Nimeamua Kutoka Kimapenzi na Binti wa Kazi ( Hausigeli) , Sina Jinsi… INGIA HAPA


Nina mke na watoto 3 wote tunafanya kazi. Tulipozaa mtoto wa pili wife alianza kupunguza umuhimu wa tendo la ndoa sijua ni kwa kuzoea au kuchoka.

Tumewekana vikao vyetu binafsi ili kila mmoja abainishe ni vichocheo gani vinakosekana ili tuviongeze kuboresha mchezo. Wote siyo walevi na tuko karibu kifamilia. 

  
Ukifuatilia labda mke wangu ana mtu sipewi taarifa zozote mbaya. Sasa tatizo ni kitu gani sijui. Ukimwuliza naye anakwambia mume wangu nivumilie nitajitahidi ila baada ya mwezi anarudi kule kule. 
  
Usipochombeza anaweza kupitiliza hata mwezi bila kukumbushia .

Hali hii imenisumbua kwa muda sana .Ili kuepuka kugombana na kuepuka kwenda nje kupata UKIMWI basi nikaamua nimweleze binti ambaye anatusaidia kazi nyumbani na akaonyesha kunisikitikia kwani mi si mtu wa baa useme ningetafuta huko na pia naogopa UKIMWI. 

  
Binti akasema anaweza kunisaidia lakini kwa masharti kwamba ataendelea kuniheshimu mimi pamoja na wife ili chochote kisishtukiwe.

Kwa mtazamo wangu hata kama mtaniona mjinga ni kwamba huyu binti anatumika kuokoa jahazi la sivyo ningekwenda huko na huko kutafuta viruka njia ambao wangeniweka mahali pabaya zaidi. 

  
Tumeanza mahusiano vizuri na tunaendelea kiasi kwamba hata wife asipokuwa tayari mwezi mzima sipati shida na hii imenisaidia kuepuka ugomvi uliokuwa unatokana na tendo la ndoa kutokuwa zuri. 
  
Je wadau katika hali kama hii ambayo mke anakuwa namna hii kwa ninachokifanya nimekosea au niko sawa??
  
Kama unafikiri nimekosea nipe ushauri kuhusu njia mbadala na jiweke kwenye hali yangu  kabla  hujazungumza chochote.

0 comments: