WAFUASI 29 WA CUF WAACHIWA KWA DHAMANA
WAFUASI
29 kati ya 30 waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es
Salaam wameachiwa leo baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Wafuasi
hao walikamatwa majuzi huko Mtoni Mtongani, Dar wakati Mwenyekiti wa
Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba akielekea Mbagala
kuwataka wananchi watawanyike baada ya maandamano ya chama hicho
kuzuiliwa na jeshi la polisi.
Wafuasi
hao 29 wameachiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar baada ya
kila mmoja wao kutimiza masharti ya dhamana kwa kutoa kiasi cha shilingi
100,000 pamoja na barua ya mdhamini mmoja ambaye hana hatia.
Mmoja wa watuhumiwa alikuwa bado mikononi mwa polisi kwa kutokamilisha taratibu za dhamana hiyo akiendelea kumsubiri mdhamini wake aliyechelewesha barua ya udhamini.
Mmoja wa watuhumiwa alikuwa bado mikononi mwa polisi kwa kutokamilisha taratibu za dhamana hiyo akiendelea kumsubiri mdhamini wake aliyechelewesha barua ya udhamini.
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo amesema kesi yao itatajwa tena Februari 12, 2015.
0 comments: