Mwanamke Amuua Mwanamke Mwenzake kwa Kummwagia Mafuta ya taa na Kumchoma Moto baada ya Kumfumania na Mumewe
Mkazi wa kijiji cha Ibosa, kata ya Nyakato, Bukoba Vijijini, Amelia Richard (50) anatuhumiwa kumuua mwanamke mwenzake kwa kummwagia mafuta ya taa na kumchoma moto baada ya kumfumania na mumewe.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe alitaja tukio hilo ni
la Februari 15, mwaka huu saa 3 usiku katika kijiji cha Ibosa kata ya
Nyakata Bukoba vijijini.
Alimtaja
aliyeuawa ni Pelagia Martin (46) aliyeunguzwa mwili mzima. Kamanda
alisema mwanamke huyo alicheleweshwa kufikishwa Hospitali ya Mkoa hadi
kesho yake; Februari 16 baada ya wanafamilia kuomba wayamalize bila
kwenda Polisi.
Makubaliano
ya wanafamilia hao yalitokana na kile kilichoonekana kwamba Amelia
alimfumania Pelagia akiwa na mumewe, Richard Bulebo (57) ndani ya
nyumba yao.
Kwa
mujibu wa Kamanda, Februari 16 walipoona hali ya majeruhi inazidi kuwa
mbaya, ndipo walifika katika Kituo cha Polisi mjini Kati wakiomba
msaada.
Polisi
walimpeleka majeruhi huyo Hospitali ya Mkoa lakini alifariki kabla ya
kupatiwa matibabu. Polisi inamshikilia Amelia na Bulebo kwa tuhuma za
kuhusika na mauaji hayo.
0 comments: