IYOBO: MIMBA YA ‘BABY’ NI FARAJA KWANGU

Moses Iyobo akiwa na mpenziwe ambaye ni staa wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel.
Na Imelda Mtema/Amani
Dansa mahiri wa staa wa muziki Bongo na nje ya nchi, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aitwaye Moses Iyobo, amefunguka kuwa hakuna kitu kinachompa faraja kubwa kama mimba ya mpenzi wake ambaye ni staa wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel.
Akizungumza na Amani hivi karibuni, Iyobo ambaye nyuma kidogo alipost picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kutoa pongezi kwa mpenzi wake huyo kwa kumbebea ujauzito, alisema kuwa hakuna kitu ambacho anaona fahari kama hicho.
“ Mimi tu nikiwaza mtu ambaye ninampenda kwa dhati ana mimba yangu napata faraja kubwa sana hivyo kila siku namuomba Mungu ajifungue salama na ampitishe katika majaribu mazito,” alisema Iyobo.

0 comments: