Uganda In Burundi Out ndani ya Simba Sc. Soma Hapa Kwa Habari Kamili

simba okwi

Ni kama vile klabu ya Simba ina mapenzi na taifa la Uganda baada ya klabu hiyo kukamilisha jumla ya wachezaji watano raia wa kigeni ambao wanatoka kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki .

Simba imetangaza na kuthibitisha kuwa wachezaji wake watano wa kigeni kwa msimu huu ni Emmanuel Okwi, Daniel Serunkumma, Simon Serunkumma, Joseph Owino na Juko Mursheed.
Emmanuel Okwi na Joseph Owino ni wawili kati ya wachezaji watano raia wa Uganda walioko Simba.
Emmanuel Okwi na Joseph Owino ni wawili kati ya wachezaji watano raia wa Uganda walioko Simba.
Wachezaji wawili kati ya hao (Okwi na Owino ) na watatu wengine (Serunkumma Simon, Dany na Juko) wamesajiliwa katika kipindi hiki ambapo dirisha dogo la usajili liko wazi.
Nafasi za wachezaji watatu hao raia wa Uganda zimekuja kujaza nafasi za wachezaji wawili toka Burundi ambao ni Amisi Tambwe na Pierre Kwizera pamoja na Mkenya Paul Mungai Kiongera .
Dnny Sserunkumma ni raia mwingine wa Uganda aliyeko Simba.
Danny Sserunkumma ni raia mwingine wa Uganda aliyeko Simba.
Kiongera bado ataendelea kuwa mchezaji wa Simba hadi atakapopona jeraha lake la goti ambapo amekwenda kufanyiwa upasuaji nchini India huku Tambwe na Kwizera wakiwa wameachwa moja kwa moja .
Mrundi  Perre Kwizera ameachwa baada uongozi wa Simba kutoridhishwa na kiwango chake.
Mrundi Perre Kwizera ameachwa baada uongozi wa Simba kutoridhishwa na kiwango chake.

Mkenya Paul Kiongera ameachwa japo Simba itamtumia msimu ujao.
Mkenya Paul Kiongera ameachwa japo Simba itamtumia msimu ujao.
Mrundi mwingine aliyeachwa ni mfungaji bora wa msimu uliopita Amisi Tambwe.
Mrundi mwingine aliyeachwa ni mfungaji bora wa msimu uliopita Amisi Tambwe.

0 comments: