PAC yaibua ufisadi wa bilioni 9/- katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere JNIA

  Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),Zitto Kabwe.
Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) imeibua ufisadi uliopelekea upotevu wa zaidi ya Shilingi bilioni tisa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam.
Akiwasilisha taarifa ya mwaka ya Kamati hiyo kuhusu hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2013, Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alisema kuwa ufisadi huo umetokea kwenye mradi wa ujenzi wa Jengo la watu mashuhuri kwenye uwanja huo. 
Zitto alisema kuwa ukaguzi uliofanyika unadhihirisha kwamba harama halisi za ujenzi wa jengo la watu mashuhuri kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere zina mkanganyiko.
Alisema katika ukaguzi ulofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG), mkaguzi huyo alishindwa upata nyaraka wala vilelezo vyote vilivyomo kwenye majalada ya ofisi za Mamlaka ya vya Ndege (TAA) na yale ya kiwanja cha JNIA ikiwemo mkataba kwa ajili ya kuonyesha gharama halisi za ujenzi huo. 
Alisema kuwa kilichopatikana ni ‘offer for Grant for VIP Launge’ yenye thamani ya fedha za kitanzania shilingi bilioni 5.3. 
Zitto alisema kuwa ili thamani ya ujenzi wa jengo hilo, CAG aliagiza Wizara ya Uchukuzi iwasiliane na mthathimini Mkuu wa Majengo ya Serikali ili afanye thathmini ya thamani ya jengo hilo.
“Kwa mujibu wa taarifa ya Mthamini Mkuu wa Majengo ya Serikali hadi kufikia mwezi Mei, 2014 gharama za ujenzi wa jingo hilo zilikuwa ni Shilingi bilioni tatu na mchango wa Serikali kwa shughuli zilizohusu ujenzi wa jengo hilo ulikuwa ni Shilingi milioni 869.4 tu. 
Alisema kuwa hata hivyo katika mikutano mbalimbali ya bunge kati ya mwaka 2011 na 2012, Serikali ilitoa tamko kuwa jengo la watu mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam kuwa ni jumla ya shilingi bilioni 12!  
 
Zitto alisema kuwa tamko hilo la Serikali ni tofauti ya shilingi bilioni tisa zaidi ya kiwango cha Mthamini Mkuu wa Serikali, hali ambayo inaonyesha kuna matumizi yasiyo ya kawaida ya fedha hizo.

0 comments: