KUTEULIWA KWA Makonda NA Zelothe KUWA WAKUU WA WILAYA NI MKAKATI WA CCM kutengeneza mazingira ya kuchakachua kura za maoni
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuteua wakuu wa wilaya wapya 27 na wengine 19 kuondolewa, wadau mbalimbali wamejitokeza wakidai huo ni mkakati wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kutengeneza mazingira ya kuchakachua kura za maoni ili kiweze kushinda kwa urahisi.
Wadau
hao pia wamedai katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, chama
hicho kimekuwa na utaratibu wa kuteua viongozi hao waweze kutengeneza
mikakati ya ushindi katika maeneo yao.
Hata
hivyo, akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
CCM, Nape Nnauye, aliwashangaa wapinzani kwa kupinga uteuzi huo huku
akisisitiza kuwa lingekuwa jambo la ajabu kama wanasiasa hao
wangeupongeza.
“Ningeshangaa
kama wanasiasa wangesifia uteuzi huo…kwa sababu ndiyo uwezo wao wa
kufikiri uliopoishia, ninaomba Watanzania kuwasamehe bure,” alisema Nape
kwa kifupi.
Wakizungumzia
uteuzi huo mpya, baadhi ya wanasiasa akiwamo Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa Chama
cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, walisema hawaoni umuhimu wa
nafasi hizo wakidai uteuzi huo umelenga kuandaa timu ya uchakachuaji wa
kura katika uchaguzi mkuu na kura ya maoni ili kupitisha Katiba
Inayopendekezwa.
Walidai
uteuzi huo ni maandalizi ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu kwa sababu
nafasi hizo hazina umuhimu kwa taifa na kwamba hatua hiyo inaongeza
mzigo wa gharama kwa wananchi.
WASOMI
Baadhi ya wasomi kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini waliuita uteuzi huo kuwa ni wa siasa na umelenga kuhakikisha Katiba mpya inapita.
“Uteuzi huo ni wa siasa zaidi kuhakikisha CCM inashinda kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani,” alisema Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Ruaha Iringa.
Baadhi ya wasomi kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini waliuita uteuzi huo kuwa ni wa siasa na umelenga kuhakikisha Katiba mpya inapita.
“Uteuzi huo ni wa siasa zaidi kuhakikisha CCM inashinda kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani,” alisema Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Ruaha Iringa.
Profesa
Mpangala pia alitoa tahadhari kwa mteule wa Kinondoni ambaye pia
aliwahi kuwa mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Paul Makonda, akisema
kiongozi huyo ameteuliwa kimkakati ili kuhakikisha anasimamia
upitishwaji wa Katiba mpya katika eneo lake.
“Uteuzi
wa Paul Makonda umekuja kimkakati, lengo ni kuhakikisha Katiba
Inayopendekezwa inapita kwenye kura za maoni si vinginevyo.
“Ndiyo
maana Rais Kikwete amefanya mabadiliko hayo kwa sababu anajua kuwa
kinachofuata ni uchaguzi mkuu, lazima aangalie watu watakaoweza kutetea
maslahi ya chama chake,” alisema.
Alisema kutokana na hali hiyo, idadi kubwa ya waliochaguliwa wanafanya kazi kwa kufuata matakwa ya viongozi wao jambo ambalo linaweza kuwasaidia kupata ushindi.
Alisema kutokana na hali hiyo, idadi kubwa ya waliochaguliwa wanafanya kazi kwa kufuata matakwa ya viongozi wao jambo ambalo linaweza kuwasaidia kupata ushindi.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Hajji Semboja, alisema nafasi
ya ukuu wa wilaya ni ya siasa zaidi kwa vile haiangalii sifa ya mtu
anayeteuliwa kushika nafasi hiyo.
“Hizi
nafasi za U-DC na RC ni za wanasiasa zaidi ndiyo maana wanachaguliwa
bila kuangalia sifa ya mtu… hali ambayo imesababisha kuwapo malalamiko
mengi kutoka kwa wananchi.
“Yaani
kila nilipopita nasikia Makonda, Makonda…, nikajiuliza ni mtu wa aina
gani? Kumbe wanamtuhumu kwenye tukio la Jaji Joseph Warioba, nikajiuliza
kwanini aliteuliwa…ila nikapata jibu kwa sababu nafasi zenyewe zimetoka
kisiasa zaidi,” alisema Profesa Semboja.
Alisema
ili kupata viongozi bora, Serikali inapaswa kuwapa elimu ya uongozi ili
wakichaguliwa waweze kujua wajibu kwa wananchi na jinsi ya kujiheshimu.
WANAHARAKATI
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba, alisema hakuna kificho, pangua pangua na uteuzi huo wa ma-DC wapya una sababu maalumu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba, alisema hakuna kificho, pangua pangua na uteuzi huo wa ma-DC wapya una sababu maalumu.
Alisema
ni wazi wakuu hao wa wilaya wamechaguliwa kwa ajili ya kwenda
kushughulikia uchaguzi mkuu ujao utakaofanyia Oktoba, mwaka huu.
Sioni
sababu hasa iliyomfanya rais apangue wakuu wa wilaya katika kipindi
hiki ambacho tumebakiza miezi minane tufanye Uchaguzi Mkuu wa Rais,
Wabunge na Madiwani,” alisema Dk. Bisimba.
Mkurugenzi
wa shirika lisilo la kiserikali la SIKIKA, Irene Kiria, alisema hatua
hiyo ni gharama ambayo inahitaji fedha wakati katika huduma nyingine za
jamii Serikali imekuwa ikisema haina fedha.
“Gharama
zinakuja kwa kuwa ma-DC hao watahitaji kuhamishwa kwa wale
waliohamishiwa vituo vipya na wale wapya pia wana mahitaji yao zaidi.
“Kupangua wakuu hao ni kupoteza fedha za umma bure wakati kuna sekta zinazohitaji fedha kwa ajili ya mahitaji muhimu.
“Hili
suala la wakuu wa wilaya tumeshalizungumza mara nyingi, hata kwenye
rasimu ya pili ya Katiba iliyosimamiwa na Jaji Joseph Warioba ilitaka
watu hao wasiwepo, lakini tunandelea kuona fedha zinatumika kwa ajili
yao bila sababu ya msingi,” alisema.
MNYIKA
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), alisema kuhamishwa vituo kwa wakuu wengi wa wilaya miezi michache kabla ya kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa ni mkakati wa wakuu hao ambao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenda kupiga kampeni za ndiyo kwa Katiba haramu.
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), alisema kuhamishwa vituo kwa wakuu wengi wa wilaya miezi michache kabla ya kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa ni mkakati wa wakuu hao ambao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenda kupiga kampeni za ndiyo kwa Katiba haramu.
“Wakuu
wote ni wajumbe wa kamati za siasa za CCM, hivyo huu ni mkakati kwenda
kupiga kampeni za ndiyo kwa Katiba haramu iliyopitishwa kiharamia katika
Bunge Maalumu na baadaye kuhujumu upinzani kuelekea uchaguzi mkuu
kuliko ufanisi wa utendaji wa Serikali,” alisema Mnyika.
Akizungumzia
uteuzi wa aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi katika mikoa kadhaa, Zelothe
Steven, alisema utachochea wakuu wengine wa polisi kuhujumu upinzani.
“Uteuzi
wa Zelothe utaendelea kuchochea wakuu wengine wa polisi kuhujumu
upinzani katika kipindi cha utumishi wao kwa kujipendekeza kwa rais
ambaye pia ni amiri jeshi mkuu ili wakistaafu utumishi wao waendelee
kupata fadhila kupitia nafasi kama za ukuu wa wilaya,” alisema Mnyika.
0 comments: