MTOTO WA ANNA TIBAIJUKA AWATUKANA WATANZANIA HUKU AKIMTETEA MAMA YAKE KWA KUCHOTA PESA ZA ESCROW
Kagem Tibaijuka.
WAKATI Rais
Jakaya Kikwete akiwa amemuwajibisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka kufuatia kumegewa mgawo wa fedha za
Tegeta Escrow, binti anayedaiwa kuwa mwanaye, amejikuta akipata wakati
mgumu baada ya kumtetea mama yake kupitia mitandao ya kijamii.
Katika
Mtandao wa Twitter, binti huyo aliyejitambulisha kwa jina la Kagem
Tibaijuka, alimtetea mama yake akisema fedha zilizowekwa kwenye akaunti
yake zilikuwa ni safi na halali na kwamba ziliwekwa kwa nia njema ya
kuwasaidia kielimu watoto wa kike
“My
mum did nothing wrong except wanting to help young girls get an
education. A school built with my late father. Accepted a donation,”
(Mama yangu hakufanya kosa lolote isipokuwa alitaka kuwasaidia wasichana
kupata elimu. Shule ilijengwa na marehemu baba yangu. Mchango
ukakubaliwa)yalikuwa ni moja ya maneno yake katika mtandao huo wa
Twitter.
Aidha,
aliwashambulia wanawake walioonekana kushangilia wakati Rais Kikwete
alipotangaza kumuwajibisha mama yake, akiwaambia kuwa anawashangaa
kushangilia anguko la mwanamke mwenzao na kwamba hata wao iko siku
yatawakuta ya kuwakuta.
Lakini
katika mitandao mingine ya kijamii, ikiwemo Facebook na Jamii Forum
inayotembelewa na watanzania wengi, walimshambulia binti huyo kwa
kumwelezea kama mtu aliyelewa fedha na kwamba mama yake alistahili
kuondolewa kwenye nafasi yake, ikiwa ni pamoja na kushtakiwa.
Wachangiaji
walioonekana kuchukizwa na utetezi wa binti huyo kwa mama yake,
walisema licha ya Profesa Tibaijuka kuondolewa, pia watu wote
waliotajwa, wakiwemo Waziri Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu, Eliakim
Maswi nao walistahili kuondolewa katika nafasi zao.
Mtandao
huu ulimtafuta mama Tibaijuka kupitia simu zake mbili za mkononi, ili
kuzungumzia maoni yake baada ya kukutwa na ajali hiyo ya kisiasa pamoja
na kumuuliza kama Kagem ni bintiye, lakini moja iliyopatikana, iliita
kwa muda mrefu bila kupokelewa. Hata hivyo baadaye simu hiyo ilipopigwa,
ilionekana imezimwa.
Aidha
Kagem mwenyewe, ambaye ofisi zake zinadaiwa kuwa eneo la Kijitonyama
jijini Dar es Salaam, naye hakupokea simu yake ya mkononi aliyopigiwa na
hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, hakujibu.
Jumatatu
iliyopita, Rais Kikwete alizungumzia suala hilo la fedha zilizodaiwa na
Bunge kuwa ni za umma, kuchukuliwa isivyo halali katika akaunti
iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania. Wakati Mwanasheria Mkuu, Jaji
Frederick Werema alijiuzulu mwenyewe na mama Tibaijuka kuwajibishwa,
viongozi wengine waliodaiwa kuhusika na fedha hizo wanaendelea
kuchunguzwa na hatua stahiki dhidi yao zitachukuliwa.
0 comments: