Nyalandu atangaza rasmi kugombea Urais kupitia CCM 2015 HABARI KAMILI IPO HAPA
WAZIRI wa maliasili na utalii na mbunge wa jimbo la Singida kaskazini(CCM) ,Lazaro Samwel Nyalandu, ambaye ametangaza rasmi kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.
WAZIRI
wa maliasili na utalii na mbunge wa jimbo la Singida kaskazini(CCM)
,Lazaro Samwel Nyalandu,ametangaza rasmi nia ya kugombea nafasi ya urais
katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Nyalandu ametangaza nia hiyo leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ilongero Jimbo la Singida kaskazini.
Alisema
baada ya kutafakari kwa muda mrefu na kujikagua kwa kina,ameona anao
uwezo wa kutosha wa kuweza kupokea kijiti kutoka kwa rais anayemaliza
muda wake mwakani kwa mujibu wa katiba.
“Kujikagua
huko ni pamoja na kutafakari jinsi alivyoweza kutekeleza ilani ya
uchaguzi ya CCM katika vipindi vitatu (miaka 15) akiwa mbunge wa jimbo
la Singida kaskazini.Katika kipindi hicho cha ubunge,nimeweza kutumia
zaidi ya shilingi bilioni mbili katika kufanikisha kuchangia miradi ya
maendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo za afya,maji na
barabara”,alisema Nyalandu.
Alisema
wakati ukifika,Watanzania kutoka sehemu mbalimbali za nchi wakiongozwa
na wakazi wengi wa kutoka jimbo la Singida kaskazini,kwenda Dodoma
kuchukua fomu za kuwania urais.
“Watanzania
waliokwisha onyesha nia ya kuwania urais mwakani,nawaomba sote
tuonyeshe kazi tulizozifanya katika kuwahudumia Watanzania,ili waweze
kutupima vizuri waweze kujijengea mazingira mazuri ya kuchangua rais
atakayewafaa kwa kuwaletea maendeleo endelevu”,alisema.
Nyalandu
alisema kuwa anakishukuru Chama Cha Mapinduzi,kwa maandalizi yake
mazuri ya kuhakikisha chama kinapata mwanaCCM safi,mwadilifu na mchapa
kazi atakayepeperusha bendera ya chama katika kinyang’anyiro cha kuwania
urais mwakani.
chanzo: gazeti la mwananchi
0 comments: