Simba yamsajili beki wa Mtibwa. Ingia Hapa Kwa Habari Kamili

hassan kessy

Katika usiku ambao umekuwa na movement nyingi za wachezaji na makocha , klabu ya Simba imekamilisha usajili wa beki wa pembeni toka timu ya Mtibwa Sugar Hassan Kessy .
Beki huyo ambaye ametokea kuwa moja kati ya wachezaji wa kutmainiwa kwenye klabu hiyo ya wakata miwa wa huko Manungu Turiani mkoani Morogoro anaungana na wachezaji wapya waliosajiliwa katika kipindi hiki cha dirisha dogo ambao ni Simon Sserunkuma , Danny Sserunkuma , na Juko Murshid wote toka Uganda .
Kessy ambaye ametajwa kuwa moja kati ya wachezaji wanaokaribia kutiwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars aliicheza Mtibwa kwa mara ya mwisho katika mchezo wa kirafiki ambao ilifungwa na Azam Fc 3-1 .
Beki huyu anasajiliwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu yaliyofanyika chini ya usimamizi wa viongozi wa Simba wakiongozwa na Geoffrey Nyange Kaburu na Kiongozi wa Mtibwa Jamal Bayser .
Tetesi zaidi zinasema kuwa Simba imemsajili beki huyo kwa thamani ya shilingi milioni 30 .

0 comments: