WEMA SEPETU AKIFUNGUKA JUU YA MAHUSIANO YAKE YA KIMAPENZI KWA SASA.

0 comments

Wema Sepetu amechoka uhusiano wa boyfriend na girlfriend. Muigizaji hiyo wa filamu amesema anataka kuolewa.
Wema alisema hayo jana kwenye reality show yake, In My Shoes baada ya meneja wake Martin Kadinda kumuuliza kwanini hana ‘kiki’ kwa sasa.


Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 alisema kuna vitu vingi anataka kuvifanya ikiwemo kuwa na hamu ya kutulia na kuwa mke wa mtu.
Hata hivyo Wema alisita kumweka wazi mwanaume anayetaka kumweka ndani na kumtaka meneja wake kuwa na subira

Read More »

HUYU NDIYE MREMBO ALIYE SHINDA TAJI LA MISS RWANDA 2015 NI BALAAAAA

0 comments

Doriane Kundwa, 19years old and student from the Northern Province of Rwanda, was crowned as the MISS RWANDA 2015 beating 14 other contestants. She was given a Suzuki Swift and will receive a monthly salary of $1000 during her reign. She also became brand ambassador for telecommunications company Airtel. Eish!! Here are the photos of the beautiful young lady
Doriane Kundwa, 19years old and student from the Northern Province of Rwanda, was crowned as the MISS RWANDA 2015 beating 14 other contestants. She was given a Suzuki Swift and will receive a monthly salary of $1000 during her reign. She also became brand ambassador for telecommunications company Airtel.
Eish!! Here are the photos of the beautiful young lady……




Read More »

MZAZI MWENZA WA MBUNGE MAARUFU WA CHADEMA MH. SUGU APOST TENA PICHA YA UTATA INSTAGRAM ONA NA ALICHOSEMA LIVE!!

0 comments



"Napenda kukaa uchi- kabisa yaani # Kama ni tatizo au kilema ninacho - nimekubali#"


Read More »

Unaletwa karibu zaidi na video mpya ya Izzo Bizness Ft Shaa ‘Kidawa’ INGIA HAPA KUITAZA

0 comments
izzo b
Hii video mpya ya Izzo Bizness amefanya wimbo na Shaa, unaitwa ‘Kidawa’ Video imeongozwa na Nick Dizzo wa Focus Films,Tanzania . Audio imetayarishwa na Dupy wa Uprise Music na kuwa Mastered na Master J pale MJ records Dar es Salaam, Tanzania.
BONYEZA HAPA CHINI KUITAZAMA VIDEO

Read More »

ANT EZEKEL ASHUSHA MANENO MACHAFU

0 comments
Mrembo na mwigizaji wa filamu za kibongo, Aunt ezekiel amejikuta akitoa maneno makali baada ya mashabiki wake kumshabulia kwa maneno baada ya kuweka mtandaoni picha ikimuonyesha amevalia kinguo ambacho kwa maoni ya mashabiki hao hakistahili kuvaliwa na mwanamke mjamzito na kibaya zaidi alionekana mkononi ameshika shupa ambao wengi waliiona kama niyakilevi.

Aunty Ezekiel alibandika picha hiyo hapo juu hivi juzi kati akiwa na jamaa kwenye ukurasa wake mtandaoni na kuandika maneno “My best friend,my love,my kimoko I love him so much”
 
Baada ya kubandika ujumbe huo baadhi ya mashabiki wake walionyeshwa kukera na mavazi na sehemu alikokuwepo nalumtaka atulie nyumbani alee mimba yake kwani kwasasa inaonekana kuwa na ya zaidi ya miezi nane na wiki kadhaa.


“Ungetulia  tu nyumbani ukasubirikujifungua salamamjamzito kuzurura namna hiyo na mijanaume sio poakabisa tena na kilaji mkononi harafu pia hata hayo mavazi mmmh!!” alisema mmoja wa shabiki na kuungwa mkono na wengine wengi.
 
Baada ya muda kidogo aunty ezekel akaibuka na  kuandika ; “Plz msiwe bac mnaongea kitu kabla ujajua undani wake, ni vizuri kuuliza kuliko kuandika tu ilimradi na wewe uonekane umeongea hiyo nguo ni special kwa mama mjamzito na hapo juu inampira wakutosha tu na mapajani ndio inabana sasa”
Lakini majibu hayo yalionekana kuamsha maneno zaidi ya kumponda Aunty ambae nae mwishoni  alionekana kushindwa kuvumilia na kutoa maneno machafu ambayo sio busara kuyabandika hapa.

Wewe je umeionaje picha hiyo ya Aunty?

Read More »

WAPI TUNAELEKEA BINTI ATUPIA PICHA TATA MTANDAONI WAKUBWA TU

0 comments

00Ps!! ladies have gone crazy to seek attention! They will do anything to win men who will say they are hot or try to engage them in talks.A lady cannot believe she is hot unless she has several who are trying to win her.They will do anything on social media to attract men.This is a Kenyan lady posting n’ude pics on social media to seek men who will appreciate her beauty.This is crazy






Read More »

Nay Wa Mitego na Diamond Platnumz studio tena,ni collabo nyingine

0 comments
tru b
Wasanii waliofanya #VituAmazing na wimbo wao wa Muziki Gani wamekutana tena studio kwaajili ya rekodi nyinine. Ni Diamond na Nay wa Mitego. Diamond kwa sasa anang’ara na rekodi ya Ntampata wapi ambayo inapewa muda mkubwa wa hewani kwenye vitui vya kimataifa ka Trace Tv huku Nay akifanya vizuri na rekodi na video yaAkadumba
nay 1 nay


Read More »

Na Producer wa collabo nyingine ya Diamond Platnumz na Nay wa Mitego ni..

0 comments
Studio
Tudd Thomas ndiye producer atakaye simamia kazi mpya ya wasanii Diamond Platnumz na Nay wa Mitego, Walikesha usikuwa wa kuamkia 19 Feb 2015. Wimbo utafanyika Surround Studios.
thomas 2 thomas


Read More »

Jibu la Amber Baada ya Kanye West kusema alibidi aoge mara 30 ili kuwa na Kim Kardashian baada ya kuwa na Amber Rose.

0 comments
amber-responds-to-kanye__oPt
Kwenye mahojiano na kipindi cha ‘BreakFast Club’ Kanye West alimkejeli mpenzi wake wa zamani Amber Rose kwa kusema alibidi aoge mara 30 baada ya kuwa naye ili Kim kardashian awe naye.
Kanye West alisema “Kim k angekubali kuwa na mimi kabla ya Amber basi nisinge kuwa na Amber Kabisa, ni ngumu kwa mwanamke kuwa na mwanaume aliyewahi kuwa na mahusiano na Amber, nilibidi nioge mara 30 ili Kim K anikubali”.
Amber amejibu kupitia twitter yake nakusema …
amber jibu


Read More »

Home » Ent. » Jinsi mitandao ya Nigeria ilivyoshindwa kutafsiri jina la wimbo wa Iyanya ft Diamond ‘Nakupenda’ kwa kingereza January Makamba - Tanzania Mpya Jinsi mitandao ya Nigeria ilivyoshindwa kutafsiri jina la wimbo wa Iyanya ft Diamond ‘Nakupenda’ kwa kingereza

0 comments
.
.


Mitandao hiyo ilikuwa ikitafsiri jina la wimbo huo unaoitwa Nakupenda kwa lugha ya Kingereza kama Marry Me, Remember, ambapo tafsiri sahihi la neno Nakupenda ni I LOVE YOU.
Hii ni baadhi ya mitandao ambayo imeonekana kushindwa kutafsiri jina la wimbo huo kwa lugha ya kingereza  ikiwemo, Uncova.com, audiomack.com, Feva tv.com, tooxclusive.com, jaguda.com, naijaurban.com na mengineyo.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Read More »

Watu wenye ulemavu wa ngozi kuandamana hadi Ikulu

0 comments
 
 
Akiongea na waandishi wa habari afisa habari wa TAS Josephat Tonner amesema kuwa ni dhamira ya chama kujua kwa nini serikali imeendelea kuangalia vitendo vya kikatili wanavofanyiwa watu wenye albinism nchini huku vitendo hivyo vikiendelea.
Aidha, katika hali isiyo ya kawaida majira ya saa nne na robo leo asubuhi mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mwalimu Mussa aliamua kutembea bila nguo katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi eneo la daraja la salenda mpaka barabara ya Kenyata jijini
Dar es Salaam huku watu wakimtazama na kupita bila kujali.
Hali hiyo iliwalazimu badhi ya watu kuchukua hatua za kumvisha nguo kijana huyo huku wakielezea kuwa ni kukosekana kwa utu kwa watu kumpita hasa watu waliopewa dhamana ya ulinzi wa binadamu bila kuchukua hatua yeyote, huku kijana huyo akieleza mkasa uliomfanya ateembee uchi wa mnyama.

Read More »

PAUL MAKONDA AWABWATUKIA WANAOPONDA YEYE KUTEULIWA KUWA MKUU WA WILAYA

0 comments
Makonda ang’aka 
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni , Paul Makonda (pichani) amesema wanaobeza uwezo wake kiutendaji baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo, wasubiri waone atakavyokuwa.



Aidha, ameweka wazi kile anachoamini anashutumiwa na kubezwa na watu kuhusu uteuzi huo na kusema wanaofanya hivyo, wanafahamu kwamba masuala yao kadhaa ndani ya wilaya hiyo yanayokwenda kinyume na taratibu, hayatafanikiwa.


Akiendelea kujibu wanaoshutumu uteuzi wake kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, alisema kwa sasa hawezi kutoa ahadi ni nini atafanya isipokuwa, anasubiri kuingia ofisini.


Akihojiwa katika kipindi cha asubuhi cha Redio ya Clouds, alisema pia anamsikiliza Rais atakachomwambia afanye kwa kuwa yeye ni mwakilishi wake wilayani humo.


Akizungumzia kuhusu taarifa za kupata nafasi hiyo kuwa gumzo katika jiji kuliko wakuu wengine wa wilaya, alisema inaonesha ni kwa jinsi gani watu wanatambua utendaji wake.


Alisema alipata taarifa za uteuzi huo wakati akitoa mada katika kikao cha kazi cha Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na kushangaa watu wakipeana taarifa.


“Kuna watu wanabeza uteuzi wangu kwa kuonekana nimepewa wilaya kubwa. Nataka kuwaambia wasubiri waone tu,” alisema na kutaka Watanzania kuacha tabia ya kumjadili mtu au jambo bila kufahamu vizuri.


Alisisitiza kuwa Watanzania wamekuwa na tabia ya kushabikia jambo wasilolijua au mtu wasiyemjua kwa kufuata mkumbo; jambo ambalo siyo zuri ni vyema kufahamu kwanza ndipo uweze kusema.

Akizungumzia baadhi ya vyombo vya habari vilivyotoa taarifa za uteuzi wake kwa kumdhihaki, alisema wamefanya hivyo kwa maslahi yao ya kuuza.


Pia alielezea uteuzi wake umekuwa gumzo, kutokana na uwezo wake wa kazi katika UVCCM pamoja na uwezo wake kwenye Bunge Maalumu la Katiba.


Uteuzi wa Makonda ambao umefanywa na Rais Kikwete, unaonesha kuwashitua wengi; hali ambayo imefanya watu wengi kumbeza hasa kupitia mitandao ya kijamii.


Baadhi ya wanaobeza, wanadai kwamba Makonda hana sifa ya kuongoza wilaya kubwa kama Kinondoni, ambayo ina changamoto na migogoro mingi ya ardhi.


Makonda ambaye ni Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa UVCCM, jina lake limekuwa kubwa hivi karibuni baada ya kutuhumiwa kushiriki kuvuruga mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, tuhuma alizokanusha.


Pia, kujitokeza kwake hadharani kumpinga mmoja wa watu wanaotajwa kuwania urais, kuliongeza jina hilo kuwa maarufu. Maisha ya Makonda pia ambaye baada ya kushindwa Umakamu Mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM, alitoa shutuma kuhusu uchaguzi huo na baadaye alirejeshwa ndani ya umoja huo kwa kupewa nafasi anayoshikilia sasa ya ukatibu wa uchipukizi na uhamasishaji.

Read More »

Picha kutoka Msibani Dodoma Nyumbani kwa Kina Mez B

0 comments







Read More »

'Sangoma' akutwa akimiliki SMG, risasi nane

0 comments
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha

Mganga wa kienyeji, Zacharia Ngobeko (35),  amekamatwa na polisi mkoani hapa baada ya kukutwa akimiliki SMG na risasi nane kinyume cha sheria.
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 1 jioni, baada askari polisi kufanya msako nyumbani kwake na kukamata silaha hiyo ikiwa na risasi zilizokuwamo kwenye magazine.
 
Kamugisha alisema baada ya kumhoji, alidai silaha hiyo ilitumika kufanya mauaji mbalimbali yakiwamo ya kumuua, Mary Kashidye, Februari 8, mwaka huu, kwa kumpiga risasi kutokana na ugomvi wa kiwanja kati yake na Jumanne Maige.
 
Aidha, alisema mauaji hayo yalifanyika baada ya kukodiwa vijana wawili, Andrew Buteye (38) na Daudi Luchemela (40), kutekeleza mauaji hayo, kisha kurejesha silaha hiyo kwa mganga huyo.
 
Kamanda Kamugisha alisema silaha hiyo kupitia vijana hao ilitumika katika tukio la unyang’anyi wilayani Kahama baada ya kumpora Manyangu Mboje, Sh. Milioni 1.5, dukani kwake Februari 13, mwaka huu.
 
Hata hivyo, alisema baada ya kuwahoji watuhumiwa wote walikiri kuhusika na matukio hayo ya mauaji na unyang’anyi kwa kutumia SMG hiyo na kisha kuihifadhi kwa mganga huyo huku wakikiri kufanya matukio mengine mkoani Mbeya mwaka 2010 na 2012.
 
Alisema watuhumiwa hao, pia walikiri kufanya uhalifu wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza 2014, kwa kupora Sh. milioni 39. Watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo kujibu mashitaka yanayowakabili.

Read More »

Kim Kardashian Ajianika Mtupu Kama Alivyozaliwa ..hii inawahusu wenye umri kuanzia WAKUBWA TU WATOTO MWIKO

0 comments

Msaanii  wa  Kike  Kim Kardashian   ambaye  ni  mke  wa  mwanamuziki  Kanye  West  na  mama  wa  mtoto  mmoja  hivi  karibuni  alikubali  kupigwa  picha  za  utupu  kama  alivyozaliwa  kwa  ajili  ya  kurasa  za  mbele  za  gazeti  la  Love  Magazine.....


Kuona Picha  zote  na  maelezo  ya  kina......Bofya  hiyo  picha  ya  chini  ambayo  Nimeififisha  kulinda  maadili  yetu.





Read More »

SIASA: Aliyetemwa ukuu wa wilaya ya Igunga ageukia ubunge

0 comments
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu. 
Siku moja baada ya uteuzi wake kutenguliwa na Rais Jakaya Kikwete, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu amesema sasa anageukia ubunge katika Jimbo la Singida Magharibi.
Kingu alisema siku nyingi alikuwa na shauku ya kugombea ubunge katika jimbo hilo, kwamba kuondolewa katika wadhifa huo kutampa nafasi ya kujipanga na kuhakikisha anashinda jimbo hilo linaloongozwa na Mohamed Hamisi Missanga (CCM).
“Unajua kwa muda sasa akili yangu ilijikita zaidi katika ubunge ili niweze kuwasaidia wananchi kwa ukaribu zaidi. Wananchi wa Jimbo la Singida Magharibi wamekaa muda mrefu bila kupata mtu wa kutatua matatizo yanayowakabili,” alisema.    
Alifafanua kuwa Februari 28, mwaka huu atafanya mkutano mkubwa wa hadhara katika jimbo hilo, ataitumia siku hiyo kutangaza rasmi nia yake ya kugombea ubunge.
“Nitakachokifanya sasa ni kuwa karibu zaidi na wananchi na kuhakikisha matatizo yanayowakabili ninayajua kiundani ili niweze kuyatatua kwa urahisi,” alisema.
Aliongeza, “Namshukuru Rais Kikwete kwani aliniamini na kazi aliyonipa niliifanya kwa uaminifu na uzalendo wa hali ya juu, kufanikiwa kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo, afya, mifugo, uvuvi na maendeleo kwa vijana,” alisema Kingu (pichani).
 “Rais ameamua nipumzike na ninamshukuru kwa uzalendo wake mkubwa naamini bado ana imani kubwa  na mimi.”
Akitoa ushauri wa wakuu wapya wa wilaya alisema, “Wanatakiwa kuhakikisha wanamsaidia kazi Rais Kikwete na kutekeleza ilani.”
Wakati Kingu akieleza hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Musoma.
Alisema:  “Sina maneno mengi kwa sasa nitasema kauli tatu; Asante kwa pongezi yako, namshukuru Mwenyezi Mungu, namshukuru sana Rais Kikwete kwa kuniteuwa kushika wadhifa huu.”
Kwa upande wake Martha Umbulla aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, alipotafutwa siku nzima ya jana alisema kuwa yupo katika kikao na kuahidi kuzungumzia uteuzi huo baada ya kumalizika kwa kikao, jambo ambalo hakulitekeleza.

Wilaya ya Kiteto ni moja kati ya wilaya zilizokithiri migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, iliyosababisha watu zaidi ya 10 kuuawa na wengine kujeruhiwa.
Akizungumzia uteuzi huo Naibu Katibu Mkuu wa Chadema- Bara, John Mnyika alisema unadhihirisha kuwa  nchi ina mifumo legelege ya kupima wanaopendekezwa kuteuliwa kabla ya uteuzi.
“Uteuzi huu unapaswa kuibua mjadala wa haja ya kufuta wadhifa wa ukuu wa wilaya. Watanzania wanatakiwa kuikataa Katiba Inayopendekezwa kwa sababu imependekeza vyeo vya wakuu wa wilaya ambavyo vipo kwa ajili ya kufanya hujuma na kuiba kura katika chaguzi,” alisema.
Hata hivyo, mkurugenzi wa masomo ya shahada ya kwanza kutoka Chuo cha Usimamaizi wa Fedha (IFM), Dk Shaban Ngole alisema kuwa mabadiliko yaliyofanywa kwa wakuu wa wilaya yanalenga kukiimarisha chama tawala baada ya tathmini ya matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Ndiyo maana unaweza ukaona kuwa wapo baadhi ya watu ambao wanazua maswali katika jamii, mfano, uteuzi wa Paul Makonda hauna kitu kingine zaidi ya kuongeza ushawishi wa chama katika Wilaya ya Kinondoni. Chama kimeona kuwa anaweza kuhimili mikikimikiki ya hapa mjini,” alisema Dk Ngole.
Alifafanua kuwa Makonda anaeleweka kuwa ni kada wa CCM ambaye hajifichi kutokana na utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya chama hicho, hivyo kuteuliwa kwake hakuwezi kuwa na maana nyingine.
Licha ya kukiimarisha chama, Dk Ngole alisema kuwa Serikali ina dhamira ya kuongeza ufanisi katika utendaji wake. Hilo limeisukuma kufanya mabadiliko ya msingi ili kujiongezea nafasi ya ushawishi miongoni mwa wananchi.

Read More »

MZEE MAJUTO NA WASANII WENZAKE WAMTEMBELEA MAMA ALIYEPOKONYWA MTOTO ALBINO NA KISHA KUUWAWA KIKATILI

0 comments



Read More »

KUTEULIWA KWA Makonda NA Zelothe KUWA WAKUU WA WILAYA NI MKAKATI WA CCM kutengeneza mazingira ya kuchakachua kura za maoni

0 comments
nape
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuteua wakuu wa wilaya wapya 27 na wengine 19 kuondolewa, wadau mbalimbali wamejitokeza wakidai huo ni mkakati wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kutengeneza mazingira ya kuchakachua kura za maoni ili kiweze kushinda kwa urahisi.
Wadau hao pia wamedai katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, chama hicho kimekuwa na utaratibu wa kuteua viongozi hao waweze kutengeneza mikakati ya ushindi katika maeneo yao.
Hata hivyo, akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, aliwashangaa wapinzani kwa kupinga uteuzi huo huku akisisitiza kuwa lingekuwa jambo la ajabu kama wanasiasa hao wangeupongeza.
“Ningeshangaa kama wanasiasa wangesifia uteuzi huo…kwa sababu ndiyo uwezo wao wa kufikiri uliopoishia, ninaomba Watanzania kuwasamehe bure,” alisema Nape kwa kifupi.
Wakizungumzia uteuzi huo mpya, baadhi ya wanasiasa akiwamo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, walisema hawaoni umuhimu wa nafasi hizo wakidai uteuzi huo umelenga kuandaa timu ya uchakachuaji wa kura katika uchaguzi mkuu na kura ya maoni ili kupitisha Katiba Inayopendekezwa.
Walidai uteuzi huo ni maandalizi ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu kwa sababu nafasi hizo hazina umuhimu kwa taifa na kwamba hatua hiyo inaongeza mzigo wa gharama kwa wananchi.
WASOMI
Baadhi ya wasomi kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini waliuita uteuzi huo kuwa ni wa siasa na umelenga kuhakikisha Katiba mpya inapita.
“Uteuzi huo ni wa siasa zaidi kuhakikisha CCM inashinda kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani,” alisema Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Ruaha Iringa.
Profesa Mpangala pia alitoa tahadhari kwa mteule wa Kinondoni ambaye pia aliwahi kuwa mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Paul Makonda, akisema kiongozi huyo ameteuliwa kimkakati ili kuhakikisha anasimamia upitishwaji wa Katiba mpya katika eneo lake.
“Uteuzi wa Paul Makonda umekuja kimkakati, lengo ni kuhakikisha Katiba Inayopendekezwa inapita kwenye kura za maoni si vinginevyo.
“Ndiyo maana Rais Kikwete amefanya mabadiliko hayo kwa sababu anajua kuwa kinachofuata ni uchaguzi mkuu, lazima aangalie watu watakaoweza kutetea maslahi ya chama chake,” alisema.
Alisema kutokana na hali hiyo, idadi kubwa ya waliochaguliwa wanafanya kazi kwa kufuata matakwa ya viongozi wao jambo ambalo linaweza kuwasaidia kupata ushindi.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Hajji Semboja, alisema nafasi ya ukuu wa wilaya ni ya siasa zaidi kwa vile haiangalii sifa ya mtu anayeteuliwa kushika nafasi hiyo.
“Hizi nafasi za U-DC na RC ni za wanasiasa zaidi ndiyo maana wanachaguliwa bila kuangalia sifa ya mtu… hali ambayo imesababisha kuwapo malalamiko mengi kutoka kwa wananchi.
“Yaani kila nilipopita nasikia Makonda, Makonda…, nikajiuliza ni mtu wa aina gani? Kumbe wanamtuhumu kwenye tukio la Jaji Joseph Warioba, nikajiuliza kwanini aliteuliwa…ila nikapata jibu kwa sababu nafasi zenyewe zimetoka kisiasa zaidi,” alisema Profesa Semboja.
Alisema ili kupata viongozi bora, Serikali inapaswa kuwapa elimu ya uongozi ili wakichaguliwa waweze kujua wajibu kwa wananchi na jinsi ya kujiheshimu.
WANAHARAKATI
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba, alisema hakuna kificho, pangua pangua na uteuzi huo wa ma-DC wapya una sababu maalumu.
Alisema ni wazi wakuu hao wa wilaya wamechaguliwa kwa ajili ya kwenda kushughulikia uchaguzi mkuu ujao utakaofanyia Oktoba, mwaka huu.
Sioni sababu hasa iliyomfanya rais apangue wakuu wa wilaya katika kipindi hiki ambacho tumebakiza miezi minane tufanye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani,” alisema Dk. Bisimba.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la SIKIKA, Irene Kiria, alisema hatua hiyo ni gharama ambayo inahitaji fedha wakati katika huduma nyingine za jamii Serikali imekuwa ikisema haina fedha.
“Gharama zinakuja kwa kuwa ma-DC hao watahitaji kuhamishwa kwa wale waliohamishiwa vituo vipya na wale wapya pia wana mahitaji yao zaidi.
“Kupangua wakuu hao ni kupoteza fedha za umma bure wakati kuna sekta zinazohitaji fedha kwa ajili ya mahitaji muhimu.
“Hili suala la wakuu wa wilaya tumeshalizungumza mara nyingi, hata kwenye rasimu ya pili ya Katiba iliyosimamiwa na Jaji Joseph Warioba ilitaka watu hao wasiwepo, lakini tunandelea kuona fedha zinatumika kwa ajili yao bila sababu ya msingi,” alisema.
MNYIKA
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), alisema kuhamishwa vituo kwa wakuu wengi wa wilaya miezi michache kabla ya kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa ni mkakati wa wakuu hao ambao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenda kupiga kampeni za ndiyo kwa Katiba haramu.
“Wakuu wote ni wajumbe wa kamati za siasa za CCM, hivyo huu ni mkakati kwenda kupiga kampeni za ndiyo kwa Katiba haramu iliyopitishwa kiharamia katika Bunge Maalumu na baadaye kuhujumu upinzani kuelekea uchaguzi mkuu kuliko ufanisi wa utendaji wa Serikali,” alisema Mnyika.
Akizungumzia uteuzi wa aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi katika mikoa kadhaa, Zelothe Steven, alisema utachochea wakuu wengine wa polisi kuhujumu upinzani.

“Uteuzi wa Zelothe utaendelea kuchochea wakuu wengine wa polisi kuhujumu upinzani katika kipindi cha utumishi wao kwa kujipendekeza kwa rais ambaye pia ni amiri jeshi mkuu ili wakistaafu utumishi wao waendelee kupata fadhila kupitia nafasi kama za ukuu wa wilaya,” alisema Mnyika.

Read More »

Precision air yafirisika...sasa kuuza ndege zake

0 comments
Precision_Air_ATR_42-600_(5H-PWH)_at_Toulouse-Blagnac_Airport_(LFBO)
SHIRIKA la Ndege la Precision linatarajia kuuza baadhi ya ndege zake na kubakiza ndege sita kupunguza mzigo wa madeni yanayoikabili Kampuni hiyo kwa sasa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo, Michael Shirima alisema Dar es Salaam jana kuwa hatua hiyo imefikiwa kutokana na uchakavu wa ndege hizo na hali ya uchumi wa kampuni.


“Kampuni iko katika mazungumzo na mwekezaji ili kukamilisha makubaliano ya kununua ndege zenye madeni na kisha kuzikodisha kwa kampuni nyingine… makubaliano haya yanatarajiwa kufikiwa mwishoni mwa robo ya kwanza ya mwaka huu,” alisema Shirima.


Alisema pamoja na kufikia hatua hiyo kampuni haijakata tamaa kwa kuweka jitihada ya kutafuta mtaji mkubwa kupitia kwa wanahisa wa sasa au wawekezaji wasio wanahisa.


Awali akiitoa taarifa katika mkutano mkuu wa mwaka wa Tatu wa wanahisa, Shirima alisema mazingira ya biashara yalikuwa na ushindani huku kukiwa na hofu juu ya usalama duniani kote.


Pia alisema thamani ya fedha za kigeni hususan Dola ya Marekani imeendelea kukua ikilinganisha na shilingi ya Tanzania hivyo kusababisha akiba hafifu ya fedha za kigeni na hasara kwa biashara ambazo matumizi yake mengi yanategemea fedha hizo.

Read More »