Aidha,
ameweka wazi kile anachoamini anashutumiwa na kubezwa na watu kuhusu
uteuzi huo na kusema wanaofanya hivyo, wanafahamu kwamba masuala yao
kadhaa ndani ya wilaya hiyo yanayokwenda kinyume na taratibu,
hayatafanikiwa.
Akiendelea
kujibu wanaoshutumu uteuzi wake kupitia mitandao ya kijamii na vyombo
vya habari, alisema kwa sasa hawezi kutoa ahadi ni nini atafanya
isipokuwa, anasubiri kuingia ofisini.
Akihojiwa
katika kipindi cha asubuhi cha Redio ya Clouds, alisema pia
anamsikiliza Rais atakachomwambia afanye kwa kuwa yeye ni mwakilishi
wake wilayani humo.
Akizungumzia
kuhusu taarifa za kupata nafasi hiyo kuwa gumzo katika jiji kuliko
wakuu wengine wa wilaya, alisema inaonesha ni kwa jinsi gani watu
wanatambua utendaji wake.
Alisema
alipata taarifa za uteuzi huo wakati akitoa mada katika kikao cha kazi
cha Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na kushangaa watu
wakipeana taarifa.
“Kuna
watu wanabeza uteuzi wangu kwa kuonekana nimepewa wilaya kubwa. Nataka
kuwaambia wasubiri waone tu,” alisema na kutaka Watanzania kuacha tabia
ya kumjadili mtu au jambo bila kufahamu vizuri.
Alisisitiza
kuwa Watanzania wamekuwa na tabia ya kushabikia jambo wasilolijua au
mtu wasiyemjua kwa kufuata mkumbo; jambo ambalo siyo zuri ni vyema
kufahamu kwanza ndipo uweze kusema.
Akizungumzia
baadhi ya vyombo vya habari vilivyotoa taarifa za uteuzi wake kwa
kumdhihaki, alisema wamefanya hivyo kwa maslahi yao ya kuuza.
Pia
alielezea uteuzi wake umekuwa gumzo, kutokana na uwezo wake wa kazi
katika UVCCM pamoja na uwezo wake kwenye Bunge Maalumu la Katiba.
Uteuzi
wa Makonda ambao umefanywa na Rais Kikwete, unaonesha kuwashitua wengi;
hali ambayo imefanya watu wengi kumbeza hasa kupitia mitandao ya
kijamii.
Baadhi
ya wanaobeza, wanadai kwamba Makonda hana sifa ya kuongoza wilaya kubwa
kama Kinondoni, ambayo ina changamoto na migogoro mingi ya ardhi.
Makonda
ambaye ni Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa UVCCM, jina lake
limekuwa kubwa hivi karibuni baada ya kutuhumiwa kushiriki kuvuruga
mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, tuhuma alizokanusha.
Pia,
kujitokeza kwake hadharani kumpinga mmoja wa watu wanaotajwa kuwania
urais, kuliongeza jina hilo kuwa maarufu. Maisha ya Makonda pia ambaye
baada ya kushindwa Umakamu Mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM, alitoa shutuma
kuhusu uchaguzi huo na baadaye alirejeshwa ndani ya umoja huo kwa kupewa
nafasi anayoshikilia sasa ya ukatibu wa uchipukizi na uhamasishaji.
0 comments: