyume na makubaliano yaliyosainiwa na viongozi wakuu wa vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD vinavyounda Ukawa.
 
Novemba 4 mwaka huu, vyama vya siasa vinavyounda Ukawa vilisaini mwongozo wa ushirikiano katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji pamoja na uchaguzi mkuu, mwakani ambapo vilikubaliana kuachiana nafasi katika kila hatua ya uchaguzi.
 
Umoja huo uliweka wazi vigezo ambavyo walishauriana vitumiwe katika kumpata mgombea mmoja katika nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo.
 
Navyo ni kuwa na mgombea anayekubalika zaidi, chama kilichoshinda uchaguzi uliopita, idadi ya wanachama, maridhiano au mwafaka wa kura ya maoni na suluhishi la mvutano wa mgombea.
 
Hii ina maana kwamba, kuanzia katika uchaguzi wa wiki ijayo wa serikali za mitaa au  ule wa mwaka ujao kwa nafasi za ubunge, udiwani na hata kwa nafasi ya mgombea wa Urais, mgombea atakuwa mmoja tu kutoka kambi ya ukawa, lakini vyama vingine vitalazimika kumuunga mkono mgombea huyo.
 
Waliosaini makubaliano hayo ni Mwenyekiti wa Umoja huo, Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Dk Willibrod Slaa (Chadema) na James Mbatia (NCCR Mageuzi).
 
Emmanuel Makaidi ambaye ni Mwenyekiti wa NLD hakuwepo, ikielezwa alikuwa na udhuru. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hakuwepo.

0 comments: