KIKONGWE ALIYEPIGWA MAWE KWA MADAI YA USHIRIKINA HALI MBAYA

 KIKONGWE Hilda Johnfan Pili (79) aliyepigwa mawe kutokana na imani za kishirikina katika Kijiji cha Kilagano, Peramiho mkoani Ruvuma hivi karibuni, bado hali yake ni mbaya kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata.

Kikongwe akiwa hoi baada ya kupigwa mawe kutokana na imani za kishirikina.Kikongwe huyo na Maurus Zenda (46) anayedaiwa kuwa ni mwanaye kiukoo, kwa pamoja walijeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na baadhi ya ndugu zake kwa kuhisiwa kuhusika katika upotevu wa mtoto Adamu Mselewa (4).
Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia wa ukoo huo, hali ya bibi huyo bado ni mbaya na wanajitahidi kwa hali na mali kuokoa maisha yake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma alikolazwa.
“Bado hali ni mbaya, bibi bado analalamika maumivu, tunaendelea na matibabu huku tukisubiri madaktari watatueleza nini kuhusu maendeleo yake, ikishindikana hapa tutamhamisha hospitali, afadhali kidogo Maurus,” alisema mwanafamilia huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Mtoto wa kikongwe huyo.Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Mihayo Msekhela, waliwakamata watuhumiwa 10 kutokana na tukio hilo, ambao ni Ambros Mselewa (24) ambaye ni baba mzazi wa mtoto aliyepotea, Maria Zenda (45), Lameck Zenda (22), Pautas Komba (24), Fredy Mende (24), Gerord Ngonyani (27), Odilo Mwingira (21), Shadrack Ngonyani (22), Hilda Zenda(36) ambao wote ni wakazi wa Kijiji cha Muunganozomba.
Msikhela alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa moja asubuhi baada ya baba mzazi wa mtoto huyo, Ambros Mselewa akiwa pamoja na watu wengine walipoanza kuwashambulia watu hao wakimtaka kijana wao aliyepotea kimauzauza tangu Februari 3, mwaka hu

0 comments: